Bismillah Al-Rehman Al-Raheem
Anti Ahmadiyya Movement in Islam
December 2004
Kwanza kabisa ningependa kujielezea kwa kifupi. Mimi ni msichana niliyezaliwa katika jamii ya Ahmadiyya, asili yangu ni Mpakistan, nimekulia Mashariki ya kati. Nilirejea katika Uislamu takriban miaka mitatu iliyopita. Ni hivi karibuni tu nimefunga ndowa.
Namna mimi mwenyewe ninavyoutazama Uhmadiyya, nasema kamwe sikuwa Ahmaddiyya. Hebu sasa nielezee zaidi. Mara yangu ya kwanza kabisa kuujuwa Uhmadiyya ilikuwa pale nilipokuwa na umri wa miaka kumi. Wakati huo nilikuwa na kawaida ya kupitisha mapumziko ya kiangazi nyumbani kwa nyanya yangu.
Huko nikawa nasoma vitabu fulani vya utenzi ambapo naukumbuka utenzi mmoja usemao, “Mariam Meray Zanoon Main, papo hapo mimi nikaona kuwa huu ni uongo. Heshima na hadhi ya Bi Mariam iko juu na haiwezi kutumika katika ubeti kama huo.
Aidha nakumbuka, baada ya kuhudhuriya Muhadhara wa Ahmadiyya, binamu yangu mmoja aliwahi kusema kuwa Majini maana yake ni watu ”watokeao mlimani.” Naye Baba yangu akazungumza na binamu huyo juu ya jambo hilo, mimi hilo halikuniingia kabisa.
Vile vile nakumbuka Baba alikuwa akisema kuwa Vitabu vya Mirza Ghulam Ahmadi vinatumia lugha ya matusi.
Basi masiku yakaenda nami nikahitimu masomo. Kwa vile sisi hatukuwa ndani ya wigo wa jamii ya Ahmaddiyya, hatukuwa na uhusiano nao mkubwa. Hii ndiyo maana ya mii kusema kuwa kamwe sikuwa Ahmadiyya na wala sikuwa hata na ile itikadi ya kupandikizwa.
Kuna vipindi vitatu ambao uhitaji dini, pale mtu anapozaliwa, anapoolewa na anapokufa. Wakati wa kutafuta mchumba wa kufaa ndio wakati ambapo familia nyingi za Ahmadiyya uhudhuria sala za Ijumaa au mikutano mingine katika vituo vilivyo karibu nao.
Ni sababu hiyo hiyo iliyoifanya familiya yetu ijinasibishe na jamii ya Ahmadiyya. Kilichoitanza akili yangu ni kile kiapo wanachokula ambacho kinasema kuwa “Ukimshuhudia Allah kuwa shahidi, basi hapo kuna tamka kutumia uhai na mali zao kwaajili ya kuitumikia Jumuiya ya Ahmmadiyya.
Kamwe mimi nisengeliweza kula kiapo hicho kwani naamini kuwa katika kiapo chochote cha kumshuhudisha Allah kama shahidi, ni heri wewe mwenyewe ukinuwiye.
Mimi nikawa nasimama tu na kuinamisha uso chini bila kuapa. Likatokea jambo jingine lililotanza fikra zangu. Ahmadiyya kwa ujumla wao hawajitangazi kuwa wao ni Ahmadiyya na hata katika Pasipoti hawaandikishwi kwa jina hilo.
Pale Baba yangu alipofanya mazungumzo na mwenzangu mmoja juu ya vitabu vya Ahmadiyya, alikitaja kitabu kimoja kiitwacho, Truth, Revelation $ Reality kilichoandikwa na Tahir Ahmadi.
Kesho yake mwenzangu huyo akawaambia Wapakstan wenzetu kuwa mimi ni Ahmadiyya, na nilipokabiliwa, nikakataa. Hiyo ilkuwa ni mara ya kwanza katika maisha yangu ambapo nilijihisi niko hatiani na dhambini, unaingia hatiani kwa kosa lisilokuwa lako.
