Imani
hii katika ujumbe na mtume wa mwisho na ukamilifu wa dini yao ndicho kitu
kinachotofautisha taifa la kiislamu na dini nyingine na kitu hicho kinakuwa
kama kizuizi dhidi ya harakati zote za uasi wa kidini na nguvu zote zinazochangukana
au zinazotengana ambazo ulimwengu mpana wa kiislamu. Quran, vitabu vya
Hadithi na sira, vitabu vya Taarikh (vitabu vya historia) na maandiko matakatifu
mengine ya dini nyingine vimethibitisha kuwa Syedna Muhammad (SAW) ni mtume
wa mwisho wa Allah (SW) na ni kisawe na imani ya ukamilifu wa dini na Quran
ni ujumbe uliofunuliwa au ni ufunuo toka kwa Allah (SW) kwa ajili ya kuongoza
viumbe wake.
Allah (SW)
anasema katika Quran:
“Muhammad
si baba wa yeyote katika wanaume bali yeye ni mtume na mwisho wa Mungu
na mwisho wa mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu (Quran 33:40).
Mtume
Mtakatifu Muhammad (SAW) alitangaza:
“Kwa
hakika utume na unabii vimesiamishwa. Kwa hiyo hakutakujakuwa na mtume
wala nabii baada yangu mimi”. (Tirmidhi, Juzuu ya 2 uk 51: Masnad ya Ahmed).
Mitume
wote wametoa (wametangaza) habari njema za ujio wa nabii mpya, lakini mtume
Muhammad alituonya kwamba:
“Katika
umma wangu kutazaliwa (kutatokea) waongo thelathini (30) kila mmoja akidai
kuwa ni mtume. LAKINI MIMI NI MTUME WA MWISHO (KHATAMUN – NABIYIIN) HAKUTAKUWA
NA MTUME BAADA YANGU”. (Abu Dawood, Tirmidhi)
JAMAA YA AHMADIYYAH NA CHUKI YAO DHIDI
YA UNABII WA SYEDNA MUHAMMAD (SAW)
Miongoni
mwa vikundi mbali mbali dhidi ya harakati za kiislam ambavyo mara kwa mara
vimejitokeza katika karne ya 14 ya historia ya kiislam, ukadiani u-ahmadiyyah
hauna kifani.
Mirza Ghulam
Ahmad Qadiani, muasisi wa harakati za Ahmadiyyah, ameshambulia ujumbe (Quran)
na mtume akiupinga unabii wa Syedna Muhammad (SAW) pamoja na kubadilisha
na kuvuruga ujumbe wa Quran. Wakijizuga na kujifanya kama wao ni mabingwa
wa kiislamu, wanaeneza itikadi yao ya uwongo wakinufaika na ujinga walionao
waislamu katika sehemu nyingi za ulimwengu.
Kwa ujumla
waislamu wanajua misingi ya kiislam. Lakini hawajui udanganyifu mtakatifu
wa Ahmadiyyah katika jina la uislam. Watu wachache wanaelewa kwamba mtu
huyu ambaye alianza kama mhubiri na mlinzi wa uislamu, alifundishwa na
bwana zake wa kikoloni (British Raj) kudhoofisha mapenzi kwa mtume Muhammad
(SAW) katika mioyo ya waislamu kwa kuvuruga na kubadilisha mafunzo ya Quran
na hivyo kujaribu kuugawa ummah wa kiislamu.
MIRZA GHULAM ALIDAI KUWA MTUME
“Wafu
ni wale ambao hawakumkubali mtume mmoja. Aliyebarikiwa ni yule aliyenitambua
mimi. Miongoni mwa njia za Allah mimi ni njia ya mwisho na katika taa zake
zote mimi ndio taa ya mwisho Mkosefu wa bahati ni yule anayenitupa kwa
kuwa bila mimi kuna giza totoro”. (Kishtee-e-Nooh, Roohani Khazain Juzuu
ya 19.uk.61)
BAADAYE ALIDAI KUWA
UJIO WA PILI WA MTUME MUHAMMAD (SAW)
"Muhammad
mMume wa Allah na wale walioamini ni wakali kwa makafiri, wanarehemeana
baina yao katika ufunuo huu (wahyi huu) Mungu ameniita mimi Muhammad na
pia mtume” (Roohani Khazain Juzuu ya 18, uk. 207)
“Pindi
ninapokuwa mfano au kiigizo cha mtume na utimilifu (mafanikio) wote wa
Muhammad pamoja na utume vinaakisiwa katika kivuli cha kiza changu, baadaye
ni mtu gani mwingine aliyedai utume?” (Ek Ghatti Ka Izala, uk 8 Roohani
Khazain, Juzuu 18 uk 212)
“Ni
mimi pekee niliyechaguliwa katika umma huu kupata jina la “Mtume” Hakuna
mtu mwingine ambaye anastahili jina hili na imepangwa kutokea hivyo …ili
kwamba kama ilivyotajwa katika hadithi iliyosahihi kwamba kutakuweko na
mtu kama huyo ambaye anatimilizwa katika bishara” (Haqeeqatul wahi, Roohani
Khazain Juzuu ya 22 uk. 407).
