Harakati
za Ahmadiayya na uzushi wa takwimu
Kupindua na kugeuza ukweli na takwimu ilikuwa ndio tabia ya
Mirza Ghulam Ahmad, mwasisi wa harakati za Ahmadiya. Mirza alijenga mazoea ya kucheza na takwimu, akiwa na
lengo la kuvuruga ukweli akilenga kuwadanganya wafuasi wake na umma kwa ujumla.
Tabia hii haikukomea kwake, imekuwa ikiendelezwa na wafuasi wa kundi hilo hadi
hii leo. Kwa miaka kadhaa sasa, Mirza Tahir kiongozi wa Ahmadiya hivi sasa
amekuwa akijigamba kuwa na maelfu ya watu wanaojiunga na kundi hilo kila mwaka.
Amekuwa akiongeza mara dufu ya idadi hiyo kila mwaka. Kwa mfano mwaka 1998
Mirza Tahir alidai:
“Katika kipindi
changu cha miaka 16 ya ukhalifa, idadi isiyohesabika ya wafuasi imeongozwa na
Mungu kuja katika uahmadiya. Kwa mwaka mmoja tu watu 3,000,000 waliingia
uahmadiya, hiyo ilikuwa baraka kubwa ambayo hata zile nchi maarufu haziwezi
walau kuota kupokea wageni wa idadi hiyo”.(Kauli aliyoitoa Mirza tahir mamo juni
10, 1998, yaliyochapishwa na Afazl International la juni 26 –julai 2, 1998 uk
4).
Katika kauli
yake nyingine aliyoitoa tarehe hiyo hiyo na kuchapishwa katika toleo hilo hilo,
Tahir alidai:
“Kwa wakati huu,
Jamaat (Ahmadiya) imejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuongezeka na kufikia idadi ya
wafuasi milioni 10,000,000 na siku zijazo inatazamiwa kuongezeka zaidi kwa kuwa
katika kila mwaka makumi ya milioni huingia Jamaat”.
Hivi karibuni
Qadiani walidai katika moja ya mijadala iliyohusu uqadiani kuwa idadi yao
ilikuwa 10,000,00 mpaka mwaka ”.
Wakitumia
tarakimu hizo za uongo, Maqadiani huhoji iwapo wao ni waongo mbona watu
wanamiminika kujiunga na uqadiani kiasi hicho.
Kwamba mpaka
mwaka 1998 walikuwa wamepata wafuasi zaidi ya milioni 10,000,000. Kwa hiyo
Mirza Tahir kiongozi wa kundi hilo la wadanganyifu amekuwa na matarajio kwamba
kila mwaka idadi hiyo itakuwa ikiongezeka mara mara mbili zaidi.
Likitazamwa
kwa mazingatio dai hili ni rahisi kuibua maswali mengi, moja wapo je upo
uwezekano Ahmadiya kupata idadi hiyo kubwa ya wafuasi katika kipindi cha mwaka
mmoja tu. Takwimu hizi zinaingia akilini kweli! Ni labda kwa mtu aliyepunguani
anayeweza kukubali majigambo haya ya kiwendawazimu. Ni namna gani mtu huru
anavyoweza kuyathibitisha madai haya. Ni vigumu sana kufanya sensa kuwajua
maqadiani kwa vipimo vya kimataifa.
Umuhimu wa takwimu
Mirza Ahmad
aliahidi kuandika juzuu 50 za Braheen
Ahmadiya na akatangulia kuchukua malipo(advance
payment). Kutokea mwaka 1880-1884 akaandika juzuu 4 tu. Baada ya juzuu hizo
4, akaacha kuandika mfululizo huo, badala yake akageuka kuandika na kuuza
vitabu 80 alivyoviita Roohani Khazain
kwa miaka 25. Baada ya hap akarejea kuandika juzuu ya tano ya Braheen-Ahmadiyya kisha katika neno la
awali la juzuu hiyo akatahayari kuandika ifuatavyo:
“Awali nilikusudia
kuandika juzuu 50, lakini nimelazimika kukomea juzuu hizi 5 tu
kwa kuwa tofauti ya kati ya namba hizo mbili(50 na 5) ni ile sifuri iliyoko
kwenye 50, kwa ajili hiyo ahadi
yangu(ya kuandika juzuu 50) imekamilika kwa kuandika juzuu hizi 5”.
