Bismillah Al-Rehman Al-Raheem

Anti Ahmadiyya Movement of Islam
7th Sept. 2003

Tatizo la ukadiani

(Na Sayid Abu’l Ala Maudud)

 

Wanazuoni wa Kiislamu wakiwakilisha jumuiya na vyama vya Kiislamu kutoka sehemu zote za Mashariki na Magharibi ya Pakistan walifanya Mkutano mjini Karachi kujadili maoni na mapendekezo ya serikali juu ya katiba mpya iliyowasilishwa Bungeni.

Mkutano huo ukamalizika kwa maoni na mabadiliko mengi (ya katiba) ambapo mojawapo ni; “…tunataka serikali iwahesabu wale wote wanamuamini Mirza Ghulam kama kiongozi wa dini kuwa ni jamii ya watu wachache sawa na jamii nyingine nyingi za watu wachache wasio waislamu nchini na iwape kiti kimoja katika Bunge la Punjab.”

Maoni mengine yalikuwa ni mazuri na ya wazi mno kiasi kwamba maadui hawakuweza kuyashambuliya, na pale waandishi wakorofi walipofanya hivyo, ushawishi wao haukuwa na maana miongoni mwa Wasomi.

Idadi kubwa ya Wapikistani wasomi hawakushawishika kuwa maoni yaliyotaka kutengwa kwa Makadiani yalikuwa ya busara na muhimu. Lakini hapa mimi nitafafanuwa kinagaubaga  kwa nini wanazuwoni wote wa Kiislamuwalikubaliana kuyatetea kwa pamoja maoni haya.

Kuwa jamii ndogo huru isiyo ya kiislamu ni jambo ambalo kiada na kimantiki, makadiani walilitaka wenyewe. Wao ndio waliosababisha na kusisitiza kila jambo ambalo limewapelekea kuwa jamii ya watu wachache wasiowaislamu.

Kwanza kabisa ni ule upotoshaji wao wa maana ya “Mwisho wa Mitume” ambayo kwayo wametofautiana na Waislamu wote wanaomuamini Muhammad (s.a.w) kama Mtume wa Mwisho na kwamba hakutakuwa na Mitume baada yake hadi siku ya hukumu.

Hii ndiyo maana ambayo Maswahaba wa Mtume waliielewa na ndiyo maana inayotokana na aya hii “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume” (33:40)

Maswahaba wa Mtume waliwapiga vita wale wote waliojifanya manabii baada ya kutawafu Muhammad (s.a.w). Na hii ndiyo maana ambayo Waislamu  waliielewa kutoka vyanzo vyote, na ndio kusema hawakumkubali na hawamkubali yeyote anayejifanya nabii.

Kwa mara ya  kwanza katika historiya ya Waislamu, Makadiani peke yao ndio waliotafasiri aya ya Qur’an, “Mwisho wa Mitume kuwa eti ina maana kuwa Muhammad ni Muhuri wa Manabii ambao unasadikisha na kusainisha utume wa Manabii wengine. Hiki tunachokisema chaweza kuthibitishwa na maandiko yaliyonukuliwa hapa kutoka katika vitabu na maandiko ya Makadiani. Hizi ni nukuu tatu.

Baada ya Ghulam kufunguwa njiya ya wahai na Manabii, akadai kuwa yeye ni nabii. Makadiani wakaliamini dai lake na wakalikubali kabisa. Tunanukuu hapa baadhi ya matamshi na maneno ya kuthibitisha upotofu na uzushi na mengineyo yawayo.

Kipengele kimoja cha msingi cha watu wanaodai kuwa ni Manabii ni kile cha kuwapachika ukafiri  wale wasiomuamini. Hivi ndivyo wasemavyo Makadiani katika hotuba zao za hadhara na katika machapisho yao dhidi ya Waislamu wanaopinga dai lao. Nanukuu yafuatayo kutoka katika hotuba zao:

Makadiani sio tu wanasema kuwa wao  wanapingana na Waislamu kwa kuamini ujumbe wa Mirza bali wanasema kuwa hakuna cha kuwanasibisha wao na Waislamu kwani Mungu wao, Uislamu wao, Qur’an yao, Sala yao na funga yao ni tofauti na Waislamu.