Kwa
hiyo Mirza aliiba heshima ya Khatam-Un Nabiyeeni – Mtume wa mwisho kutoka
kwa Mtume Muhammad (SAW) na akaitumia yeye mwenyewe. Baadaye Mirza anaweka
msingi wa umma ambao ni sambamba kwa kuita taifa lote la kiislam makafiri
na wanaharamu.
“Isipokuwa
kwa watoto wanaozaliwa na MALAYA, ambao mioyo yao imepigwa muhuri na Allah,
kila mtu ananiamini mimi na amekubali utume wangu. (Aina – e – Kamalat
– Islam, Roohani Khazain Juzuu ya 5 uk 547).
“Mungu
amenifunulia (kwa njia ya wahyi) kwamba mtu yeyote aliyefikiwa na ujumbe
wangu na hakunikubali basi sio Muislam” (Barua ya Mirza iliyotumwa kwa
Dkt Abdul Hakeem).
MATAMSHI YA MIRZA BASHIR,
Mwanae Mirza:
“Yeyote
anayemuamini Musa lakini hamwamini Yesu, au anamwamini Yesu lakini hamwamini
Muhammad, au anmwamini Muhammad lakini hamwamini Masihi aliyeahidiwa sio
kafiri tu lakini ni kafiri aliyethibitishwa na ametoka katika uislam”.
(Kalimatul Fasl, uk 110, - Mirza Bashir Ahmad)
MABADILIKO KATIKA QURAN NA JAMAA YA AHMADIYYA
Jamaa ya
Ahmadiyya inajivuna kwa kuchapisha misahafu ya Quran Takatifu katika lugha
nyingi. Kitu watu wanashindwa kukijua ni kuwa Mirza Ghulam na wafuasi wake
walijaribu kwa maksudi kabisa kupotosha ujumbe wa Quran. Mabadiliko hayo
yanaweza kufanywa katika njia zifuatazo:
-
Mabadiliko katika matini ya Quran
-
Mabadiliko katika tafsiri na ufafanuzi wa matini
-
Matumizi mabaya ya aya za Quran
-
Utanguzi na ubatilishaji wa sheria za Quran.
Mirza Ghulam
A. Qadiani ni mwenye hatia (mkosaji) katika makosa yote manne. Wakati msahafu
kwa lugha ya kiarabu haijabadilishwa maana, ametoa mchango mkubwa katika
kupotosha tafsiri, ufafanuzi na matumizi mabaya ya aya zake mbalimbali.
MABADILIKO KATIKA MATINI YA QURAN
Japokuwa
matini ya kiarabu ya msahafu wa jumuia ya Ahmadiyya haukubadilishwa, lakini
Mrza Ghulam amebadilisha matini ya aya mbalimbali za lugha ya kiarabu akivinukuu
katika vitabu vyake. Mifano michache inaambatanishwa katika ukurasa huu.
MABADILIKO KATIKA
TAFSIRI NA UFAFANUZI:
Mifano
ya mabadiliko ya maana za Quran ni mingi, mashuhuri zaidi ikiwa aya 33:40
“Muhammad
si baba wa yeyote katika wanaume wenu bali yeye ni mtume wa Mungu na mwisho
wa mitume. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu”. Kutokana na aya
hii na hadithi ya mtume kuhusiana kuwa kwake mwisho wa mitume wa Allah,
karne zote waislamu wamekuwa wakiamini kwa pamoja kuwa mtume Muhammad (SAW)
kuwa mtume wa Allah (SW) Khatam – Un-Nabiyiin. Lakini muulize Qadiyani
au Ahmadiyya yeyote, mfuasi wa Mirza Ghulam, watasema hivyo hivyo. Hapana
hapana! Huu mhuri (Khatan) siyo mhuri wa kuhitimisha, bali ni mhuri wa
kuidhinisha ujio wa mitume wengine. Lakini hata hivyo baada ya kunyemelea
katika huu mlango wa nyuma wa utume,
(Mirza
Ghulam) anaufunga tena kwa kusema. “Atukuzwe yule ambaye amenitambua
mimi. Miongoni mwa njia (ziendazo) kwa mwenyezi Mungu, mimi ni njia ya
mwisho, na katika taa zake zote, mimi ni taa ya mwisho. Amekosa bahati
yule ambaye ataacha kunifuata mimi, kwa sababu bila mimi vyote vitakuwa
giza” (Roohani Khazain, Juzuu ya 19, uk 61).