Baadaye nilipoanza kutafakari mambo hayo, nikatanabahi kuwa kumbe hatupaswi kurithi dhambi za wazee wetu waliotangulia na kukirithisha kizazi kijacho. Iwapo Uhamadiyya ni ukweli basi mimi napaswa kusimama kidete kuuteteya na napaswa niuonee fahari, lakini kama si ukweli basi niachane nao kabisa, nisijibebeshe tena dhambi hiyo katika maisha yangu yaliyosalia.
Ndipo nikakutana na Mirza Tahiri Ahamadi mjini London. Kwa vile wazazi wangu walimueleza kuwa mimi nilikuwa bado sijaolewa yeye alipendekeza wachumba kadhaa. Alinisifu kwa kuniambia kuwa mimi ni mrembo. Sina budi kukiri kuwa kweli nilivimba kichwa.
Baadaye nilipotafakari na kukutana na viongozi wengine wa Dini, niliona kuwa wao hushusha macho ya chini wanapozungumza na wanawake na hawaghafiliki kuthubutu kutamka maneno kama hayo. Basi ukafika wakati wa kufanya uchaguzi wa wachumba. Kulikuwa na mchumba mmoja kutoka Suni. Kwa dhati mimi nikamwambia Mama, kwanini mtu huyo asifikiriwe, yeye akaniambia kuwa sisi haturuhusiwi kuoana na mtu yeyote asiyekuwa Ahmadiyya. Na Yule anayefanya hivyo basi familiya yake yote hutengwa na jamii ya Ahmadiyya. Familiya hiyo huenguliwa Hazoor (Neno lenye maana ya viongozi.
Mimi jambo hilo likanishangaza kwani Allah hamtowi yeyote yule katika jamii yake. Hapo ndipo mimi nilipochanganyikiwa. Nilipoanza kuyatafakari mambo yaliyonitatiza kichwani na kuanza kutafuta majibu: Nilijadiliana na mwenzangu mmoja juu ya mambo haya naye akanishauri kwamba niamuwe niwe nani kisha ndiyo nifikiriye kuolewa, kwani vinginevyo kutakuwa na tathira mbaya.
Kwa kweli ushauri huu ulinigusa sana na kwa mara ya kwanza sasa katika maisha yangu yote, nikaanza kuusoma Uahmadiyya. Nilisoma tovuti zilizopinga uahmadiyya, nikasoma tovuti zilizounga mkono uhamdiyya. Nikajadiliana na wenzangu ambao niliona wanajuwa mengi kuhusu Uislamu.
Jambo la mwisho kabisa ambalo lilinileta katika Imani ya kweli, ilikuwa pale nilipopata vitabu halisi vilivyoandikwa na Mirza Ghulam Ahmadi katika lugha ya kihudu.
Mimi naamini kabisa kuwa Ahmadiyya yeyote yule anayesoma vitabu hivyo sambamba na kusoma Qur’an, huku akiwa ameiweka huru akili yake ataachana kabisa na Ahmadiyya.
Kuna mambo machache ambayo ni muhimu kuyataja, kama vile Mirza anavyojielezea kuwa yeye aligeuka kuwa Nabii Issa (Yesu)! Anaeleza katika kitabu chake kuwa, kwanza yeye alikuwa Bi Maryam, kisha akawa mjamzito kwa kipindi cha chini ya mwaka mmoja, kisha ndipo Yesu akazaliwa. Huu ni mzaha mtupu wa kuchezea aya ya Allah!
Hitimisho langu juu ya kwanini Mirza Ghulam Ahmadi aliamuwa kupinga muujiza wowote uliotajwa katika Qur’an ni kwasababu yeye hakuweza kufanya muujiza wowote. Kwavile yeye hakuweza kufanya muujiza wowote ndio maana akakanusha miujiza yote ile iliyotokeya kwa uweza wa Allah (s.w).
