ÈÓã Çááå ÇáÑÍãä ÇáÑÍíã
Mirza Ahmad: “Mtamani pesa
wa Qadiani”
Mwasisi wa dini ya
Ahmadiya
Aliogopa Ufukara
Aliwataka wafuasi wake
wamtii Malkia Viktoria
Na. Dk. Rashid Ali
Historia inabainishia kwamba, mitume
walikuja kuwakomboa watu kutokana
na utumwa wa aina zote tangu ule wa minyororo hadi wa tamaa za nafsi, ili kuwafanya wawe huru wanaomtii na
kumtumikia Allah, ambako kutawapelekea wafikie kilele cha amani katika ulimwengu
huu na ujao.
Kwa ajili hiyo, Mitume hawakupigania kujilimbikizia
mali wakilenga kuishi kwa wasaa na starehe, hawakufanya hivyo kwao binafsi wala
kwa wafuasi wao. Kwa mfano, usiku wa siku ya aliyokufa mtume(s.a.w), hata taa
nyumbani kwake haikuwa na mafuta.
Kinyume na uchaMungu huo waliokuwa nao Mitume, wapo
wadanganyifu wanaowadanganya wanaadamu kwa jina la dini, wakilenga kujipatia
mali ili waishi vizuri. Watu hawa hawauzi tu imani yao kwa starehe ndogo za
ulimwengu huu bali kibaya wanachouzia nafsi zao ni kuwajibika kwao katika
kuharibu imani za wale ambao kwa bahati mbaya wametumbukia katika hadaa zao za
kidini.
Katika toleo hili la Fatwa, Mwandishi amelenga
kufichua vipengele vyote ya maisha ya
mmoja wa Wadanganyifu(matapeli) wa kidini aitwaye Mirza Ghulam Ahmad
Qadiani, Mwasisi wa Jamaat Ahmadiya ambaye kwa tamaa ya kujipatia pesa,
amepoteza wengi, na tutaonesha pia ni kwa kiasi gani amejikhasirisha yeye
mwenyewe.
Baada ya kuyasoma makala haya, tunatumai wafuasi wake
wachache waliobaki hapa na pale, wataona jinsi walivyotekwa kwa laghai.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape busara ya kupambanua ukweli na uongo kisha
awaongoze katika njia sahihi. Amiin.
Ndugu wasomaji,
Waislamu wote tunaamini pasi na shaka kwamba
wahyi(ufunuo) ulikomea kwa Mtume Muhammad(s.a.w). lakini hata tukijaalia ufunuo
bado ungaliunaendelea(kama wanavyodai akina Mirza) na usiku mmoja ikatokea
mmoja wetu kwa ghafla anazungumzishwa na Allah, hivi anaweza kujisikiaje kwamba
licha ya kupata fursa hiyo ataendelea kuona ni kitu kidogo tu kisicho na maana
sana kwake? Ni taathira gani atakayokuwa nayo mara baada ya tukio hilo?
Tukiangalia tukio kama hilo na fursa hiyo ilipomfikia Mtume Musa(a.s) haraka
sana aliomba amuone Allah. Kadhalika Mtume(s.a.w) alipopata fursa hiyo ya
kwenda Miiraj na kutakiwa aombe atakacho, akawaombea maghfira wafuasi wake.
Lakini tunamshuhudia mdanganyifu Mirza akidai
kusemeshwa na Allah, alichokiwaza akiwa katika “fursa” hiyo ni hofu yake ya
kufikwa na ufukara na tamaa ya kupata mali. Katika moja ya maandiko, Mirza
amenukuliwa akisema:
“Nilipopokea
Wahyi kuhusiana na kifo cha baba yangu, ubinaadamu ukanifanya nidhani kwamba
tungeishi maisha ya dhiki kwa kuwa aliyekuwa akituhudumia sasa hayupo”, (imenukuliwa
kutoka “The founder of the Ahmadiya Movement kilichondikwa na Muhammad Ali uk.
7; pia taz. Ruuhani Khazin juzuu ya 13 uk. 194).
Mirza alidai huu ndio “Wahyi” wa kwanza alioshushiwa na
Mwenyezi Mungu. Hata hivyo wakati anashushiwa wahyi huo kikubwa alichokiwaza ni
ile dhiki itakayowafika mara baada ya kufa baba yao. Anafikiria pesa. Wakati
Mwenyezi Mungu anamfahamisha juu ya kifo cha baba yake, haraka anachokichelea
“Mtume” Mirza ni upungufu wa mali!
Mtume asiyejua jukumu lake
Kwa mujibu wa Mirza wakati huo
kama mtume hakujua jukumu lake lingekuwa lipi katika ulimwengu huu, katika hali
hiyo anadai Mwenyezi Mungu(naudhubillahi) alimfanya kuwa ndiye Yesu aliyekuja
kwa mara ya pili. Uzoefu huu uliwezaje kuyageuza maisha ya Mirza Ghulam.
Kuhusiana na hili Mirza amenukuliwa akisema:
“Kwa
kuzingatia ahadi ya kwamba mtu anayeitwa Maryam ameahidiwa kwamba atainuliwa
daraja kwa Yesu kuzaliwa naye ambaye ataitwa mwana wa Maryamu; ambaye ni mimi.
Ufunuo utamjia Maryamu na mimi kadhalika lakini tofauti itakuwa kwamba Maryamu
atasumbuliwa na mateso ya kimwili mimi nitataabika kwa kukosa pesa”(Taz.
Nazool ul-Masih).
Kwa mara nyingine tena,
alichokificha nyuma ya madai yake kinadhihirika, kwamba anateuliwa na Mwenyezi
Mungu kuwa Masihi aliyeahidiwa lakini kikubwa anachowaza ni namna atakavyosumbuka
kipesa!
Ni vipi tutamtofautisha mtu
huyu anayedai utume na wale
walaghai watafuta pesa.
Sababu za kudai kwake utume
Akielezea sababu ya
kuteuliwa kwake kushika jukumu hilo, Mirza katika “ufunuo” wake anasema:
“Masihi
aliyeahidiwa amepokea ufunuo ili kuifanya biashara hii kuwa yenye faida kwangu”(Taz. Riwayat sahaba. Juzuu ya 11 uk. 106, na juzuu ya
14, uk.40).
“Masihi
aliyeahidiwa amepokea ufunuo: Nimewekeza mtaji wangu kwenu. Mnajua
faida na hasara yake”.(Taz. Mansab Khilafat uk. 40).
Kuporomoka kwa familia yake
Katika wasifu wake, Mirza
anaelezea kuporomoka kwa familia yake:
“Huko
nyuma, babu yangu, Mirza Gul Mohammed alikuwa Chifu na mtu maarufu kwetu,
baadaye karibu babu zangu wote waliteketezwa....baadaye katika utawala wa
Ranjit Singh, marehemu baba yangu, Mirza Ghulam Murtza, alirejea kijijini
Qadiani, na alivichukua vijiji 5 vilivyokuwa vikimilikiwa na baba yake...katika
hali hiyo ya uzee, baba yangu Ghulam Murtaza aliendelea kuwa chifu maarufu eneo
hili”. (Kitab ul Bariyah, Roohani Khazain juzuu ya 13 uk 175-176).