Sambamba na
kauli hiyo, akatangaza kuandika kitabu kingine alichokiita Arbaeen kwa kukigawanya katika sehemu sehemu 40. Kama ilivyokuwa
katika Braheen, Mirza alipokamilisha kuandika sehemu 4 akaacha kuandika kitabu
hicho na kudai:
“Kama Mwenyezi Mungu
alivyofanya katika kufardhisha swala alianza na idadi ya 50 akazipunguza hadi
kufikia 5 mahala pa 50, vivyo hivyo kwa sunna hiyo ya Mola Karim, nazipunguza
juzuu hizo na kuzifanya 4 mahala pa 40”.(Arbaiin N 4. Roohani Khazain
juzuu ya 17 uk. 442).
Majigambo kuhusiana na kukua kwa Uhmadiya
Katika
kipindi cha uhai wake, Mirza Ghulam alidai katika vitabu vyake mbali mbali
kwamba ana mamia ya maelfu ya wafuasi waliochukua ahadi kwake. Kuhusiana
na dai hilo aliandika:
“Mwenyezi Mungu
ameisheheneza wafuasi wangu miji ya Punjab na India. Kwa mika michache tu zadi
ya watu laki moja wamekula kiapo mbele yangu”.(Risala Tohfatun Nadwa, Roohan Khazain juzuu
ya 19 uk. 101).
Katika
matamshi mengine Mirza alidai:
“Naweza kuapa kwamba watu 100,000 katika Jamaat Ahmadiya wamenikubali mimi
kikweli kweli na wanajitahidi kuwa waadilifu na wanaposikiliza hotuba zangu,
hutokwa na machozi yanayolowanisha hadi kola za mashati yao”.(Mirza semi za Mirza Ghulam zilizotajwa katika Sira ya
Mahdi, sehemu ya 1uk. 165, riwaya
N 157 na Mirza Basheer Ahmad(Mirza Ghulam).
“Mwenyezi Mungu amenitukuza mimi katika nyanja zote. Kwa hivyo ningepaswa
kumshukuru mara alfu kwa kuwa watu
400,000 wameungama dhambi zao
kwangu na wameahidi kuachana na ukafiri.(Tutamma Haqeeqattul Wahi, Roohani Khazain juzuu ya 22 uk. 553).
“Mara zote nimekuwa nikiwashauri kwa hisia wafuasi wa Jamaat walioko sehemu mbali katika miji ya Punjab na Hindustan ambao kwa
fadhila zake Mwenyezi Mungu, idadi yao inafikia mamia ya maelfu, kwamba
wanapaswa kuyakumbuka mara kwa
mara mafundisho yangu niliyoyapandikiza katika vichwa vyao kwa hotuba na maandiko
kwa muda wa miaka 26, yanayowaamrisha kuitii serikali hii ya Uingereza”(Matangazo yaliyoitwa “malekezo muhimu kwa wana jamaat
wenzangu, mkusanyo wa matangazo I]k,=8juzuu 3 uk. 583).741
Katika
gazeti rasmi la propaganda za maqadiani, yametolewa madai ya majigambo. Katika
gazeti lao hilo waliandika kama ifuatavyo katika tahariri:
“Yaa Masiha Mowood, ujasiri, matumaini na matarajio yako yanadhihirishwa na
ukweli huu kwamba kwa mitume wengine wajibu wao ulikuwa kupata tu watu
wanaowakubali kuwa wao ni mitume, lakini kwako kulikuwa na ugumu wa namna
mbili: Ule wa kukubalika kuwa kuna mtume mwingine atakayekuja na ugumu mwingine
ni ule kukubalika kuwa wewe ni mtume. Hivyo umelifanya jambo hili kama nguzo ya
imani kwa watu 400,000”.( Gazeti la AlBadri,
Qadiani, juzuu ya 8 n 30 uk. 4 tarehe 11n20 mei 1909, Qadian, Qadian
Madhab toleo la 1995 uk 500.
