Bismillah Al-Rehman Al-Raheem

Anti Ahmadiyya Movement in Islam

Miaka Mia ya Vurugu la Ucha Mungu 

Na. B.A. Masri

ALFATWA 7A YA KIMATAIFA


12th January 1998

Ndugu Wapendwa akina Kaka/Dada katika Uislam

Assalam Aleikum wa Rahmatullah.

Ukadiani ambao pia unajulikana kama Umirza au Ahmadiyya umekuwa jambo lenye ubishani mzito siku hizi, kote Ulimwenguni, Waislam wameanzisha kampeni dhidi ya Jumuia hii katika Uislam. Kwani inakuwa hivi? Kwa nini upinzani wetu dhidi yao unakuwa mkali sana miaka hii ya karibuni?

Nimekuwa nikiulizwa na vikjana wetu wa Kiislam, kwani tunakuwa imara sana dhidi ya Umirza Ahmadiyya wakati ambapo uislam unafundisha kusubiriana na kuvumiliana katika mambo yanayohusu elimu ya dini na tofauti zake. Hasa vijana wasomi wa Kiislam wa sasa wanadhani kuwa hatujisikiihivyo dhidi ya zile dini ambazo maadili yake yanapinga maadili ya Uislam. Kwa mfano kuna dini zingine ambazo huamini mitume wao kuwa ni watoto wa Mungu, wengine wanaabudu wanyama, wakati ambapo kuna wengine ambao hawaamini kuwako kwa Mungu kabisapamoja na kutofautiana kote huko katika Imani, tunaendelea kuwavumilia.

Waislam kama hawa wanajisikia vyema kuwaacha Mirzai peke yao na wafuasi wake wafuate njia yao wenyewe, kama wapendavyo. Ili kujua habari kamili ya jambo hili na maswala mengine mengi lazima kuchimba zaidi ili kuelewa ukweli wa asili ya Imani hii.

Je, jumuia hii ni ya marekebisho ndani ya Uislam, kama inavyodaiwa? Au ni vurugu la Ucha Mungu katika Uislam?

Wakati wa hatua za mwanzo za jumuia hii Ukadiani, miaka 100 iliyopita ujamaa wetu haukupata mshituko udanganyifu na ughushi wa mafunzo ya Imani ambayo Imani hii imeanza kupandikiza katika Theolojia na sharia ya Kiislamu. Walitarajia kuwa uzushi huu na upotofu huu, FITINA hii itakufa kifo cha kawaida kama mapote mengine yaliyokwisha shindwa ambayo yalijitokeza wakati uliopita kwa jina la Uislam, yamefifia hadi kufa. Hata hivyo jinsi muda unavyopita waligundua kuwa jumuia hii ni ya hatari.

Baada ya muda inadhihirika wazi kwa Waislam, kuwa Makadiani wamekuwa wateja wakarimu, kwa Rajwa wa Waingereza. Serikaliya kikoloni huko India katika muda huo walijua Waislamkuwa ni uadui wa dhati. Ni kabla ya miaka 35 nyuma Waislam walipokaribia kupata ushindi wa Kimapinduzi unaojulikana Kihistoria kama “Maasi ya 1857”. Uongozi wa Uingereza uliona kuwa Makadiani ni wasaliti wazuri wa kuvuruga ustawi wa mafunzo ya itikadi ya Kiislam na wakaanza kuwaunga mkono na kuwapa misaada.

Ilikuwa katika hali kama hizi tunapoona maandishiya Makadiani yakihubiri utii kwa serikali ya Kiingereza. Walifikiakutamka kwamba utii kwa mfalme wa Kiingereza ni wajibu wa kidini kwa waislamu walioko India. Kuunga mkono usemi auFatwa hii walinukuu ayaQuran inayotuamrisha kuwatii wale ambao wamepewa madaraka ya utawala juu yetu kumaanisha serikali ya kiingereza. Kwa kadiri yoyote wakati wannukuu aya hizi waliruka kifungu katika Quran kisemacho kwamba viongozi wachaguliwe kati yetu nayo ni kwamba lazima wawe waislamu.

Ulikuwa sio ule wakati wa siku za mwanzo ambapo ukadiani ulifanya kazi ya vibaraka kwa serikali ya kikoloni, bali tokea historia yao ya miaka 100 walikuwa wakishirikiana kisirisiri na maadui wa kiislamu. Ni siri iliyowazi kuwa katika juhudi za sasa za kimataifa kayika uwanja wa siasa, hasa katika mashariki ya kati (Makadiani) walitoa huduma za kutoa askari wa kukodishwa kusaidia adui wa wazi wa mataifa ya kiislamu.