        -Hotuba ya Khalifa wa Kadiani iliyochapishwa katika Al-Fadl,

        Agosti 21, 1927 chini ya kichwa Advice for Students’

        kinawafafanulia wafuwasi wake tofauti kati ya Ahmadiya na

         wasio Ahmadia. Anasema “... Kwa kuwa Kristo aliyeahidiwa

         alisema kuwa. Uislamu wao, Mungu wao na hija yao ni

         tofauti na zetu, daima tunatofautiana nao kwa killa kitu.”

Mnamo Julai 30,1931 Al-Fadl likachapisha hotuba nyingine ya Khalifa wa Kadiani ambapo alielezea ugomvi uliotokea baina ya Makundu mawili. Moja likatowa hoja kuwa kwa vile tofauti kati ya Makadiani na Waislamu zinajulikana, na Kristo aliyeahidiwa amekwishazifafanuwa hakuna haja ya kuanzisha shule binafsi za kadiani: tunaweza kuyasoma yale mambo yote yasiyo na ubishani katika shule za Waislamu. Makundi mengine yakakataa. Huku bado wakibishana, Kristo mwenyewe aliyeahidiwa akaingia na kusikiliza mabishano yao. Kisha akatowa hukumu hii, akisema: “Ni makosa kusema kuwa tunatofautiana na Waislamu katika suala la kifo cha Yesu tu. Tunapingana nao katika yote; Mungu, Mtume (s.a.w), Qurian, sala, hija na zaka. Kwa kifupi aliwafafanulia kuwa tunatofautiana kabisa na Waislamu kwa mambo yote yanayohusiana na dini”.

Makadiani wenyewe ndio waliovunja mahusiano na Waislamu kwa lile pengo kubwa waliweka baina yao na Waislamu. Walijikusanya peke yao kana kwamba walikuwa ni jamii ndogo isiyo ya kiislamu kama inavyothibitishwa na maandiko yao wenyewe.

-         ENDELEA

Sio tu Makadiani walivunja mahusiano na mashirikiano na Waislamu kwa hotuba na maandiko yao, bali walifanya hivyo kwa vitendo kama mamia kwa maelfu ya waislamu walivyoripoti. Walijiundia jamii ya  peke yao wakikataa kusali au kuowana na Waislamu.

Ikiwa tatizo ndilo hilo, hakuna mantiki kwa Makadiani kubakiya kuwa sehemu ya jamii ya Waislamu. Si lazima kwamba uhuru wao utolewe kisheriya kwani jambo hilo limekuwepo kwa miyaka hamsini iliyopita

Kwa ule mwenendo wao, Makadiani wamethibitisha kile ambacho kilikuwa kigumu kuthibitika hapo kabla kuhusiyana na hikima na faida za kukoma kwa ujumbe wa Allah. Huko nyuma mtu alikuwa akijiuliza kwa nini wahayi na Mitume wamekoma kuja

Hivi leo, uzowefu umeonesha Hikima kubwa na faida za neema hii ya Allah. Imani kuwa Muhammad ndiye Mtume wa mwisho iliwaunganisha waumini wote katika kumfuwata Mtume mmoja tu, na hivyo imani hiyo ikawajengeya nguvu, umoja na mashirikiyano. Kuibuka kwa itikadi ya manabii wengi kunalimegamega Taifa katika makundi mengi ya kijamii.

Tukiwafukuza Makadiani hakuna mtu yeyote miyongoni mwetu atakayethubutu kusimama na kudai utume kutuvurugiya umoja na mshikamano wetu. Lakini kama tutaufumbiya macho Ukadiani, basi tutawasaidiya na kuwahamasisha wazushi wengi kuibuka na kudai hivyo, na hivyo tutakuwa tumeshiriki katika kuuhujumu mshikamano wetu.

Na tukiipuziya hatari hii, mfano wetu utaigwa na vizazi vyetu, na kwa hivyo hujuma hii haitakoma na jamii yetu itakabiliyana na hatari za aina nyingine kila siku; hatari hizo zitaligawa Taifa letu.