“Baada ya kusoma tamshi hili(lililotajwa hapo juu) hapakuwa na shaka yoyote
kwamba 1909 Jamaat ya watu 400,000 walimkubali Masihi Mowood, Hazrat Ghulam
kama ni mtume”. (AlFazl Newspaper, Qadian, uk.
11n67uk.67 tarehe 26 februari 1924, Qadian Madhhab toleo la 1995, uk 500).
Aliyekuwa
akijiita mtume, mara Masih mara Mahd alitoa matamshi hayo kukonga nyoyo za
Wanajamaat la kuchekesha aliyemfuatia, Mirza Basherudii Mahmud, Khalifa wa
pili, naye akaiga maneno hayo. Kwa maneno yake Khalifa huyo alidai:
“Naweza kuthubutu kuwaambieni idadi ya wafuasi wa jamaat inakadiriwa
kufikia watu 400,000 mpaka 500,000. Kundi la Ghair Mubain la mijini Lahore lina
watu 1000 hivi”.(Kauli ya Mirza
Basheer mbele ya mahakama iliyotajwa katika gazeti AlFazl Qadian tarehe 26
mpaka 29 juni 1922, juzuu ya 9,n 101-102, uk. 6, Qadian Madhhab toleo la 1995,
uk 500).
“Sisi Ahmadiya zaidi ya laki 400,000 tunajiandaa kuwapeni mikono(Wahindu)
iwapo mtakubali masharti yaliyotajwa
Paigham”.(Tangazo la Khwaja Kamaludin, tarehe 15,
1908 lililotajwa katika Paigham Sulh uk.6 Qadiani Madhhab toleo la 1995, uk.
1905.
“Katika kesi ya Akhbar ‘Mubahila, mashuhuda wa Ukadiani wanatajwa kufikia
1,000,000. Mnamo mwaka 1930, kwa mujibu wa Mwandishi wa kijitabu cha ukadiani
‘Kaukab Daree’ alidai kuna zaidi ya Makadiani 2, 000,000 duniani kote. Katika
mdahalo uliofanyika mwaka 1932
mjini Bheerah(Punjab), Maulana Mubaraka Ahmad Saheb, Profesa Jamia
Ahmadiyya Qadiani, walidai kwamba watu waliokubali ukadiani wanafikia
5,000,000. Hivi karibuni Abdulrahim Dard, mlinganiaji wa ukadiani alitoa
matamshi akidai mbele ya Bwana Philby nchini Uingereza kwamba miongoni mwa
Waislamu mjini Punjab wengi wao ni Maqadiani,. Punjab ina zaidi ya Waislamu
Milioni 15, hii kwa mujibu wa Abdulr Rahiim Dard inamaanisha wapo makadiani
zaidi ya 7,5000, katika mji wa Punjab.(Risala Shamsu
Islam, Bheera, Punjab, juzuu ya 5 N 10
Madhehebu ya Qadiani toleo la 1995, uk.50).
Khawaja Hasan Nizami Saheb alidai kwamba Mian(Mahmud Ahmad, Khalifa Qadiani
hawezi kuonesha orodha ya Muridi japo 20,000 kwa sababu kwa mujibu wa Khawaja
Saheb idadi ya jumla ya Ahmadiyya wote Mjini Hindustan haizidi 18,000. Sijui
Khawaja Saheb ana hoja zipi zilizompelekea akione kikundi cha Ahmadiaya kama ni
cha watu laki 4-5 wakati ambapo hawazidi 18,000. Hiyo ndio kusema, hapana shaka
dai la Mian Saheb kwamba yeye ndiye Imam wa watu laki nne mpaka
tano(400,000-5000,000) halina msingi wowote.(Akhbar Paigham Sulh, Lahore uk. 5 N 59 ya tarehe 6 Februari 1918).