Lakini
hawatakuwa na ibu kwa swali hili: unamuitaje mtu anayeiba cheo au (heshima)
Khatam – Un-Nabiyiin kutoka kwa mtume mtakatifu? Watu hawa wamepigwa na
bumbuwazi!
MATUMIZI MABAYA YA AYA ZA QURAN
Quran takatifu
imejaa aya ambazo Allah anamsifu kipenzi mtume wake Muhammad (SAW). Kwa
mfano Quran 9:33, 17,1, 3:31, 48: 1 – 2, 36:1 – 3, 108:1, 21: 107 n.k.
zote ni aya mashuhuri ambazo ziliteremshwa hususan kumsifu (au kumtukuza)
mtume wa kiislam.
Kwa hali
yoyote ile fungua vitabu vya Mirza Ghulam, hususan Haqeeqatul wahi, Juzuu
ya 22 Roohani Khazain, na utaona kuwa toka kurasa 77 hadi 111 wizi wa maandishi
usiokuwa na haya wa matini ya Quran inayotajwa na Mirza kama kielelezo
ufunuo au uzinduzi ulioletwa kumsifu Mirza kwa mfano:
-
“Ni yeye aliyemleta (aliyempeleka) mtume wake na mwongozo
na dini ya haki, ili iweze kushinda dini zote” (As-Saff 61:9) (Tazkirah
uk. 387 – 388 toleo la 4).
“Sema (ewe
Muhammad, kwa wanaadamu):
-
Kama mnampenda Mwenyezi Mungu, nifuataeni mimi, mwenyezi
Munguatawapendeni” (Aal-Imran 3:31) Haqiqat-ul-wahi, uk 82).
-
“Wala hasemi kwa matamanio yake (ya nafsi yake) hayakuwa
haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake)” (An-Naju
53:3-4) (Tazkirah. uk 378).
-
"Sema (ewe Muhammad) Enyi watu hakika mimi ni mtume wa
Allah kwenu ninyi nyote” (Al-A’raf 7:158) (Tazkirah uk, 352 toleo la
4).
-
“Bila shaka wale wanaofungamana nawe. (Muhammad) kwa hakika
wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Uwezo wa Allah uko juu ya uwezo wao” .
(Sarat Fath 48:10) (Haqiqatul-wahi, 80).
-
Sema mimi ni binaadamu kama ninyi, mola wangu ananifunulia
(ananiletea wahyi) kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja” (surat Kahf 18:110)
(Haqiqat-ul-wahi uk 81)
-
“Bila shaka tumekupa (ewe Muhammad) kushinda kuliko dhahiri
ili mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja”
(Surat Fath 48:1-2) (Haqiqat-ul-wahi uk. 94)
-
“Hakika sisi tumekuleteeni mtume aliyeshahidi juu yenu, kama
tulivyompeleka mtume kwa Firauni”. (Surat Muzammil 73:15) (Haqiqat-ul-wahi,
uk 101).
-
“Hakika tumekupa kheri nyingi” (Suratul Kauthar 108:1) (Haqiqat-ul-wahi,
uk 102).
-
“Yaa Syn, Naapa kwa hii Quran yenye kutengenezwa vizuri (iliyojaa
hekima) kuwa hakika ya wewe ni miongoni mwa mitume (wa mwenyezi Mungu)
waliotumwa juu ya njia iliyonyooka” (Suratul-Yasin 36:1-4) (Haqiqat-ul-wahi
uk. 107, Tazkirah uk. 479).
-
“Na (wewe Muhammad), hukutupa wewe ule mchanga katika gao
lako la mkono ulipotupa, lakini Allah ndiye aliyeutupa (Suratul-Anfal 8:17)
(Haqiqatul wahi uk. 70).
