muislamu.
&n bsp;
Kitu ambacho mimi sikukielewa ni kwanini mayahudi wawe wateule wakati ndio
hao waliojaribu kumuua nabii Issa [as]/ zaidi ya hivyo wanaweza kuwa
wateule ikiwa wao hao ndio waliompigia vita mtume wetu Muhammad [saw] na
mpka sasa wanafanya mbinu kubwa kupiga vita uislamu na juu ya hivyo qur-
ani tukufu inaeleza waziwazi kuwa mayahudi ni maadui wa uislamu.
Kutokana na maandiko [fasihi andishi] yao nikagundua kumbe makadiani walikuwa
na mahusiano mazuri sana na waingereza katika kitabu chake kiitwacho.
Invitation ton Ahmadiyyat; mtoto wa Mirza Ghulam anaelezea ukweli
kuwa yeye alikuwa akiiombea dua dola ya uingereza ishinde vita vya
kwanza vya dunia. Je India haikufanywa koloni la waingereza/ Nadhani lingekuwa
jambo la maana kama angeomba uingereza ishindwe vita
Kwa hiyo hii ikanibainishia kuwa lazima tu kuwe na mahusiano ya aina fulani
kati ya makadiani na wakoloni wa kiingereza. Baadae tena nikaona kitabu
kiitwachoAhmadiyya Movement: British Jewish Connections <http:/alhafeez.org/rashid/british
Jewish /> kitabu hicho kimeandikwa na Bashir Ahmad ambae ni muislamu kitabu
hicho kilinisaidia sana kuelewa kuwa ukadiyyani ni upotovu mkubwa kabisa
kitabu hicho kilinisaidia kutoka katika maisha ya udanganyifu[ukadiyyani]
khaswa khaswa nilifurahi kupata ushahidi kuwa makadiyyani wana mahusiano
madhubuti na mayahudi ni pia ni vibaraka halisi wa waingereza ndani ya
uislamu Allah anasema katika Qura an
Enyi mlioamini! msiwafanye wayahudi na wakristo kuwa marafiki
zenu[wa kuwapa siri zenu]wao kwa wao ni marafiki na miongoni mwenu atakayefanya
urafiki huo nao basi huyo atakuwa pamoja nao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi
watu madhalimu[5:51]
Ndoto
Miezi 6 kabla sijawa kadiani niliota ndoto ambayo ilikuwa ya kueleweka
kabisa katika ndoto hii nilimuona Mtume Mtukufu Muhammad SAWS] amesimama
mbele yangu ijapokuwa hakusema yeye ni nani mimi nikajua kabisa alikuwa
yeye.
Nilifurahi sana kuota ndoto hiyo njema hapo kabla sikupata kuota ndoto ya aina hiyo katika ndoto hiyo niliona wingu la buluu kama lile la hasubuhi na mwangaza wa jua Mtume wetu Muhammad alivaa mavazi meupe yenye mistari stari michache ya kijivu alikuwa na nywele nyeusi na sura yenye mvuto Muhammad [SAW] akazungumza kwa lugha yangu ya asili [kialbania]akinambia ‘wewe utapata ‘garth[sijapata kulisikia neno hilo] hapo hapo nikaamka nikamuona mjomba akienda zake kazini mapema mno hasubuhi nikamuuliza mjomba hivi neno hili lina maana gani akaniambia ni uzio unaozunguuka nyumba [fensi] mara nyingi kwa ajili ya kondoo au wanyama wengine naye kaka yangu mkubwa nilipomuuliza alinijibu hivyo hivyo ila yeye akaongeza tu anaweza kuwa ni uzio unaotumika kwa ajili ya usalama
Nilipokuwa kadiani ndoto hii haikunijia kichwani nikamsimulia ndoto hii kiongozi wa kadiyyani mhadhiri huyo akaniambia eti niliyemuona ndotoni ni Mirza Ghulam au mmoja wa viongozi [makhalifa]wanne wa dini ya kadiyyani mimi nikawajibu kwa kuwaambia kinagaubaga kuwa yule si mwingihne bali alikuwa mmbora wa viumbe Mtume Muhammad[SAW] ndiye niliyemuona ndotoni.