Baadhi ya wenzetu wanavutiwa na uwazi wa muundo wa madhehebu haya na maoni yao ya ulaghai katika ufanisi katika ufunguzi wa nyumba zao za mahubiri katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Hawajui kuwa nyumba zile ni vituo vya upelelezi vinavyosingizia Da’wah au vituo vya Tabligh. Kwa jambo hili hata Makadiyani hawajui kinachoendelea nyuma ya jukwaa. Wanadhani kuwa maendeleo yote wanayoyaona yametokana na sadaka zao. Wakati ukweli ni kwamba fedha nyingi zinalipwa na shirika la Makadiani na kutoka nchi ambazo uhusiano wao wa kiuchumi na kisiasa ni wa kuzikwamisha na kuzitia hatarini nchi za Kiislamu. Maadui hawa wa kiislamu wanapata wafuasi wenye ari na makachero wenye manufaa. Inakuwa rahisi zaidi na salama zaidi kwa Wakadiani au ma-Ahmadiya kufanya kazi kama hivi, kwa sababu ya kueleweka kuwa wanafanya kazi katika vazi la uislamu na wao kukubalika na makafiri katika dhehebu ndani ya uislamu.

Umewahi kushangaa kwa nini katika miaka ya karibuni imekuwa ni rahisi mno kwa makadiani mna wa-Ahmadiya kuhamia nchi za ulaya na marekani wakati vizuizi vya uhamiaji kwa wengine vinazidi kuwa vikali? Nimesema mapema kuwa ugomvi au mapambano yaliyopo na dini hii ni kwa sababu ya lile dai lao la kinafiki la kuwa Waislamu. Ngoja nikuhakikishieni kuwa siyo kwa sababu kutowavumilia (au kutowastahimili) au imani mbaya ya kibubusa. Watu hawa basi basi wajitangaze kuwa wao wanafuata dini mpya. Kufuata mafunzo ya kiislamu kama yalivyo mambo tutakayowafanyia yatakuwa sawa kama yale tuwafanyiayo dini nyingine. Mafundisho yetu na dini nyingine yanatofautiana. Japouwa tofauti zetu ni kubwa tunajaribu kuzichambuakatika majadiliano yenye amani.hatuwezi kumuahcia laghai anayejifanya kuwa mmoja kati yetu kupotosha misingi ya dini yetu. hebu tuangalie mifano michache. Dhana ya umwisho wa utume katika uislamu ni ya asili na ya kipekee katika historia ya dini zilizopata ufunuo toka kwa Allah. Tunaambiwa kwamba hapajatokea kipindi ambacho Mungu hajatuma mjumbe (mtume) wake kwa kumwongozamwanaadamu na kwamba ni moja katikamasharti ya uislamu kuwa tunawajibika kuwakubali mitume wote kama mitume wa Allah. dHana yote imejengwa katika msingi kwamba, Allah analeta mwongozo wake kumuelendeleza mwanadamu kiroho polepole, kidogo kidogo kila wakati kutegemea na uwezo wa akili ya mwanadamu. Maendeleo haya ya kupata ufunuo kidogo kidogo kupitia kwa mtumehadi mtume yaliendelea hadi yalifikia muda ambao Mungu alileta sharia yake kupitia kwa Mtume Muhammad (SAW). Kufuatana na mwongozo huu waislamu wanaamini kuwa hawatakuja mitume baada ya mtume Muhammad (SAW) na kwamba yeyote atakayedai utume ima ni mwendawazimu au laghai au mnafiki.

Pindi Mirza Ghulam A. wa Qadiani alitangaza dai lake kuwa alikuwa mtume aliyetumwa na Mungu kama masihi aliyeahidiwa,umma wa kiislamu uliweka msimamo wake katika suala hili, na kumshutumu kamamuasi. Kama nilivyowahi kusema huu UASI WA KITHEOLOJIA (uasi wa kidini) au FITNA katika uislamu zingeweza kukomeshwa lakini kutokana na serikali ya kiingereza kuwa mlezi na sasa misaada ya kifedha anayopata kutoka nchi maadui na nchi za kiislamu, uasi huo haukuweza kukomeshwa.

Ingawa kuna madhehebu mengi katika uislamu tofauti zao ziko katika mambo madogo na yauchunguzi yanayohitaji ufafanuzi. Hakuna kutokuelewana wala ugomvi katika misingi ya imani. Mambo mawili yamechangia katika kudumu kwa ari ya udugu wa kiislamu kwa ujumla:

·Moja ni kukamilika kwa Quran Majeedkama neno la Allah.