“Kwa
kifupi, hali ya nyumbani kwetu iliendelea kuporomoka siku hadi siku, mwishowe
tukafikia mahali ambapo familia yetu ikawa ya daraja la
chini”.(Tohfa-e-Qaiseriya, (Roohani Khazain juzuu ya 12 uk.
271).
Baada ya hapo wakati Waingereza
walipokuja, wakaitaifisha ardhi yetu, na wakawa wanatulipa kiinua mgongo cha
Rupiya 700 kwa mwaka ambacho kiliendelea kupunguzwa hadi kufikia Rupiya 180
wakati alipokufa babu, na baada ya kufa mjomba malipo hayo
yakasimamishwa”.(Taz. Seerat ul Mahdi sehemu ya kwanza riwaya na. 48,
kilichoandikwa na Mirza Basheer Ahmad(Mirza Ghulam Qadian).
Mirza Ghulam alichanganyikiwa
kutokana na kuporomoka kiuchumi kwa familia yake. Kuchanganyikiwa kwake
kulimfanya asiwaze kingine ila namna takavyoweza kuishi katika mazingira hayo
duni kiasi kwamba kama anavyodai mwenyewe Mungu alipomteua, muhimu alichoweza
kukikumbuka ni dhiki yake ya
kipesa.
Mirza - mwana mfujaji
“
Mama(mke wake Mirza) aliniambia(mtoto wake Mirza) kwamba katika ujana wake
Hazrat Masiih Mowood(Mirza Qadiani) alikwenda kuchukua kiinua mgongo cha babu
yako, kisha Mirza Imamudin alikwenda mbele yake. Alipopokea ushuru ule, Imamdin
akamshawishi(Mirza) badala ya kwenda Qadian wakenda sehemu ya mbali, na akawa
anahangaika naye huku na kule. Baadaye Mirza akazifuja pesa zote, Imamdin
akaachana naye na kumkimbia”, (Siiratul Mahdi sehemu ya kwanza
riwaya na. 49, kilichoandikwa na Mirza Bashiir Ahmad, mtoto wa Mirza Qadian).
Mirza Imamdin alikuwa mpwa wa
Mirza Qadiani wakati tukio hili linatokea yeye alikuwa na umri unaopata miaka
30 hivi. Kiinua mgongo hiki cha Rupiya 700 kwa kulinganisha na pesa ya hivi leo
inaweza kuwa sawa na laki kadhaa za Rupiya. Wapi Mirza na mpwawe walikwenda
kufuja pesa nyingi kiasi hiki kwa muda wa siku chache, kila mmoja anaweza
kuhisi vyake. Lakini kubwa ni vile mtu anavyoweza kupima akili ya mtu huyu
ambaye baadaye amekuja kudai
anapokea ufunuo kama mtu aliyekuja kuuhuisha upya Uislamu. Kwa hiyo
hakuja kuupigania Uislamu bali alichokuwa akikipigania ni mfuko na tumbo lake
akikusanya mapesa kutoka kwa
wajinga ndio waliwao.
Mirza ataraji kupata riziki
kimiujiza
“Awali,
Mirza Saheb alikwenda Amratsir, akakutana na mtakatifu Maulvi Abdullah
Ghaznawi. Mirza akamuomba: “Niliajiriwa(Mirza) kama karani wa mahakama ya
Sialkot kwa mshara mdogo sana. Kwa kuwa ilikuwa vigumu kuishi kwa kajimshahara
haka, nikajaribu kufanya mitihani ya kozi ya sheria, nikafeli. Moulvi Saheb alimuuliza,
sasa ndio unatakuniambia nini, unakusudia nini sasa? Mirza Saheb alisema: Sasa
sikusudii kufanya kazi, nataka kuishi kwa Tawakkul(kwa kumtegemea Mungu bila ya
kufanya kazi), kwa hiyo nakuomba uniombee dua ya Rajuu’at na Futuhaat( Rajuu’at
ni neno litumikalo kwa mtu mwenye kutaraji kuwa na mvuto kwa watu, na Futuhaat
ni neno lenye maana ya watu watakaovutiwa naye watampa vitu mbali pamoja na
pesa). Tafadhali niombee dua”,(Masih wa karne ya 14 uk. 48).
Mirza adai kapata ufunuo
afunge ndoa, lakini ahofia ulofa
"Alama
ya 27 ya utume, ni hii bishara kuhusu ndoa yangu ambayo ilifanyika mjini Delhi.
Mwenyezi Mungu aliniteremshia ufunuo usemao: “Ametukuka Mwenyezi Mungu aliyekuinua daraja kinasaba na
kindoa, huyo ni Mungu aliyeifanya nasaba yako kuwa tukufu na mke pia atatokana
na familia tukufu”. Ufunuo huu
ulikuwa bishara ya wazi, kwa sababu hiyo ule wasi wasi wangu uliongezeka
nilikuwa nikihofia ni namna gani nitakavyomudu gharama za ndoa hii”.(Roohani
Khazain juzuu ya 22 uk. 2470).
Mirza anadai kupewa bishara na Allah kuwa ataoa, anachohofia
atapata wapi pesa ya kufunga ndoa na atamlisha nini mke huyo!
Mirza aomba michango kuchapisha
Njia rahisi na ya
haraka ambayo Mirza alidhani ingemuwezesha kutatua dhiki yake ya pesa ni
kuwanyonya watu kwa kutumia ujinga wao kuvuna mapesa yao. Bara hindi kama
linavyofahamika limegubikwa na imani nyingi za kishirikina zinazonasibishwa na
dini, hivyo tangu awali Mirza aliona mwanya mzuri wa kueneza mawazo yake ya
kijinga ni kuchapisha vitabu atakavyovinasibisha na Uislamu.
Kitu cha awali
alichofanya ilikuwa kutangaza azma yake ya kuandika kitabu chenye juzuu 50
kuthibitisha ukweli wa Uislamu. Kwa ajili hiyo akawataka Waislamu wachangie
gharama za uchapishaji. Hiki kilikuwa kipindi ambacho Waislamu wa India
walikuwa katika hali ngumu sana. Waingereza waliua kabisa nguvu za Waislamu
ambao walitawala bara hilo kwa zaidi ya miaka 1000 badala yake walizipa nguvu
jumuiya za Wamishenari wa kikristo na Wahindu kueneza itikadi zao huku wakiukejeli
na kuupotosha Uislamu. Hivyo Mirza kwa tangazo lake ilionekana ni uamsho mkubwa
kwa Waumini wa dini ya kiislamu ambao hawakujua kuwa ilikuwa ni katika njama
zile zile za wakoloni wa kiingereza kuupiga vita Uislamu. Ilikuwa katika
mazingira haya Mirza akatangaza mradi wake wa kuchapisha juzuu 50. Kwa
kauli yake Mirza anasema:
“Ni
vigumu kuweza kuchapisha kitabu kikubwa kiasi hicho bila ya msaada wa
ndugu Waislamu. Na kila mtu anajua
thawabu atakazopata kwa kusaidia mradi huu muhimu. Kwa hiyo shime kila mwenye
imani yake, achangie kazi hii nzuri ili asaidie uchapishaji wa kitabu hiki.