Hivyo pale mtu anapo thibitikiwa na ukweli, kuna njia mbili za kufuata, ama abakiye kuwa Ahmadiyya kwaajili ya kuwafurahisha watu au aachane kabisa na Ahmadiyya. Mtandao wa kijamii wa Ahamdiyya una nguvu sana na humfanya mtu aone vigumu kujitowa.
Mimi niliamini watu wanaweza kuwa na mitandao katika maisha yao, yawezekana ni kutokana na taaluma yako, yawezekana ni kutokana na tabiya zako au kwaajili ya maslahi. Msimamo wowote wa maisha ya mtu huwezekana iwapo tu utamuamini Mwenyezi Mungu.
Nilisoma aya moja katika Qur’an ambayo inasema kuwa kama ukiona dhihaki inafanywa juu ya aya ya Mwenyezi Mungu basi usikae pamoja nao vinginevyo nawe utakuwa kama wao. Mimi naamini kuwa Ahmadiyya wanatumia hoja ya ujanja ujanja kuthibitisha Imani yao na ili kufanya hivyo, wachezee aya za Mwenyezi Mungu. Kwahiyo mimi nikaamuwa kutohudhuria Jalsa Salana ya Ahmadiyya. Hapo nikaelewa kwanini Ahmadiyya wanahesabiwa kuwa wako nje ya wigo wa Uislamu.
Nikazungumza na maalim mmoja iwapo baada ya kuwa nimeachana na Ahmadiyya, je ningeweza kuolewa na Ahmadiyya, naye akanieleza kuwa hilo haliruhusiwi. Basi hatimaye ulipofika wakati, nikaamuwa kuolewa na Muislamu wa Sunni, nikakabiliwa na hatuwa ya kususwa kabisa na Ahmadiyya.
Wazazi wangu walihudhuriya Arusi yangu lakini ndugu zangu hawakuhudhuriya. Yafaa hapa niitaje hatuwa ya mchumba wa dada yangu ambaye alitishiya kuvunja uchumba naye iwapo angehudhuriya harusi yangu kwani hilo lingemaanisha kuwa Dada yangu naye piya si Ahmadiyya na kwasababu hiyo yeye asingeweza kumuowa.
Kwa kuwakosa ndugu zangu katika harusi yangu iliniuma kweli kweli. Upuuzi mwingine wa kutajwa hapa ni kuwa Baba yangu alimuuliza kaka yangu kuwa sheria inasemaje, Kaka yangu akajibu, “Iwapo Ahmadiyya anaolewa na mtu asiyekuwa Ahmdaiyya basi nyiye hamtakiwi kuhudhuriya harusi ya wa tu hao.” Baba yangu akajibu kuwa sheria hiyo haifanyi kazi hapa kwani yeye (Dada yako) amekwishatangaza kuwa yeye si Ahmadiyya, kwahiyo hii ni harusi ya watu wawili wasiokuwa Ahmadiyya ambayo wewe unaweza kuhudhuriya.
Kwa kauli hiyo kaka yangu akasema iwapo mtoto wa kiume ndiye anayeoa basi kuna fursa ya kuongeza idadi ya Ahamdiyya hivyo unaweza kuhudhuriya harusi yake, lakini kwa msichana ndiye anayeolewa haiwi hivyo. Basi ndugu zangu, na hao wanaoitwa wanajamii wenzangu wa Ahmadiyya na wengineo wote wakanisusa.
Kwakweli mimi nawasikitikia wao kwa dhambi yao, kwani wanaamini kama wangehudhuriya harusi hiyo kiongozi wao angewatenga. Jamaa zangu wa Sunni walinisaidiya kikamilifu na wote walikuwepo kwaajili yangu.
Mwisho namuomba Allah. Authubutishe msimamo wangu juu ya Uislamu na awaoneshe ukweli kuhusu Mirza Gulam wale Ahmadiyya waliopotea waukane Uahmadiya ili na wao waukatae uongo huu wa Mirza Ghulam Qadiyyan. Amiin
Mwanamke aliyerejea katika Uislam
Nitaandika makala yenye maelezo ya kina hivi karibuni.
http://alhafeez.org/rashid/swahili.html