·Pili ni mtume Muhammad (SAW) kuwa mtume wa mwisho

Kutingisha nguzo mbili hizi, jengo la uislamu litaanguka. Hivyo, Shakhsia ya Muhammad (SAW) akiwa kama mtume wa mwisho imekuwa kiini au chimbuko ambalo udugu wa kimataifa wa kiislamu unauzunguuka. Ni kwa maana hii, maadui ya kiislamu wanapojaribu kung’oamizizi ya kiislamu wanauliza uhalali wa Quran-Majeed na kukashifu Shakhsia ya Mtume (SAW). Tumezoea mashambulizi kama hayo kutoka nje na tunaelewa namna ya kushughulika nayo. Tatizo hasa linatokea wakati mtukutoka ndani anakuwa msaliti, kama wafanyavyo makadiani. Waweza kuepusha hatari ambayo waweza kuiona, lakini waweza usifahamu, ukagongwa na nyoka katika majani. Na hili ndilo lililotokea kwa baadhi ya waislamu.

Mirza Ghulam Ahmaed alipoanzishajumuia yake ambayo aliita ahmadiyyat, waislamu huko India walikuwa katika kipindi kigumu san. Missionari za Kikristo zilianza kampeni za nguvu za kuwabadilisha waislamu dini. Hata Wa-Hindu walianza kampeni kama hiyo ya kubadilisha watu dini chini ya chama kilichoitwa “Shudhil”. Juu ya mashambulizi yote haya, serikali ya kiingereza bado ilikuwa inatumia siasa yake ya kuwadhalilisha waislamu. Katika mazingira hayo ya kutisha ndipo Mirza Ghulam Ahmad alijitokeza. Katika maandiko yake ya mwanzo hakugusia au kudokeza kuwa yeye alikuwa mtume na masihi aliyeahidiwa.

Nilizaliwa Qadian mwaka 1914 na niliishi na watu hawa tangu mtoto. Naelewa kwa mtizamo wangu binafsi kuwa wengi kati ya wale walijiunga na chama hiki mwanzo walikuwa waislamu waaminifu ambao walidhani kuwa hiki ni chama cha kweli cha mageuzi katika uislamu.

Vyovyote ilivyokuwa wakati ulivyoendelea na habari zilivyoenea kwa watu, madai kabambe yalianzakuenezwa moja baada ya moja, pole pole sana na kwa siri kiasi kwamba makadiani wa kizazi cha tatu na cha nne hawawezi kuunganisha au kuhusisha jinsi walivyoghiribiwa. Hawajui kuwa Mirza Ghulam Ahmad yule yule baba zao walimkubali kwa makosa kama mtumishi wa mtume Ahmad amegeuka mtume Ahmad yeye mwenyewe. Kizazi cha sasa cha makadiani kimelishwa kasumba kukifanya kiamini kwamba utuma wa Mirza Ghulam Ahmad ni sharti laimani ya kiislamu. Imani hii ni muhimu sana kwao kiasi kwamba wale waislamu wasiokuwa makadiani ni makafiri!

Kwa makadiani wakifanya mambo yafuatayo wamekufaa; kumfuata muislamu katika swala, kumswalia maiti wa kiislamu; kufunga ndoa na mwislamu na mengineyo. Kwa wao mji wa Qadian umechukua mahali pa mji wa Makka.

Sehemu zake na viwanja vyake kwa wao vimekuwa alama au dalili za kuweko kwa mwenyezi Mungu; kwa maana ile ile Quran Takatifu ilivyoita sehemu tukufu za mji wa Makka kama alama za Allah, k.m. “Sha’air Alla. Mke wa mtume wao anapewa heshima ile ile ya mama wa waumini kama Ummul-ul-muumineen, kama vile vile heshima hii walivyopewa wake za mtume (SAW) na waislamu.

Khalifa wao wa pili niMirza Basheeruddin Mahmud mtoto wa Mirza Ghulam A. Qadian. Alianza kudai kwamba hadhi yake ya kiucha Mungu ya juu zaidi kuliko ile ya Hazrat Omar ibn Alkhattab, Khalifa wa pili wa msaliti huyu ni mpotoshaji mashuhuri na mfisadi.

Nimeweka kumbukumbuya maono yangu juu ya maovu ya kimaadili ambayo yalikuweko katika jamii ya Qadian. Jibu langu, undani wa wahusika na masualayao, na hali zilivyokuwa hata niliahca imani (dini) hii, yote haya yamechapishwakatika kijitabu kama barua ya wazi kwa Amir wa Makadiani. Inapatikana toka wka mvulana Sohail Hassan, 101 Belmout Road Tottenham London N17 680 – Wassalamo Alaikum. B. A. Masri June 1992.

Dr. Syed Rashid Ali 

P.O. Box 11560

Dibba Fujairah UAE

rasyed@emirates.net.ae

http://alhafeez.org/rashid/