Wale walio matajiri wakichangia gharama ya maakuli yao ya japo siku moja,
itarahisisha zaidi kuchapishwa kitabu
hiki , vinginevyo mwanga huu utabaki mafichoni. Au wale watakaoweza kutanguliza pesa zao kununua kitabu
hiki kabla ya kuchapishwa, wanitumie rupiya 5 wakimbatanisha na maombi yao,
pindi kitabu kitakapochapishwa watatumiwa” (Majmoo-Istihaarat, Collection of
Advertisement, juzuu ya 1 uk 11-12).
Waislamu walichangia kwa
ari kubwa mradi huo huku wengi wakitanguliza pesa kusubiri nakala za kitabu
hicho baada ya kuchapishwa. Mirza hakuweza kutimiza ahadi yake licha ya mapesa
mengi aliyopokea kutoka kwa Waislamu badala yake kwa muda wa miaka minne(1880-1884)
akaandika juzuu 4 tu akielezea Uislamu na kuwatumia watu, baada ya hapo
akadhamiria kwa kipindi cha miaka
50 baadaye awe anaandika juzuu baada ya juzuu alizoziita Braheen Ahmadiya
akielezea dini yake hiyo mpya na kuzigawa bure baada ya kutangulia kupokea
mapesa ya watu. Alisimama kuandika Braheen Ahmadiya baada ya kutoa juzuu
nne tu. Licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa wanunuzi, kwa kipindi cha
robo karne alichapisha na kuuza vitabu vingine vipatavyo 80. Miaka 25 baadaye
akachapisha juzuu ya tano ya Braheen Ahmadiya. Katika neno la awali la juzuu hiyo amendika:
“Awali
nilifikiria kuandika juzuu 50, lakini sasa nimeamua kuzinya juzuu 5 badala ya
50 na kwa vile tofauti ya tano na hamsini ni sifuri(dot)(sifuri inatamkwa kama
dot katika numerali za kiarabu /kiurdu) kwa hiyo kwa juzuu hizi 5 nimekamilisha
ule mradi wa juzuu 50”.(Preface to Braheem Ahmadiya, Roohani Khazain vol.21
uk.9)
Laghai huyu ndiye
anayedai utume.
Funuo
50,000 zinazungumzia masuala ya pesa
Ukisoma maisha ya Mirza Ghulam,
ukisoma vitabu vyake, na ukitazama harakati zake zote utagundua yote
yanahusisha masuala ya pesa:
“Kumbukeni
kwamba Mwenyezi Mungu amejenga desturi kwangu mara nyingi ninapoelekea kuata
pesa au vitu vingine kama zawadi, Hunifahamisha mapema ama kwa njia ya wahyi au
ndoto; na alama hizo zimenifunukia si chini ya mara 50,000”. (Haqeeqat
ul-Wahyi, Roohan Khazain Vol. 22 uk. 346).
Mifano mingine ya funuo
zinazoelekea kwenye pesa
“Ndoto
nilimsikia mtu mmoja akitaja: Noti, kisha nikapewa kitabu kana kwamba kina noti
ndani yake na wahyi ukaanza kutiririka kutoka katika ulimi wangu):Tazameni
rafiki zangu, habari mpya imechapishwa”.(Al-Hakam, Vol.X,
Na. 6, February 17, 1906, uk.1).
“Niliona
karatasi ndotoni, mistari michache iliandikwa kwa herufi za Kipeshia na
iliyosalia iliandikwa kwa kingereza. Niliielewa kana kwamba mtu aliniita jina
langu na kuniambia angenipa rupiya 25.(Review of
Raligions, Vol.IV, No.2 Februari 1905
“Ndotoni,
nilimuona mke wa Qudratullah akinipa rupiya”(Al-Hakam,
Vol.IX, Vol. IX, Na. 36, oct.17, 1905, uk. 10)
“Niliona
ndotoni alfajiri moja mtu mmoja akinipa kifurushi kilichojaa rupiya ambacho
nilizikipokea na kuzivingirisha kwaa kitambaa cheupe”(Diary
of the promised Mesiah, uk 23).
Mara
moja nilipokea Wahyi kwamba ningepata rupiya 21. Kwa hiyo Wahyi huu uliwataja
vile vile Aryas(Wahindu wanaoishi Qadiani)...ziada ilikuwa kuwafanya Waarya
washuhudie, utamu uanaogharimu rupiya 1 utakaogaiwa kwao...kama si hivyo,
huenda wakakumbuka alama hii baada ya kuonja tamu tamu hiyo.(Roohani
Khazain Vol. 22 uk. 318.
Mpaka hapo msomaji ameona
unaodaiwa kuwa ni wahyi aliopokea
Mirza ulivyojihusisha na mambo ya pesa. Zaidi ya hivyo inaonekana alikuwa
makini sana na ndoto au wahyi zake
zilizohusu pesa.
Mipango ya kuvuna mapesa
Ili kuijpatia mapesa kutoka kwa
watu, Mirza alibuni njia nyingi ikiwa ni pamoja na kuwaahidi watu kuwa
angechapisha kitabu muhimu hivyo walitakiwa kuachangia gharama kuwezesha kutoka
kitabu hicho. Aliweza kuchapisha Kitabu chake cha Braheen Ahmadiya kwa mbinu
hii kisha kujikusanyia mapesa za mauzo. Moja ya maandiko yamemkairiri Mirza
akidai:
“Taifa
lazima lisaidie Jamaat kwa kila namna iwezekanayo. Vile vile wasisite pia
kuisaidie kifedha. Tazameni, hakuna harakati zozote za duniani zilizoshamiri
pasi na watu kuchangia... hivyo
kwa wanajamaat vile vile hili ni muhimu kwao kulizingatia. Iwapo kila
mmoja atatoa pesa ndogo tu kila mwaka ni wazi mengi yatawezekana kufanywa. Na
iwapo mmoja wenu hayuko tayari kujitolea walau visenti vichache alivyo navyo,
ana haja gani ya kuwepo ndani ya Jamaat?”(Matamshi ya
Mirza yaliyochapishwa katika Al Ahbar ABadr Qadian ya tarehe 9 JUlai1903).
Kauli hiyo inathibitisha wazi
kwamba ili uwe mwanajamaat wa Ahmadiyyat hunabudi kuwa na tabia ya udanganyifu.
“Tangazo
hili si la kawaida, najaribu kutoa
wito wa mwisho kwa wale wanaojiita muridi wangu kwamba mapenzi yangu yako kwa
wale tu wanaoonekana kuwa ni watoa misaada, lakini wako wengi wanaotaka
kumdanganya Mwenyezi Mungu. Sasa kwa mujibu wa mfumo huu mpya, kila mmoja
arejee upya kiapo chake na atoe ahadi mpya ya maandishi kwamba ni sharti kwake
kila mwezi achangie kiasi gani....
mpaka miezi mitatu baada ya kuchapishwa tangazo hili, tumekuwa
tukisubiri majibu kutoka kwa kila mmoja wenu kulingana na alivyoahidi katika
mfumo huu kwa kila mwezi na iwapo hapatakuwa na majibu kwa muda wa miezi mitatu
jina la muhusika litaondolewa katika ahadi hiyo... na iwapo mtu baada ya
kukubali kuchangia, hatatuma mchango wake kwa miezi mitatu, jina lake pia
litafutiliwa mbali”.(Collection of Advertisement vol.3 uk
468-469).
Dua kwa malipo kwa malipo ya rupiya 500
“Nawab
Saheb, chifu wa Maleer Kotla alipatwa na maradhi, maradhi hayo yalidumu muda
mrefu. Mawakala wa Qadiani waliokuwa wakiishi eneo hilo wakamwambia mama yake
Nawab Saheb kwamba iwapo Mirza Saheb angeombewa dua angepona haraka. Baadaye
alipelekwa kwa Qadian Saheb ambaye aliahidi kumuombea dua na akawataka
wailipie kiasi cha Rupiya 500. Baada
ya kupokea pesa hiyo kutoka kwa mama yake Saheb, Qadian Saheb alimuombea dua,
hata hivyo Nawab hakuweza kupata nafuu yoyote na hatimaye akafariki dunia na
ile pesa haikurejeshwa”.(Isha’at us Sunnah
Vol. 18 uk. 146, iliyotajwa katika Raees-e-Qadian uk. 427 na Rafiq Dilawari).
Lengo la Zaka-
Kueneza jina la Mirza
Zaka, na sadaka kwa
kawaida hutolewa na waumini kwa lengo la kupata radhi za Allah, hayo ndiyo
mafundisho ya Uislamu. Lakini kwa mujibu wa itikadi ya Ahmadiayya inelezwa kama
ifutavyo:
“Wakati
wa Hazrat Maseeh Mowood mwarabu mmoja fukara alimjia. Mirza akampa kiasi
kikubwa cha pesa. Mtu mmoja alipoona hivyo akapinga, lakini Mirza akamwambia. (Nimempa
pesa hii) kwa kuwa kila atakakokwenda atakuwa akinijitaja mimi kwa msaada huu
niliyompa, atakuwa akinitaja kila atakapopokea chochote, kwa ajili hiyo atakuwa
ameeneza jina langu sehemu za mbali”.(Akhbar AlFazl, Qadian, vol.22. No.103, uk.9 ya
tarehe 26 februari 1935).
Techee Techee
Mirza anadai alipokea msaada
kutoka kwa malaika ulioitwa Techee Techee.
Mnamo
Machi 5 1905 niliota ndoto mtu mmoja ambaye alionekana kama Malaika, alikuwa
mbele yangu na akaweka mdomoni kwangu pesa; nikamuuliza jina lake, akasema hana
jina. Nikamuuliza tangu hapo unalo jina fulani; akasema jina langu Techee
Techee, Techee katika lugha ya kipanjapi ni jina la muda fulani ulioahidiwa,
nimekuja katika muda ule khasa ninaohitajika. Nikaamka. Kwa kweli sikuamini
macho yangu nikajikuta nikipokea maelfu ya Rupiya kutoka kwa watu baada ya
ndoto hiyo”.(Haqeeqatul Wahi, Roohani Khazain, juzuu ya
22,uk.345-346).
Pesa za misaada na matumizi
yake
Pesa zilizokusanywa kwa njia
mbali mbali zilitumikaje.
“Sasa
tutazame namna gani tunavyoweza kumpa pesa za matumizi Mahdi aliyeahidiwa
kutokana na ama hizi za msaada au vyanzo vingine kwa ajili ya familia, ndugu na
jamaa zake. Kila mtu anafahamu jambo hili kwamba Hazoora(Mirza) angepaswa
kupewa sehemu ya pesa kutoka katika makusanyo haya. Hivyo baada ya kifo chake
iwe wajibu kwa Anjuman(Ahmadiyya) kuipa familia hiyo kama alivyofanya Masih
Mowood mwenyewe, hiyo ni kwa sababu Anjuman hawezi kuwa muaminifu zaidi kuliko
Masihi Mowood”.(Izhaar-e- Haqeeqat uk. 13 tarehe 28
Novemba 1913, iliyochapishwa na Anjuman Ansarullah Qadian).
Mirza ashtakiwa kwa kuiba pesa a
ushuru na matumizi mabaya ya michango ya wafuasi wake.
“Mwaka
huu Mirza Ghulam Ahmad kipato chake cha mwaka kilikadiriwa kuwa Rupiya 7200 na
kodi itakayokatwa kutokana makadirio hayo ni Rupiya 187.50...Mirza Ghulam Ahmad
akaidai anapata kipato chake kutoka katika shamba lake, ardhi na bustni zake;
maingizo ya kutoka katika shamba lake ni kiasi cha Rupiya 82 annas 10, kutoka
kaika kipande chake cha ardhi anachomiliki ilikadiriwa ni Rupiya 300 na kutoka
katika Bustani yake ilikadiriwa kwa mwaka inaingiza Rupiya 200/300 au 400 au
kiwango cha kabisa Rupiya 500. Mirza alidai kuwa hakuwa na vyanzo vingine vya
pesa mbali ya maingizo hayo. Mirza Ghulam alidai vile vile kwamba alikuwa
akitegemea kupokea kiasi cha Rupiya 5200 mwaka huo kutoka kwa wanafunzi na
wafuasi wake. Hata hivyo hapakuwa na kumbukumbu zozote za namna alivyokuwa
akitumia pesa hizo, aliyatamka hayo kutoka kichwani mwake. Mirza vile vile alidai
kwamba kipato chake binafsi kutoka shambani kwake, ardhi aliyokuwa akimiliki na
bistani yake kiliosheleza mahitaji yake binafsi, hivyo hakuhitaji kupewa misaada na wafuasi
wake kujikimu.”(Matamshi ya Munshi Tajuddin Saheb,
Sub-divisional income tax collector, Batala, District Gurdaspur tarehe 31 Agost
1898, iliyorekodiwa katika Income Tax Case no. 46/55 ya 1898; haya yameelezwa
katika Roohani Khazain juazuu ya 13. uk.516).
Mirza aliapa mbele ya watoza kodi
kwamba hakuwa akitumia pesa iliyotokana na michango ya wafuasi wake kwa
mahitaji yake binafsi. Lakini awali tuliona:
“Sasa
tutazame namna gani tunavyoweza kumpa pesa za matumizi Mahdi aliyeahidiwa
kutokana na ama pesa hizi za msaada au vyanzo vingine kwa ajili ya familia,
ndugu na jamaa zake. Kila mtu anafahamu jambo hili kwamba Hazoora(Mirza)
angepaswa kupewa sehemu ya pesa kutoka katika makusanyo haya. Hivyo baada ya
kifo chake iwe wajibu kwa Anjuman(Ahmadiyya) kuipa familia hiyo kama
alivyofanya Masih Mowood mwenyewe, hiyo ni kwa sababu Anjuman hawezi kuwa
muaminifu zaidi kuliko Masihi Mowood”.(Izhaar-e- Haqeeqat uk. 13 tarehe 28 Novemba 1913, iliyochapishwa na Anjuman
Ansarullah Qadian).