Hii ndiyo hoja yetu sahihi ambayo kwayo tunaegemeza madai yetu ya kuwafanya Makadiyani kuwa jamii ya watu wachache yenye haki  za jamii ndogo za Wasiowaislamu. Kwa hakika hoja yenye nguvu ni hii yetu na hakuna hoja nyingine yenye mashiko inayoweza kutolewa dhidi ya dai letu.

Wale wanaopinga dai letu wanataka kuwababaisha watu kwa vijisababu na vipingamizi visivyohusiyana kabisa na suwala hili. Mathalani eti wao wanasema kuwa makundi mbalimbali ya Waislamu bado yanashutumiyana kwa ukafiri. Na kama tutaendeleaya kulitenga kundi moja baada ya jingine Taifa litatoweka.

Aidha wanasema kuwa yapo madhehebu huru ya Kiislamu kama Ukadiani, ingawaje hayatofautiyani na Waislamu kiitikadi. Eti wanatuhoji iwapo hayo nayo tunakusudiya kuvunja mahusiyano nayo au tuamuwe tu kuwachukuliya Makadiani kama madhehebu hayo bila chuki na hasama.

Watu wengine wengi walihadaiwa na wito  wa Makadiyani wa kuingiya katika Uislamu. “Makadiani wanateteya  Uislamu dhidi ya mashambulizi ya Wakristo na Waaryan, na hivyo wanaueneza duniyani kote, ni vyema kuwachukuliya hivyo.”  Lakini sisi tutazungumziya kila nukta kati ya nukta hizi ili kujibu swali lolote linaloweza kujitokeza.

  1. Kweli inasikitisha kuwa makundi mbalimbali ya Waislamu yanashutuyana kwa ukafiri lakini si sahihi kulifanya hili kuwa kisingiziyo cha kuuhesabu Ukadiani kuwa ni dhehebu halali la Kiislamu; hii ni kwa sababu:

-         a) Hakuna mantiki kutowa mifano ya shutuma mbaya na kuhukumu kuwa kila shutuma isikubalike, na kwamba kumshutumu mtu yeyote kwa ukafiri si sahihi. Kwa kweli ni  makosa kuwashutumu watu kwa ukafiri kwa khitilafu ndogondogo kama ilivyo makosa kuukubali upotevu uliothibitika wazi wazi wa kutoka katika misingi ya Uislamu. Wale wanaofikiya hitimisho kutokana na shutuma zisizo za kweli dhidi ya wanazuwoni fulani kwamba aina zote za shutuma si sahihi wanaombwa kujibu iwapo Muislamu atabakiya kuwa muumini pale napodai yeye ni Mungu au Mtume, au iwapo anatoka katika mafundisho ya msingi ya Uislamu.

 -         b) Makundi na Madhehebu ya Kiislamu yanayotoleyana        shutuma ambazo zinatumika hapa yalifanya kongamano Mjini Karachi na yakakubaliyana juu ya kanuni za msingi za dola ya kiislamu. Yalikubaliyana juu ya kanuni hizo kwa sababu kila moja linaliona kundi au dhehebu jingine kuwa ni la Kiislamu. Hakuna hata moja lililoliyona jingine kuwa nje ya dini japo kulikuwa na tofauti ndogo ndogo miyongoni mwao. Hivyo kudhani kuwa kuutenga ukadiani kutoka katika Taifa la Kiislamu kutakuwa chanzo cha kuyatenga mengine mengi ni njozi tu.

-         C)  Shutuma ya jamii ya Kiislamu ya kuwashumu Makadiani kwa ukafiri si sawa na shutuma dhidi ya wengine. Makadiani, kwa uzushi, walidai kuwa kuna Mtume mpya ambaye anawahesabu wale wanaomuwamini yeye kuwa ni jamii tofauti na kuwaona Makafiri wale wasiomuwamini. Kwa hiyo Makadiani wote wanakubaliana kuwashutumu waislamu kwa kukufuru na Waislamu nao piya wamewahukumu Makadiani kuwa ni Makafiri.