-
“Aya ya Quran Takatifu (17:1) Subhana ladhi asra be’abdihi
lailan min al-masjid al haram ila almasjid alaqsa… “Utukufu ni wake yeye
ambaye alimpeleka mja wake usiku (mmoja tu) kutoka msikiti mtukufu (wa
Makka) mpaka msikiti wa mbali (wa Baitul Muqaddas) – Masjid Aqsa… matumizi
yake halisi ni ule msikiti ambao umejengwa na baba yake Mirza na ambao
upanuzi wake umefanywa na Mirza”. (Makusanyo ya matangazo, juzuu ya 3 uk
286)
Hebu fikiri
kwa karne nyingi waislamu walikuwa wapumbavu kupigania umiliki wa mji mtakatifu
wa Jerusalem. Kutokana na Mirza Ghulam, Masjid Aqsa (msikiti wa Jerusalem)
uko Qadian na mtume mtakatifu alienda Qadian na sio Jerusalem usiku wa
Miiraj. Huduma ilioje kwa Mayahudi!!
UBATILISHAJI WA SHERIA ZA QURAN
Dhana ya
Jihad katika uislam ni vita ya halali iliyo na malengo na makusudi yaliyowazi:
Kukomesha uonevu (au udhalimu) ili kuihifadhi haki ya mtu katika makazi
yake na uhuru katika Taifa lake, kuzuia mateso katika dini na kuhakikisha
kuwepo uhuru wa imani (ya dini) kwa watu wote.
Allah
anasema:
“Na
piganeni nao mpaka kusiwe na mateso, na dini iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa madhalimu. (Quran
2:193)
“Na
waueni popote muwakutapo, na muwatoe popote walipokutoweni…” (Quran
2:191)
“Na nyote
piganeni na makafiri kama wao (wote) waanvyopigana nanyi; na jueni kwamba
Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaomuogopa. (Quran 9:36)
Licha ya
makatazo au amri hizi za wazi toka kwa Mwenyezi Mungu, kutokana na amri
za wakubwa wake, Mirza Ghulam alitangua (alifuta) au kubatilisha wazo la
Jihad. Aliandika:
“Kutokana
na umri wangu mdogo hadi sasa nikiwa na umri wa miaka 65, nimejishughulisha
na kalamu na ulimi, katika shughuli muhimu ya kugeuza mioyo ya waislamu
na kuelekea mapenzi ya kweli na urafiki na upole kwa ajili ya serikali
ya kiingereza na kuondosha kabisa (kufitilia mbali) wazo la Jihad kutoka
katika mioyo ya waislamu wasio na akili (wapumbavu)”. (Kitabu-ul-bariyah,
roohani Khazoin Juzuu ya 13 uk 350).
“Kwa
ajili ya serikali ya kiingereza, nimechapisha na kusambaza kurasa zenye
matangazo 50,000 katika nchi hii na nchi nyingine za kiislamu (dhidi ya
Jihad)… matokeo ni kwamba mamia ya maelfu ya watu wametupilia mawazo yao
machafu kuhusu Jihad” . (Roohani Khazain, Juzuu ya 15 uk. 114).
Ni matusi
kama haya dhidi ya Mtume mtakatifu wa kiislamu na majaribio ya kugeuza
au kubadili ujumbe wa Qurani uliopelekea au kuufanya umma mzima wa kiislamu
kutamka au kutangaza kuwa Mirza Ghulam na Jamaa ya Ahmadiyyah kuwa ni makafiri
na kuwa wametoka nje ya uislamu. Lakini wanaendelea kujigamba kama wao
ni mabingwa wa uislamu wakiwashawishi waislamu wajinga na wasio na hatia
hasa wale waliopo Afrika tokana na uislamu aliokuwa nao Mtume Muhammad
(SAW) kuelekea katika kanuni ( au itikadi) ya udanganyifu ya Mirza Ghulam,
iitwayo Ahmadi Islami (uislamu wa Ahmad).
(Tunamuomba)
Allah, awaepushe waislamu wote na udanganyifu huu katika jina la uislamu
na kuwaonyesha wafuasi wa Ahmadiyyah walio wajinga, sura halisi ya Mirza
Ghulam Qadiani, kwa kuwa (itikadi zake) haziafikiani na maandiko yake ya
asili. Amin.
Rehema na
Amani kwa wale wote wanaofuata mwongozo.
Dkt. Syed
Rashid Ali
P.O. Box
11560
Dibba Fujairah
U.A.E