Pesa za misaada
kutoka kwa wafuasi na maisha ya nyumbani kwa Mirza
“Awali
tulikuwa tukiwataka wanawake waishi kwa kuiga mwenendo wa Mtume; wale kiasi na
wapendelee vitu vikavu, na wavae nguo chakavu na vilivyoziada wavitoe kwa ajili
ya Allah.Kadhalika nasi tuwe na mwenendo huo. Kwa hotuba hii tuwe na kawaida ya
kuhifadhi pesa na kuzipeleka kwa Qadian. Wake zetu walipokwenda kwa Qadian na
kukaa huko, walifuatilia kila kitu kwa makini sana na waliporejea
walitushambulia kuwa tu waongo wakubwa kwa kuwa wameshuhudia wenyewe maisha ya
Mtume Mirza na wafuasi wake baada ya kutembelea Qadian. Maisha
ya raha wanayopata wanawake huko ni sawa na 0.1%. Mbali ya ukweli kwamba
tunaingiza mapesa mengi na vyovyote pesa itakavyotumika itakuwa imetumikia
Taifa letu. Kwa hiyo ninyi ni waongo mliotudanganya muda mrefu, sasa
hatutadanganywa nanyi tena. Hivi sasa hawatupi tena pesa tupeleke Qadian..”(Kashf
ul Ikhtilaf uk. 13 by Sarwar Shah Qadian).
“Siku
moja msikitini mbele ya Maulvi Mohammed Ali Khwaja Kamaludin, Sheikh Ramat Ali
mtu mmoja kutoka Ludhiana alieleza kwamba jumuiya imechukua mkopo kadhalika
watu hujitolea kutoka katika mishahara yao ya mwezi kuchangia jumuiya lakini
inavyoonekana hapa pesa zinatumika kununulia nguo na mapambo ya mke wa
Mirza(Biwi Saheb), nini hiki kinachofanyika?”(Sermon of Mira
Mahamud, Khalifa wa pili Alfazl Qadian tarehe 31August 1938).
“Kikwazo
kikubwa ni kwamba yeye(Dr. Abdul Hakeem) alitoa hoja kumpinga Masihi
aliyeahidiwa kuhusiana na masuala ya pesa, eti Mirza anachukua pesa kutoka kwa
watu na anazitumia atakavyo....yeye Mirza anakusanya pesa akidai kutaka
kuchapisha vitabu na anazikusanya kwa kudanganya watu, na anazitumia hivi na
vile atakavyo, haulizwi kwa matumizi hayo”.(AlFazl Qadian
ya tarehe 20januari 1921).
Shaghalabaghala za mahesabu ya
pesa za michango
Moulvi(Mohammed
Hussein Batalvi) Saheb alisema unakwenda Qadian, mpe ujumbe wangu Mirza Saheb
kwamba anipe hesabu za maingizo yake.. pesa za uma zinazotumika hovyo, pesa hii
inatumika wapi na vipi... nilifika Qadian na nikampa ujumbe ule Moulvi Saheb.
Hazrat Masih Mowood akaniambia kwamba nimjibu ya kwamba pesa iliyokuja ni kwa
ajili ya Allah na tutaitumia kwa ajili hiyo, hatuna rekodi yoyote ya matumizi
ya pesa hizo..”(Mapokezi ya Qadian yaliyotajwa katika AlFazl Qadian Na. 201 juzuu ya 123
ya terehe 28August 1946).
Maoni ya wafuasi kuhusiana na
Mirza
Iwapo itadhaniwa kuwa wafuasi wa
Mirza walifurahiwa na namna ya ufujaji wa pesa ulivyokuwa ukifanywa na Mirza
basi asome yafuatayo:
“Hazrat
Maseeh Mowood.... alionesha kuhuzunishwa sana pale alipotakiwa na Kamaluddin kukabidhi kazi ya uangalizi wa meko ya umma kwao, kwa
kuwa hawakumuamini. Na kwa hivyo aliona meko hiyo ifungwe badala ya kukabidhiwa
waangalizi wengine. “Hii kazi imekuwa chini yangu lakini yeye licha ya mimi kumwambia haya ni
majaaliwa ya Allah na katika maisha yangu kazi ya nimekuwa nikifanya kazi hii
alishikilia nikabidhi usimamizi huo .”(Kashf ul
Ikhtilaaf uk. 14 na Srwar Shah Qadian).
Kulingana na matumizi mabaya ya
pesa, utumiaji mbaya wa meko za umma, na ufujaji uliokuwa ukifanywa na Mirza,
Kamaluddin kwa hasira alimwambia Moulvi Mohammed Ali kwamba:
“Hii
ni haki kweli, kama unavyojua pesa za umma zinakusanywa kwa taabu sana na hoja
inayotolewa na Taifa limekuwa likiwataka watu wajinyime katika mahitaji yao,
sasa badala ya pesa hizo kutumika katika miradi iliyopangwa zinatumiwa na watu
binafsi kukidhi mahitaji yao(Mirza na familia yake) na kiasi hicho cha pesa
vile vile hakitoshelezi kuendesha miradi tuliyoinzisha. Tumelazimika kuiweka
kando miradi mingine kwa ukosefu wa pesa, iwapo kusingelikuwa na matumizi
binafsi haya ya pesa tungaliweza kutenga kiasi cha pesa kwa ajili ya
kukamilisha miradi hiyo iliyowekwa kando.”(Kashaf ul
Ikhtilaf uk. 15 na Sarwar Sha Qadiani).
“Katika
tukio moja wakati zilipokwenda kukusanywa pesa kwa ajili ya ujenzi wa shule,
Khawaja alimwambia Moulvi Mohammed Ali kwamba Hazrat Saheb(Mirza Qadian) peke
yake amekuwa akiishi maisha ya anasa huku akituhutubia sisi tujinyime na kwa
kupunguza matumizi yetu. Katika kujibu Moulvi Saheb alisema ndiyo hatuwezi
kulipinga hilo, huo ndiyo ubinaadamu.”(Barua ya Mian
Mahmud kwa Hakeem Nuruddin, Haqeeqat e Ikhtilaaf uk. 53 na Muolvi Mohammed
Ali).
Mirza akasirishwa na Muridi
wake
Mirza anatakiwa kutoa mahesabu ya
pesa za jumuiya badala ya kuto hesabu hizo anageuka kuwakaripia wanaomuhoji.:
“Yule
anayenipa, kisha akanikemea kwa namna ninavyotumia, amenishambulia, na
shambulio hilo haliwezi kuvumiliwa...sitowajali hata kidogo watu hao, nitawaona
sawa na vijidudu vifu ambavyo nyoyo zao zimejaa kutu na kukosa uaminifu... Mimi
si mfanyibiashara ninayeweka mizania ya mauzo, manunuzi na matumizi. Mimi vile
vile si muweka hazina ninayetakiwa kuhakikiwa na yeyote .”(Matamshi
ya Mirza Qadian yaliyochapishwa katika gazeti la Alhakm la tarehe 31 Machi
1905; Mafoozaet juzuu ya 7uk.325).