“Lakini wakati hesabu ya watu ikifanywa na serikali ya Uingereza mnamo
mwaka 1911 na mwaka 1931, fumbo lote la kukua kwa uhamadiyya liliporomoka na uongo wa Mirza Ghulam
A. Qadiani na waliomfutia ukadhihirika na kuwatia aibu. Idadi halisi ya watu waliokuwa wakiufuata ukadiani
mjini Punjab ambako ndiko ngome kuu ya itikadi hiyo, haukuzidi 55,908.(Mnamo
mwaka 1921 idadi ya watu ilikuwa 28,816).( Sensa ya Punjab, Part 1-Ropoti, uk. 313,
na Khan Ahmad Hassan Khan, M.A.A., K.S, Msimamizi wa sensa, Pumnjab na Delhi).
Ndugu Msomaji
Imekudhihirika
ni namna gani Jamaa wa Makadiani wamekuwa wakiwadanganya watu, akiwemo Mirza
mwenyewe, wafuasi wao na magazeti yao. Mirza tahir, Mubashir(Khalifa) wa nne
baada ya Mirza naye kadhalika yumo katika hao wanaoendelea kuwadanganya watu
hivi sasa. Kwa maneno yake anasema:
“Katika kipindi cha miaka 16 ya Ukhalifa wangu kumekuwa na wimbi kubwa la
watu kuingia katika Ukadiani na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwaka mmoja tu
Uahmadiya ulifanikiwa kupata wageni 3,000,000 hii neem ambayo hata Mataifa
makubwa hayangeweza kuiota”.(haya ni matamshi
aliyoyatoa Mirza Tahir tarehe 10 juni 1998, na kukaririwa katika Alfazl
International, tarehe 26 juni-Julai 2 1998. Uk.4).
“Kwa wakati huu, Jamaat (Ahmadiya) imejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuongezeka
na kufikia idadi ya wafuasi milioni 10,000,000 na siku zijazo inatazamiwa
kuongezeka zaidi kwa kuwa katika kila mwaka makumi ya milioni huingia Jamaat”.
Kama ambavyo Mirza Ghulam alivyowadanganya wafuasi wake
kuhusian na kukua kwa Uahmadiya, ndivyo walivyofanya waliomfuatia na Khalifa wa
sasa, Mirza Tahir amekuwa akiwadanga wafuasi wake kuhusiana na kukua kwa
itikadi yao.
Tunatumai
kwa ukumbusho huu mdogo Makdiani watajaribu kuuona ukweli. Mirza Tahir hvi sasa
akionekana mwenye kukata tamaa amekuwa akijitahidi kuwatia moyo wafuasi wake
kwa upande mmoja na kwa upande wa pili na anajaribu kuwashawishi wafadhili wake
wa nchi za magharibi kwamba misaada yao inaendele kuzaa matunda na kwamba
uahmadiya utashika mahala pa Uislamu kwa kuwa ni itikadi inayokuwa kwa haraka.
Ni kwa watu wapuuzi na mataahira
wanaoweza kuamini propaganda hizo. Ukweli unajieleza wenyewe. Amkeni kabla
hamjachelewa:
“Haqeeqat Chup Naheen sakte banawat kay usoolon say(Ukweli hauwezi kufichwa
na uongo) Khushboo a naheen saktee kaaghaz ka phoolon say ( na harufu nzuri
haiwezi kutokana na uwaridi bandia).
Wassalaam
alaa manittaba’al Hoodaa(amani iwe juu ya wale wanaofuata uongofu).
Dr.
Syed Rashid Ali
Box
11560
Dibba
alfujaira
United
Arabs Emirates
http:/alhafeez.org/rashid
rasyed@emirates.net.ae