Nilipoota ndoto hii tayari nilikwishayajua mambo fulani kuhusiana na harakati za ukadiyyani kupitia kwa mwanafunzi mwenzangu huyu mwanafunzi alinitia mashaka juu ya ujaji wa ya ujio wa Imam Mahd mimi nikampa jibu hili baada ya hapo yeye akaniandkia kuniambia kuwa ‘si mimi asilani niliyekuotesha ndoto hizo hizo bali ni Allah kwa hiyo kama unataka kulaumu basi mlaumu Allah aliyekuleta katika njia hii ya ukadiyyani” mimi nikaendelea kuwajibu kuwa kwa hakika ile ndoto niliyoota alikuwa si mwingine bali ni Mustafa Muhamma[SAW] viongozi wa jumuiyya ya Ahmadiyya wakaendelea kunieleza kwa kuniambia ‘hivi wewe una hakika kweli sio Mirza ghulam aliyekutokea ndotoni au sio mmoja wa makhalifa wake?” nikaendelea kuwajibu kuwa je ndoto hiyo hawezi kuoteshwa mtu atakayejitoa katika njia ya Ahmadiyya je mwaweza kusema kuwa ndoto hiyo ndio wanaoteshwa watu wenye kufuata itikadi ya kadiyyani peke yake labda ninyi makadiyyani mwaweza kuniambia mbona mimi nimejitoa katika njia yangu ya uislamu na kuingia katika jumuiyya ya Ahmadiyya ni kweli nakubali mimi nilitoka katika njia ya uislamu lakini ikaja kunibainikia dhahiri kuwa shahiri kwamba ukadiyani ni upotevu wa wazi kabisa na ni ukafiri pasina shaka
Kisa cha mwisho
Mirza Ghulam wa kadiyyani aliandika kitabu kiitwacho ‘The philosophy
of teaching of islam”[falsafa ya mafundisho ya uislamu] kiongozi wa shura
akapendekeza nisome kitabu hiki baada ya mimi kuwaomba wanipatie vitabu
vilivyoandikwa na mwasisi wa ukadiyyani tokea utotoni mwangu hii ilikuwa
ni mara ya kwanza kusoma kusoma kitabu kilichoandikwa na mwanzilishi wa
dini ya ukadiyyani.
Kwa rehema za Allah kitabu hiki kidogo kikanipa maelezo ya kutosha kumbaini mtu muongo na muhalifu wa misingi ya uislamu katika tafsiri ya kiingereza ya kitabu hiki jambo ambalo mimi limenishangaza ni tafsiri ya sura 102 ya qur an [surat takathur ambayo ina aya 8] Mirza ameifasiri vibaya mno tena ovyo kabisa.
Amefanya hila kubwa ili kuipa nguvu tafsiri anayoitaka yeye mwishoni ameongeza jambo ambalo halikuelezwa kabisa katika aya zote na nalo ni “ninyi mtaijua jahanam kutokana na hisia zenu” [Taz.Ahmad Mirza Ghulam;The philosophy of teaching of islam London[1992]uk.75]kwa kweli huu ni uhalifu mbaya sana na mtu mwovu tu ndiye anayeweza kuthubutu kufanya hivi kwa hiyo Mirza Ghulam Ahmad ni DAJJAL[mrongo mkubwa]kwa sababu hii ndio maana mimi nimejitoa kwenye mtego wa makadiyyani.
Maelezo yangu kuhusu hali ya ukadiyyani nchini Ubelgiji
Kiongozi wa harakati za ukadiyyani pamoja na kiongozi wa shura wamekataa
katakata kunipa maelezo kuhusu idadi ya makadiyyani nchini ubelgiji ninaposema
kukataa sina maana kuwa wamesema hatuwezi kukupa idadi hiyo bali wanapiga
chenga kujibu wazi kuwa ukadiyyani hauna nafasi ubelgiji.
Kwa utafiti wangu makdiyani kwa hapa wako200 tu[wakiwemo na watoto
wao]wengi wao wanatokea Pakistan wasio wapakistan walioingiakatika
ukadiyyani ni 10 tu katika kipindi cha miezi mitano ya kuwemo kwangu katika
ukadiyyani nilishuhudia watu wawili wakijitoa katika jumuiyya hii ya upotovu
watu hao sikuwaona tena wakija kituoni kwa miezi chungu mzima mimi nilimuuliza
kiongozi wa shura je vijana hao wawili wako wapi akawa hana jibu
kabisa la kunipa.
Huu muhtasari tu sikueleza mengi sana yaliyonipelekea kuuona ukweli na hatimaye kuuacha ukadiyyani na kurejea katika uislamu mapungufu yote niliyoyagundua kunahitaji ufafanuzi wa kina kwa hiyo nitawaleza zaidi mengi yaliyomo katika ukadiyyani InshaAllah nitawaelezeni siku nyingine