Hivyobasi, inadhihirika wazi kuwa hii ni tofauti ya kimsingi ambayo haiwezi kuchukuliwa kuwa ni ndogo kama zilivyo tofauti ndogo ndogo- miongoni mwa mdhehebu ya Kiislamu.

  1. Bila shaka kuna madhehebu mengine ukiondowa Qadiani ambayo yamepinzana na Waislamu na kuvunja uhusiyano nao, na kujiundiya madhehebu zao peke yao, lakini kosa ambalo hawa wamelifanya ni tofauti kabisa na lile lililofanywa na Makadiyani kwa namna nyingi.

a)     Madhehebu haya yakajitenga kabisa na jamii ya Waislamu kiyasi kwamba yamekuwa kama  upukupuku njiyani ambao haudhuru wala haudhuriki. Kuwepo kwao kwaweza kustahamilika. Makadiyani huchanganyika na Waislamu, wakijidai kuamini mafundusho yao, wakiyajadili na wengine na kubishana kwa jina la Uislamu, na kwa kweli, huigawa jamii ya Waislamu na kuwateka upande wao. Mtafaruku mkubwa, mfarakano wa kufedhehesha na tawala kandamizi zimewasibu Waislamu  kutokana na Ukaragosi wa makadiani kwa nchi za kigeni. Kwa sababu hii na kwa sababu nyinginezo hatuwezi kuvumiliya kukaa na Watu hawa.

b)      Madhehebu ambayo yana tofauti na jamii ya Waislamu yanahukumiwa na sheria ya Kiislamu. Sheria inahukumu iwapo hizo imani zao binafsi zinawatowa nje ya dini. Na hata tukijaaliya kuwa wao si wafuwasi wa Uislamu , imani yao haitawatiya hatarini Waislamu na haitasababisha matatizo ya yoyote ya kijamii, kiuchumi na kisiyasa. Lakini uzushi wa Makadiyani unahatarisha imani ya mamiya kwa maelfu ya Waislamu na kusababisha tatizo la kijamii katika kila familiya ya kiislamu  inayoshawishika nao kiyasi kwamba mume humwacha mkewe, baba hutengana na mwana, na uwadui hutokeya baina ya ndugu. Zaidi ya hivyo madhehebu mengine yasiyokuwa Kadiani hayana malengo yoyote ya kisiyasa ambayo yangeweza kuonekana kama hatari kwa maisha yetu ya kijamii. Lakini makadiani wanazo nyendo fulani hatari za kisiyasa ambazo haziwezi kufumbiwa macho.

Makadiani walikuwa na uhakika kabisa kuwa katika jamii huru ya Kiislamu, huo utume unaodaiwa usingeliweza kushitadi  au kufikiya malengo yake. Wao wanajuwa kuwa jamii ya kiislamu inachukizwa na madai kama hayo kwani yanawaparaganyisha Waislamu, yanavunja sheriya ya kiislamu na yanaimegamega jamii ya Waislamu.

Huku wakifahamu msimamo wa Maswahaba wa Mtume katika kuwakabili wazushi wa Utume , na huku wakiutambuwa ukweli kuwa pale Waislamu wanaposhika madaraka katika nchi yoyote katu hawaruhusu madai ya uzushi, Makadiani wakaamuwa kujinasibisha na serikali ya kikafiri kwa sababu  hakuna mazingira mengine wanamoweza kuuhujumu Uislamu kwa uzushi.

Wameiteka Jamii ya Waislamu kwa vile wanawaita katika mafundisho yao kwa jina la Uislamu. Wanajuwa vizuri sana kuwa ni kwa maslahi yao wanaunga mkono utawala wa wageni kwani unawakaba Waislamu na kuwasaidiya wao kupata maslahi yao na kuuhujumu Uislamu. Taifa huru la Kiislamu kwao wao ni adui na halina faida, ni Taifa ambalo wao hawalipendi kabisa.

Twaweza kunukuu maandiko mengi ya Mirza {Madai ya Ahmad na mengine kutoka katika maazimio ya wafuwasi wake} lakini yatosha kunukuu baadhi tu bila sherehe.

Maelezo ya hapo juu yanauthibitisha  waziwazi ule ukweli  kuwa genge hili la wazushi linafahamu maslahi ya utawala wa makafiri katika nchi za Waislamu, chini ya hifadhi ya wavamizi hao ndio wao huweza kufikiya malengo yao.

 Kama Waislamu watashika madaraka, basi wazushi hawa watasambaratishwa kwa sababu Waislamu walio huru hawatavumiliya kukaa na  wale wanaohujumu dini yao na kuiparaganyisha jamii yao.

Hatari zaidi ni nyendo za Makadiani za kutaka kuanzisha taifa lao huru nchini Pakistan. Mwaka mmoja baada ya kuibuka kwa Pakistan, Khalifa wa Makadiani alitowa hotuba mjini Ku’ta mnamo Julai 23, 1948, iliyochapishwa katika Al Fadl mnamo Agosti 13, 1948. Alisema, “British Plukhistan inatolewa kwenu. (hivi sasa ni sehemu ya Pakistani Plukhistan).

Idadi ya wakaazi wake ni laki tano au sita japo ina idadi ndogo ya watu kuliko wilaya nyingine, ina umhimu mkubwa. Kwa vile watu ni muhimu katika ulimwengu wetu, wilaya hii ni muhimu kama vile sehemu nyingine yoyote ya Pakistan. Mfano kutoka katika katiba ya Marekani utathibitisha umuhimu wake. 

Kila nchi ina idadi sawa ya wawakilishi bila kujali ukubwa au wingi wa watu wake. Hivyo kama tutaiongeza British Plukhistan katika wilaya ya Blukhistan, wakazi wake watafikiya miliyoni moja. Nadhani mnatambuwa ugumu wa kuwabadili dini watu  wa wilaya hiyo kubwa.

Lakini ninyi hamuwoni kuwa tunaweza kuwabadili watu wa wilaya hiyo ndogo? Tukitiliya maanani basi tutapeperusha bendera za Ahmadiya katika wilaya yote hiyo. Itikadi yetu haitafaulu mpaka mizizi yake ijikite chini ya ardhi.

 Hivyo, fanyeni kazi na enezeni mafundisho yenu na fanyeni yakite mizizi barabara. Kwanza Ijengeni itikadi  mahali hapo na tukifanikiwa kuwabadili watu tutajivuniya wilaya hiyo. Kuwabadili watu siyo jambo jepesi”.

Baada ya kuzungumziya yote haya nataka kuwauliza wale wanaotaka tuvumiliye kukaa na Makadiani na tuvumiliye matendo yao na wanaong’ang’aniya kisingiziyo kuwa  kuna madhehebu mengi katika Uislamu, nauliza kama yana nyendo na sera za hatari kama hizo za Makadiani?

Je lipo dhehebu linalouona Uislamu ni hatari, na linalouona mfumo usio wa Kiislamu kuwa ndio wenye maslahi? Je lipo dhehebu litakaloukataa Uislamu na kuwa tayari kuanzisha dola huru ndani ya nchi ya Kiislamu?

Yumkini hakuna dhehebu lolote lenye mwenendo huo wa Qadiani na hivyo tunauliza kwa nini wanatutaka tuuchukulie Ukadiani kama madhehebu hayo mengine?

Dhehebu hili dogo linakabiliwa na tatizo jingine; Lenyewe linadai uhuru kutoka kwetu. Je hii haiswihi kuwafukuza nje ya jamii?

Imesemwa kuwa shida humlazimu mtu kuhitaji kitu chochote kile. Ukweli wa hitajio lake hutegemeana na ukali wa shida yake. Kuwemo kwa Makadiani miongoni mwa jamii kubwa ya Waislamu kwaleta madhara makubwa kwa Waislamu.

 Kwa ajili hii jamii ya waliowengi inadai kutengwa kisheriya kwa jamii hii ndogo yenye madhara. Makadiani, kwa matendo yao, wanajitenga na jamii ya waislamu na wanatumiya uhuru wa kujitenga kuanzisha dhehebu lao na kuhujumu misingi ya Uislamu kwa mbinu zilizokwishapangwa kwa hila.

 Aidha wanajificha nyuma ya Uislamu na kumwaga mbegu za mgawanyiko na mifarakano miongoni mwa Waislamu. Kwa njiya ya ujanja ujanja ya kujidai Waislamu, wanapata nyadhifa zaidi za utawala na ajira.

 Hii inaleta madhara katika jamii na hivyo basi, ni kisingiziyo gani tena kilichobaki kwa mtu kuiachiya jamii ya wachache iiletee madhila jamii ya wengi au kulikataa dai letu la kuwatenga Makadiani na jamii ya Waislamu kisheriya.

Jamii ya walio wengi haikubuni sababu ya kutengana na jamii ya wachache bali jamii ya wachache ndiyo iliyofanya hivyo pale walipojianzishiya jamii zao peke yao na kuvunja mahusiano ya kijamii na kidini na Waislamu. Kukataa huku kutengwa na Waislamu kisheriya kwafanya Makadiyani wawajibike wenyewe kwa ubishi wao.

Allah amekujaaliyeni, wasomaji, akili na upeo wa kuelewa hivyo, angaliyeni jinsi wanavyokataa matokeo ya vitendo vyao. Ikiwa wao wanataka kudanganya, kuhujumu na kuvuruga umoja wa Waislamu kwa nini nyinyi mkiwa wawakilishi wa jamii kubwa mnaiacha jamii ya wengi ihujumike kwa ujanja wa wadanganyifu wachache.

Sasa tulishughulikie suwala la mwisho ambalo linadai kuwa, kwa vile Makadiani wanateteya Uislamu na kuusambaza, si sahihi kuwachukuliya kama tunavyowachukuliya sisi.

Kwa kweli hii ni hoja isiyo na msingi ambayo imewahadaa baadhi wasomi wapya. Tunawaomba wayasome na kuyatafakari haya tutakayoyanukuu kutoka katika maandiko ya Mirza Ghulam Ahmad mwenyewe ambayo yatafichuwa malengo ya wazushi hawa katika kuteteya Uislamu.

Anasema “Nimekuwa nikichapisha vitabu kwa Kiingereza, Kiarabu, Kipesia na Kiudu, kutokana na mapenzi yangu mwenyewe ili kuwapa imani Waislamu kuwa jukumu lao ni kuwa waaminifu kwa Serikali ya Waingereza kwamba waachane na dhana ya jihadi takatifu na waache kumsubiri Mahdi mmwaga damu na waachane na njozi nyingine zote za kipuuzi ambazo haziwezi kuthibitishwa na Qur’an. Ikiwa bado wanafuwata makosa haya, basi, angalau, wasikanushe neema za serikali hii karimu au watakuwa waovu kwa kukosa utii kwa sheriya za Allah” (Tiryaq Al Quloub 28 Oct 1902 pp.307)

-Katika waraka huu huu kwa serikali ya Muingereza kaandika hivi: “Ni wakati muwafaka niiambiye kwa fahari serikali yangu yenye hisani kuwa huu ni utumishi wangu wa miaka 20 kwenu. Hakuna familiya ya Kiislamu katika British India anayeweza kufanya nilivyofanya mimi. Ni dhahiri kabisa kuwa jitihada endelevu ya miyaka 20 ya kuwashawishi watu kwa mafundisho yaliyotajwa juu haiwezekani iwe kazi ya Mnafiki. Ni kazi ya mtu aliye na imani na ukweli kwa serikali hii. Nakiri kuwa huwa najadiliyana mambo ya dini na Makasisi lakini kwa niya y dhati. Nimechapisha hoja nyingi kuhusu Ukristo, lakini piya nakiri kuwa pale baadhi ya wamishenari walipoandika vibaya dhidi ya Uislamu kama vile lugha isiyo ya kiungwana ya hoja ya kifedhuli katika Nur Afshan ambamo mmeshenari amemshutumu Mtume wetu kwa wizi, tamaa, uzinzi na binti yake, uwongo na umwagaji damu, mimi nilihofiya maandiko haya yasije yakawakasirisha Waislanu ambao ni wepesi kughadhibika. