BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM
Mara mbili au tatu kila mwaka wakaguzi huakikisha kuwa makusanyo ya michango yanafikiwa asilimia 100% Ili kutia msukumo katika ukusanyaji motisha utolewa. Wale watakaofikisha asilimia 100%majina yao yatapelekwa kwa kwa huzoor [mirza Tahir Ahmad Qadian sasa ni hayati kwa sasa hupelekwa kwa Mirza Tahir [sasa ameshafariki badala yake ni Masroor] kwa ajili ya kuombewa dua na nyakati fulani fulani majina yao yatakuwa yanatajwatajwa n.k
Kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha viongozi wa jumuiyya hutoa hotuba juu ya umuhimu wa chanda [mchango] na kusisitiza ukusanyaji wake na mwishoni mwa mwaka maelezo ya mchango huo hutolewa, ahadi za michango hutolewa na bajeti ya mwaka unaofuata hutangazwa.
Kwa kila mtu awe na kazi asiwe na kazi mchango wa tahreek jadeeed ni lazima.kuweza kufikia 100%ya makusanyo ya chanda tahreek jaded wakaguzi mbalimbali hutawanywa kutoka kituo kikuu, viongozi hutoa hotuba na chombo kizima cha jumuiya hushughulika na ukusanyaji wa mchango huu.
Mchango wa "chanda salana" nao lazima kila mwaka kima cha mchango huu ni asilimia 10%ya kipato cha mwezi kusisitiza makusanyo yake hotuba maalum hutolewa.nayo chanda ya ‘wakf jadeed’ pia ikaanzishwa ambapo mwanzoni ulikuwa mchango wa hiari lakini hivi sasa ni mchango wa lazima. Wakaguzi waliotajwa katika aina zote NNE za michango huja kutoka kituoni mara tatu kila mwaka kufuatilia makusanyo ya michango hii [chanda] wakaguzi hufika hata majumbani kukusanya michangokwa wanaotakiwa kutoa michango hiyo.
Mfuasi wa Ahmadiya ambaye mshahara wake ni Rs 3000 kwa mwezi anatakiwa kutoa angalau Rs 300 kwa mwezi katika michango hii kama mke,watoto na wazazi wako pamoja naye basi nao sehemu ya michango yao itatoka katika mshahara huohuo hivyo mtu huyu hutakiwa kutoa kati ya Rs3000 hadi500 kila mwezi.na asipolipa atalimbikiziwa katika hesabu yake ambapo mwisho wa mwaka atalazimika kulipa kati ya Rs3000 hadi4000 vilevile kama mtu anakipato cha Rs10,000 kwa mwezi basi ni lazima alipe zaidi ya Rs 12,000.
Mbali na michango hii hapohapo tena kuna utaratibu mwingine ni kuwa kama mtu anataka azikwe kwenye makaburi maalum ya makadiyyani ambayo huyaita "makaburi maalum ya peponi ya Rabwa"pindi atapofariki dunia italazimu kwamba badala ya ule mchango wa asilimia 6.25%[chanda Aam] atalipa asilimia 10% ya mali na atapeleka asilimia 10 ya mali yake kwa kiongozi wa Anjuman-e-Ahmadiyya na ataendelea kulipa asilimia 10%ya mapato yake yote huko mbele.
Masharti haya huanza kumbana tokea pale anapoazimia kuzikwa katika makaburi hayo sasa Kama mtu amekufa kisha maiti yake ikapelekwa Rabwah huku ikawa asilimia 10 ya mali yake bado haijapelekwa Kwa kiongozi wa jumuiya ya Ahmadiyya au Kama hajalipa michango mingine basi maiti yake huzuiwa kuzikwa hapo mpaka warithi wake wamalize kulipa michango hiyo vinginevyo maziko hayatafanyika kabisa. Kama mfuasi wa Ahamadiyya hatoi michango yote iliyotajwa hapa basi huwa si Ahamadiyya tena kama halipi chanda au kama anachelewesha malipo basi chanda hiyo itajilimbikiza akifa, itabidi ikusanywe kutoka kwa ndugu zake.
Yeyote yule mwenye madeni ya michango [chanda] jina lake litatangazwa hadharani na atachukuliwa kama muasi katika jumuiyya na mithili ya mnyama aliyekatwa mkia macho ya watu wote yatamwandama
Yeye ndiye aliyetakiwa awe mtu wa kushikamana zaidi na dini lakini angalia kafanya hijja ngapi? Yeye huyu ndiye aliyetangaza na kuwaambia waahmadiyya [makadiyyani] kwamba wale wote wasiokuwa wahamadiyya ni makafiri tena ni makafiri wa kutupa.
Waahmadiyya hawafanyi ibada ya Hijja kwa sababu ya vikwazo lakini wanatumia maelfu ya fedha [rupia] kwenda London kuhudhria jalsa salana muajiriwa wa serikali hawezi kuondoka nchini bila ruhusa maalum ya kiofisi lakini Ahamadiyya ambaye ni mtumishi wa serikali hufanya kila njia na kila aina ya ujanja kama kupata pasipoti za kughushi na kutoa maelezo ya urongo ili aende nje ya Nchi kuhudhuria Jalsa salana wanakwenda hata Qadiyyan kuhudhuria Jalsa salana kwa maneno mengine wanathibitisha kwa vitendo kuwa Jalsa ni muhimu kuliko Hijja.
Yule anayetoa pesa ndio hueshimiwa na kuwekwa mbele na yule asiyetoa pesa hudharauliwa.je Ahmadiya si inadai ni jumuiyya halisi ya kidini sasa vipi ukandamizaji huu wa tabaka la wenye nazo na masikini? Sasa ebu tutazame utaratibu wa uchaguzi wale wenye haki ya kupiga kura wote au baadhi yao ndio huwa viongozi mwanzoni kabisa mwa uchaguzi mtu mmoja husimama na kupendekeza yeyote yule kwa ajili ya nafasi yoyote ile.
Mtu ambaye jina limependekezwa yeye mwenyewe huwa hajui wala haombwi idhini yake na hata kama ridhaa yake atakataa kushiriki bado jina lake litakuwa miongoni mwamajina yaliyopendekezwa.
Halikadhalika mtu mwingine naye atasimama kumpendekezea mtu mwingine kwa ajili ya nafasi hiyohiyo kwa hiyo hawa wawili watakuwa ni wagombea wa nafasi moja hapo ndipo kura ya wazi hupigwa watu wataulizwa je wangapia wanaompendekelea yule wakwanza hapo hutakiwa kunyoosha mikono kama yule mgombea wa kwanza ni mtu mwenye mvuto basi kura zote humuangukia yeye na kama mgombea wa pili ana mvuto basi kura zote zitamsuburi yeye hakuna utaratibu wa kura za siri.
Ni dhahiri kuwa katika mikutano yote ya uchaguzi vijijini ni makabaila tu ni watu wa ovyo na wanapotoa kura kwa sababu tu wanauwezo na watu huogopa kumnyima kura kama huyo hali yakuwa yuko mbele yao akimuona kila mpiga kura.
Hivyo katika mikutano Kama hiyo pale mtu wa namna hiyo anapokuwa Amir au kiongozi ndio basi hubakia madarakani hadi kufa kwake kwani katika kipindi cha miaka mitatu uongozi wake hujiimarisha madarakani. Aidha jinsi utaratibu huo wa uchaguzi ulivyo ni kuwa mgombea haruhusiwi kuzungumza dhidi ya mpinzani wake hawezi hata kuzungumzia upande wake kwa wapiga kura. Hapo mtu fisadi huweza kuwa rais na kubakia kuwa hapo na atabaki katika nafasi hiyo kwani hakuna njia nyingine ya kumuondoa jumuiyya haiwezi kumuondoa kwani inasema wale waliomchagua ndio wanaweza kumuondoa je ni nani anaweza kumpigia kura ya kumkataa mtu na kujijengea uadui naye. Ni kutokana ana mfumo huo wa kizamanai usioleweka na uchaguzi ndio maana maamiri wengi wa jumuiya hukaa madarakani kwa muda mrefu kwa miaka na miaka.maamiri wa mijini na wilayani huweza kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka ishirini sehemu nyingine hata miaka 30 kuna eneo Fulani mtu anashika madaraka kwa miaka 47. Maamiri wote hawa hukaa madarani hadi kufa kwao na kwa sababu hiyo wanakuwa juu ya kanuni na taratibu na sera wao hutawala mithili ya madikteta.ni kwa sababu hiyo ya sifa hizi za maamiri ndio maana watu huachana na jumuiyya ya Ahmadiyya. Hali hii inaendelea kila kukicha wengi miongoni mwa wale wanaoondoka katika jumuiyya ni wasomi na wamekinaishwa na utaratibu huu mbovu usio na misingi ya uadilifu.
Sasa hotuba ya ijumaa ni wajibu wa kidini itakuwaje kwa Amiri wa jumuiyya kwa vile mtu kuwa Amir katika jumuiyya hakuna sharti la elimu ya dini na wala si lazima awe na elimu nyingine bali ukiwa mtoaji michango ndio sifa ya kuwa kiongozi wa jumuiyya yawezekana mtu akawa mbumbumbu ili mradi tu mtoaji michango basi ana haki ya kuwa Amir wa jumuiyya. Je mtu wa namna hii atakuwaje na uwezo kiutawala kwa hiyo Amir wa jumuiyya kwa namna zote na katika kila eneo liwe la utawala, kidini utungaji sera au jambo lingine lolote amir ndio ana uamuzi wa mwisho ni wake.hawajibishwi na mtu yeyote wala hawajibiki kwa mtu yeyote wala hawezi kupingwa popote kila shuri la kiutawala kila FATWA ya kidini itatoka kwake.
Kwakuwa Amir sasa ndio ana ghadhabu na mfuasi huyu wa dhati wa jumuiyya aliyempinga basi na ‘khalifa’ wa jumuiyya duniani naye humkasirikia mfuasi huyo wa Ahmadiyya bila kuzingatia malalamiko yake kama ni haki au la kwa sababu tu eti Amir wa jumuiyya ni mwakilishi wake hivyo ni sharti khalifa naye akasirike na kwa mujibu wa imani za Ahmadiyya mungu humkasirikia pia mfuasi huyo na kama kweli mungu hukasirika hivyo ebu fikiri hatima yako! na kama atamfurahia mtu basi naye mungu humfurahia mtu huyo kwa maneno mengine ni kuwa mungu anawajibika kufuata matashi ya Amir wa jumuiyya kwa hiyo kama Amir wa jumuiyya akiruhusu atakapokuwa radhi naye Ahmadiyya huyo mwenye kutaka uadilifu.
Mfumo uliotajwa juu ndio haswa unatumika katika kazi za jumuiyya kwa hiyo basi picha inayojitokeza ni kuwa mungu anafuata matakwa ya wakandamizaji, mafisadi na wahalifu wa kila mji kwa yeyote ambaye yeye ataomba asamehewe basi mungu atamsamehe na yule ambaye yeye atapendekeza atiwe motoni basi mungu atamtia motoni kila mfuasi wa Ahamadiyya kimoyoni atakubaliana nami ni kweli tupu niliyotaja lakini hatokubali kamwe kukiri haya hadharani.
Wasalaam
Munawwar A..Malik Profesa wa fizikia Jhelun