“Yeye(Mirza
Saheb) alisema kwamba leo Khawaja Saheb ameleta barua ya Moulvi Mohammed Ali na
akasema kwamba Saheb ameandika kwamba matumizi ya meko ya uma ni kiasi, maelfu
ya rupiya zinazokusanywa yanakwenda wapi? Na kisha yeye(Mirza)alikuja huku na
kutuambia kwa hasira kwamba hawa jamaa wanatuona sisi ni Haram
Khor(wabadhirifu)? Wana uhusiano gani na pesa hizi? Iwapo mimi nitajiondoa
kwenye jumuiya pesa hizi hazipatikana tena.”(Barua ya Man
Mahmud kwa Muolvi Nuruddin, Haqeeqat e Ikhtilaf uk. 52 na Moulvi Mohammed Ali).
Kustawi kwa ukadiani na
vishawishi kwa Muridi
Mirza alithubutu hata kuwahonga
watu ili kuwafanyawajiunge na uqadiani, kwa maneno mengi Mirza alitumia pesa:
“Tuliota
Ukadiani umekuwa kama Jiji kubwa na soko lake likiwa limetandwaa kwa mawanda ya
mbali. Majengo yenye roshani 2 na 4 yenye maduka yaliyo na dari na kuta
zinazovutia, na matajiri wanene
wakiwa mbele ya masoko yaliyofura bidhaa na mapambo ya almasi, lulu, fedha na
sarafu za dhahabu.(Matamshi ya Mirza yliyonukuliwa na
gazeti la AlHakam Qadian la tarehe 3 Aprili 1902).
Masharti ya kuzikwa katika
eneo la makaburi ya watu wa
'mbinguni '
Mnamo mwaka 1906, Mirza Ghulam
alitoa andiko lenye masharti kadhaa kwa wafuasi wake wanaotaka wazikwe kwenye
makaburi maalum ya watu mbinguni baada ya umauti kuwafika. Aliorodhesha
masharti kadhaa baadhi yake ni haya:
1. Sharti la kwanza
“...Kwa hiyo sharti la kwanza ni
kwamba, yeyote ambaye angetaraji kuzikwa katika makaburi haya, atapaswa
kuchangia pesa ili kufidia gharama za ujenzi.
2. Sharti la pili
“Sharti la pili ni kwamba
mwanajumuiya yeyote wa Ahmadiyya atapaswa kuzikwa hapa iwapo ataacha wasia
akiwa bado yu hai kwamba atakapokufa moja ya kumi ya mali yake yote itakwenda
kwenye mfuko wa mazishi ya eneo hili la makaburi haya”.
3. Sharti la tatu
“Sharti
la tatu ni kwamba yule anatarji kuzikwa katika eneo hili la makaburi atapaswa
kuwa muangalifu sana katika uhai wake, yule ambaye atajiepusha na makatazo yote
na ambayo hatafanya dhambi yoyote ya shirki”(Chanzo: The
Will. uk. 40-44. Roohan Khazain juzuu ya 20 uk.316-327).
Hapa msomaji atakuwa ameona
kwamba ukiacha sharti la tatu, masharti mawili ya mwanzo yote yamejiegemeza
kwenye pesa. Kwa mujibu wa masharti hayo, ni wale tu watakaoweza kulipia ndiyo
watakaopta fursa ya kuzikwa eneo maalum la watakatifu na hatimaye kuingia
peponi! Si hivyo tu, ili kupata nafasi katika makaburi hayo, mtu atapaswa
kuacha wasia kwamba atakapokufa sehemu ya mali yake iingie katika mfuko wa
Jamaat. Zaidi ya hivyo, Mirza alisisitiza kwamba:
“Hazrat
Masih Mowood anasema..yule ambaye hataacha wasia(utengao fungu la pesa kwa
jamaat), ni mnafiki”(Minhaj ut Talibeen, collection of
Speech na Mian Mahmaud, Khalifa wa pili
Nukuu zote hizi zinathibitisha
kuwa alichokithamini Mirza Ghulam Ahmad katika uhai wake ilikuwa ni pesa.
Ilikuwa ni pesa zilizomsukuma kuibua fikra potofu na kuanzisha miradi ya
kuwanyonya watu kwa jina la dini na ilikuwa ni kwa sababu ya kutafuta pesa na
maslahi ya kidunia yaliyompelekea Mirza kikaragosi wa Serikali ya Uingereza.
Kwa sababu hizo Mirza hakusita kuuza imani yake na wala hakuogopa kupoteza
imani ya maelfu ya watu waliomfuata.
1. Mirza alipandikiza fundisho
potofu la imani ya kurithisha katika mafundisho ya kiislamu ili kuhalalisha na
kudumisha madai yake ya kikafiri.
2. Aliugawa umma wa kiislamu
3. Alihubiri kuwatumikia makafiri
na akawafanya waliomfuata kuwa watumwa wanaowanyenyekea makafiri(hasa serikali
ya Uingereza).
Mirza Qadian na Serikali ya
Uingereza
Akitumia vipeperushi na makala,
Mirza Ghulam alijigamba kuwa angeweza kuifutilia mbali dhana ya Jihad miongoni
mwa waislamu. Alifanya kazi hiyo kwa kutumwa na serikali ya uingereza:
“Waheshimiwa
maafisa wa serikali mara kwa mara katika nyaraka zao wamekuwa wakieleza wakitoa
ushahidi juu ya msimamo huu wa maoni kwamba familia hii tangu huko imeendelea
kuwa imara yenye matarajio na yenye utii. Serikali iwe makini na mbegu hii
inayojiotosha yenyewe....inapaswa kuwaelekeza maafisa waoneshe ukarimu,
wanisaidie na kutoa kipaumbele kwangu na kwa Jamaat yangu. Sisi hatutasita
kumwaga damu zetu kwa ajili ya kuwalinda watawala wa kiingereza, hatukusita huko
nyuma wala hatutasita sasa kufanya hivyo”. (Roohan Khazain
juzuu ya 13 uk. 350).
“Mimi
binafsi nimeungana na serikali ya Uingereza kwa jili hiyo ambayo kwa hakika ni
ya kuonesha wema kwa serikali hii tukufu, hiyo ni kazi kubwa na muhimu kuliko
wahenga wangu(mababu zangu) na kwamba jukumu lenyewe ni hili, nimekusanya
vitabu vya kiarabu, kifursi na kiurdu kwa ajili hii kwamba...kuitii serikali
kwa dhati kabisa ni wajibu kwa kila Muislamu”.(Advertisement
of Mirza Qadian, collection of Advertisement vol. 2 uk.366).
“Hivyo
nimetumia kiasi kikubwa cha pesa kuchapisha vitabu hivi na kuvigawa katika nchi
za kiislamu. najua kwamba vitabu hivi vitakuwa na athari kubwa katika nchi hizo
pia. Na wale wote wenye usahiba nami wa kiitikadi unaotufanya tuwe jumuiya
ambao mioyo yao imeshibishwa imani ya kuitii serikali , msimamo wao thabiti na
nadhani kwamba watakuwa wazalendo kwa nchi na wenye dhati ya kuyatoa muhanga maisha yao kwa ajili ya
serikali.”(Advertisement of Mirza Qadian, Collection of
Advetisment vo.2uk.367).
“Katika
ukurasa wa 241 wa Braheen Ahmadiyya, kuna bishara juu ya serikali ya Uingereza.
Na bishara yenyewe ni hii: Mwenyezi Mungu si yule ambaye ataifanya serikali
ipate isumbufu na ninyi watu muishio ndai ya utawala huu. Kokote mtakakoelekea,
Mwenyezi Mungu yuko huko. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu anajua kwamba moyo wangu
unafuraha chini ya kivuli cha ulezi wake na serikali ya amani, nabaki kuwa
mwenye hamasa ya kuiombea dua kwa sababu siwezi kufanya kazi zangu kikamilifu
katika miji ya ya Makkah na Madina wala Istanbul(Rome), Syria, Iran, wala
Kabul”.(Collection of Advertisement vol.2 uk. 370).
“Hazrat
Masih Mowood anasema, Serikali ya Uingereza ni upanga wangu. Kwa nini sisi
Ahmadiyya tusifurahie ushindi huu dhidi ya Baghdadi(Iraq), iwe ni Arabuni au
Syria, tunataka kuona mnga’aro wa upanga wetu kila mahali”.(Matamshi
ya Mirza Mhamud katika AlFazl Qadian ya tarehe 7 septemba 1918).
“Huu
ni kama ushahidi wa kuchomoza mwanga katika siku mpya kwamba kiuhalisia
Serikali ya Uingereza ni ngao inayokinga uahmadiyya uweze kusonga mbele. Jaribu
kuondoa ngao hii walau kwa muda mdogo tu utaona ni namna gani utakavyoandamwa
na kuchomwa na mvua ya mikuki yenye sumu kichwani mwako. Hivyo kwa nini tusiwe
wenye shukrani kwa serikali hii? Maslahi yetu yanasimamiwa na serikali hii na
kuvurugwa kwa serikali hi itakuwa ni kuvurugwa kwetu na kustawi kwake itakuwa
ni kustawi kwetuPopote utakapoenezwa utawala wa serikali hii, itakuwa umefungua
eneo jipya kwa mahubiri yetu. Kwa hiyo hapatakuwa na upinzani wowote dhidi ya
serikali utakaogeuza utiifu wetu kwayo, na kamwe hapatakuwa na mpumbavu
aliyetayari kuhatarisha maisha yake mwenyewe”.(Alfazl Qadian,
vol.3 Na.51 ya tarehe 19Oktoba 1915).
“Namshukuru
Mwenyezi Mungu ambaye amenipa nafasi chini ya kivuli cha serikali hiyo, ambayo
kwa ulinzi wake naweza kuwa huru kuendelea na kazi ya kuhubiri na kushauri.
Ingawa ni wajibu kwa kila mmoja kuonesha shukrani kwa ufadhili wa serikali hii
lakini nadhani imekuwa wajibu zaidi kwangu kwa sababu malengo yangu haya makuu
yamefikiwa kutokana hifadhi na ulinzi wa serikali hii ya Malikia Victoria,
nisingaliweza kukamilisha malengo hayo chini ya serikali nyengine yoyote ile
hata kama ingalikuwa ni serikali ya kiislamu.(Roohani Khazain vol. 12uk. 283).
SubhanAllah!! hapa ndipo mahali
pa kupazingatia. Ni malengo yepi hayo aliyokusudia Mirza kuyakamilisha ambayo
yasingaliwezekana bila ya ulinzi wa Serikali ya Uingereza ambayo
yasingaliwezekana kufikiwa chini ya hata serikali ya kiislamu.
“Awali
ya yote namshukuru Allah kwa kwa fadhili zake kwangu wakati wa utawala wa
Malkia wa India(Malkia Victoria) na amuongezee hadhi na heshima abaki kuwa
mwenye furaha yeye, jamaa na watoto wake”... uaminifu huu una kiwango cha juu
cha utiifu, mapenzi na unyenyekevu ambao sina maneno ya kuuelezea kwa Hazoora Malika-Aalia(Mtukufu
Malkia) na waheshimiwa Maafisa wake . Kwa sababu ya imani na mapenzi ya kweli,
naandika juzuu kwa mnasaba wa sherehe za jubelee na kuiita “Tohfa
e- Qaiseriyah” ambayo nitaituma kwa Janab Mamdooha(mtukufu) kama
Darwesh wa sasa...nanyanyua mikono yangu kuomba; Ee Mwenyei Mungu uweke
utawala huu wa mpendwa Malkia wa
Uhindi juu ya vichwa vyetu, himaya yake idumu. O Qaisariyya e
Mubaraka Malkia! Mwenyezi Mungu
akulinde, akupe uhai mrefu, heshima na mafanikio, nyoyo zetu zielekee kwako...
ni ukweli kwamba nyoyo zinazopendana hukumbukana), Sihitaji kutumia lugha ngumu
kuelezea ninavyokupenda katika moyo wangu, moyo umekita mapenzi na heshima kwako. Dua zetu za usiku na
mchana zimeendelea kukutiririkia kama mkondo... ingawa najua kwamba nimetekwa
na hisia kali katika moyo wangu, ningepaswa kelezea heshima, utii na shukrani
zangu mbele ya Hazoora e Hind, utawala wake uwe daima dumu, lakini siwezi
kuelezea shauku ya dhati niliyo nayo”.(Sitara
-e-Qaisariyah, Roohan Khazain juzuu ya 15 uk. 111).
“Vitabu
nilivyoandika katika kuutukuza utawala wa kiingereza vimesheheni makabati, hasa
vile vilivyojaribu kufutilia mbali dhana ya Jihad ambayo waislamu wengi
wameishikilia na kuiamini sana. Hili ni jukumu kubwa kwa serikali. Kwa hiyo
natumai zawadi nono inayolingana na kazi hiyo”.(Tabligh e
Risalat, Vol.7, uk. 19).
Picha halisi ndiyo hii. Jukumu la
Mirza lilikuwa kujiingia katika kupiga vita moyo wa Jihad miongoni mwa Waislamu
ili wawe watiifu kwa makufari. Alikuwa akimuomba Mwenyezi Mungu adumishe
utawala wa serikali ya kikafiri kwa sababu ilikuwa ndio ngao yake. Mirza Ghulam
Ahmad alikuwa ndiye wa kwanza kujiita Mtume katika historia ya Uislamu
aliyehubiri utwana kwa wafuasi wake. Tukiwaweka kando Mitume wa Allah,
hajatokea kiongozi wa nchi yoyote ile iliyependelea utumwa badala ya uhuru kwa
nchi yake. Lakini Lahaula! Mirza kwa tamaa ya maslahi ya kidunia, aliuza imani
yake na imani ya maelfu ya waliomfuata. Hii ndio maana alipokula kiapo cha
utii, moja ya masharti ilikuwa utii kwa serikali ya Uingereza:
“Masharti
ya uzinduzi: Nimewasilisha vielezo vya hotuba zangu za muda wa miaka
17...ambazo zinazothibitisha wazi kwamba nimekuwa nikiitakia mema serikali ya
uingereza kwa dhati ya roho na moyo wangu..kama nilivyoelekeza mwanzo katika
sharti la 4 la uzindui kwamba kwa ukweli kabisa nimekuwa mtiifu kwa serikali ya
kiingereza na ni mwenye roho yenye kujali
ubinaadamu”...”(Kitab ul-Bariyyah, Roohan Khazain
vol.13 uk.10).
Ukweli huu waweza kuwashangaza
wafuasi wengi wa Ahamadiyya wa hivi sasa kwa kuwa wengi wao hawajawahi kusoma
vitabu vya Mirza Ghulam Ahmad na elimu yao juu ya mafundisho yake kwa kiasi
kikubwa imeegemezwa katika maandiko ya propaganda yanayosambazwa ndani ya
jumuiya hiyo. Uthibitisho mkubwa ni mfumo wa kuapa. Kiapo cha asili hivi sasa hakipo. Kiapo cha hivi sasa hakina sharti Na. 4
lililotajwa hapo juu. Limekwenda wapi sharti hilo? Nani
aliyeliondoa sharti hilo? Nani anayejaribu
kumdanganya nani? Makadiani
waulize maswali haya kwa masheikh(murrabbi) wao.
Dondoo
kutoka maisha ya Mirza
Mnamo mwaka 1907 kuelekea mwisho
wa uhai wake, Mirza alifanya tathmini ya kazi ya aliyoifa kwa miaka yote na
mafanikio aliyoyapata:
“Hakuna
anayenijua. Wala hakuna ajuaye kuwa ningaliweza kuja kuishi maisha ya wasaa.
Nilivyokuwa navyo ni ilikuwa sehemu ndogo tu ya urithi katika vijimali alivyoacha baba yangu.
Baadaye Mwenyezi Mungu akaniwepesishia kidogo wakati ambapo sikuweza kutegemea
kupata walau rupiya 10 kwa mwezi. Hata hivyo Mwenyezi Mungu akaigeuza hali
yangu ya maisha na akaniunga. Sasa
nina zaidi ya rupiya laki tatu”(kwa kulinganisha na pesa za sasa hivi
rupiya laki tatu ni mamilioni ya dola).(Roohan Khazain,
Vo. 22,uk.220-221, Haqeeqat ul-Wahi, uk.211-212, 1907).
“Imekuwa
ni wajibu kwetu kubaki tukiishukuru serikali hii tukufu ya Uingereza”.(Iza
e Auham, footnote).
“Ushauri
wangu kwa Jamaat ni huu, wanapaswa kuufanya himaya ya Kiingereza kama yenye
mamlaka juu yao(Uulil Amr) na wabaki kuitii kwa moyo mkunjufu kabisa”.(Zuroorat
ul Imam uk.23).
Taratibu za kipesa katika
Ahmadiyya ya leo
Waliomfuatia Mirza katika uongozi
wa Maqadian walikuwa na utamaduni wa kujali pesa zaidi:
“Ndoa
ya Binti wa Amiiril Muuminina, Khalifa wa Masihi al Rabbi(Mirza Tahir), Atiya
tul Mujiib(Tooba), Mwenyezi Mungu amlinde, ilifanyika mnamo saa 1.00 usiku
uliokuwa wa furaha sana na baraka ndani ya eneo la Msikiti wa AlFazl...si chini
ya wageni 600 walihudhuria... kabla ya hapo wakati wa swala za Ijumaa na
Alasiri siku hiyo, Huzoora
aliitangaza ndoa hiyo ambayo ilifanyika kwa Muoaji Mukarram Malik Sultan
Mohammed Khan Saheb mtoto wa Mukarram Malik Sultan Haroon Khan Saheb kulipa
Mahari ya Rupiya Milioni 1”.(AlFazl
International 119 Novemba 1999 mapka 25 Novemba 1999).
Leo hii, kuna kiwango cha moja ya
kumi au theluthi moja ya kipato
cha mwezi kinachotakiwa kilipwe na kila mwanachama wa Ahmadiyya kusaidia
harakati za kueneza itikadi hiyo. Zaidi ya hivyo, kuna taratibu za aina nyingi
za ukusanyaji pesa kwa madhumuni maalum. Profesa Munawaar amendika katika
makala yake:
Kuna utoaji na utozaji mkubwa wa
pesa katika jumuiya ya Ahmadiyya. Kila Ahmadiyya anapaswa kulipa asilimia 6 ya
kipato chake kama CHANDA AAM. Ni malipo ya wajibu, kiasi ambacho hakitalipwa
huoneshwa kama deni linalotakiwa kulipwa baadaye kupitia katika akiba yake ya
benki. Iwapo Ahmadiyya atakataa kulipa CHANDA, anakoma kuwa mwanachama. Ingawa
hiyo CHANDA ni kitu cha hiyari kisicho na kiwango maalum, mwanachama huweza
kulipa zaidi kwa kadri ya uwezo wake wakati ambapo ushuru una kiwango maalum na
ulipaji wake huwa wajibu, na kiasi kisicholipwa huoneshwa kama salio la deni
lisilokwisha abadan.
Mbali ya malipo ya CHANDA AAM,
pia kuna malipo mengine ya:
·
CHANDA JALSA SALANA
·
CHANDA TEHREEK JADEED
·
CHANDA WAQF JADEED
·
CHANDA SAD SALA JUBILEE(hii hivi sasaimefutwa)
·
CHANDA KHUDDAMUL AHMADIYYA(CHANDA MAJLIS) ambayo
inatakiwaitekelezwe na vijana
·
CHANDA TAMEER HALL(ukumbi huu ulijengwa mwaka 1973
na kumalizika lakini ukusanyaji wa CHANDA hii unaendelea.
·
CHANDA AFRICA
·
CHANDA DISH ANTENA (Ahmadiyya TV Network).
·
CHANDA LAJNA AMA’ALLAH(hii inatozwa wanawake)
·
CHANDA ATFAAL(hii wanatozwa watoto).
·
CHANDA ANSAAR(hii wantozwa watu wazima waliovuka
umri wa mika 40).
Kwa ufupi, Ahmadiyya anatakiwa
kulipa walau asilimia 10 ya kipato chake cha mwezi. Kuna mfumo wa hiyari wa
ukusanyaji wa pesa za CHANDA ambazo mkusanyaji hapati sehemu. Ni mfumo ambao
haupatikani mahali popote nje ya Ahmadiyya. Mara mbili tatu kwa mwaka
wasimamizi tofauti wa CHANDA tofauti huja kutoka vituoni kuhakiki Akaunti ili
kuhahakikisha kama kiasi kilichopokelewa kimetumwa(Chanbnagar-Rabwah).
Kwa sababu ya mfumo huu, Jamaat inaonekana kama mtandao uliopangwa vizuri kumbe
ni shaghalabaghala tupu usiofuata sheria wala kanuni. Jamaat ni kundi
lililojiweka vyema katika ukusanyaji wa pesa. Kama kusingalikuwa na mfumo huu
mzuri wa CHANDA, leo hii familia za watoto(warithi) wa Mirza Saheb
wasingalimiliki maeneo makubwa ya Ardhi(murrabba)(inakadiriwa Murrabba 1 ni
sawa eka 25) wala wasingeishi maisha ya anasa na ubadhirifu kama walivyo. Hii
ndiyo “Baraka” ya mfumo huu wa pesa za Ahmadiyya). Waahmadiyya wengi huchanga
pasi na kujua undani wa michango hiyo.
Rejea
Growing Number of Member in
Jamaat Ahmadiyya by Prof. Munnawwar
Email: rsyed@emirates.net.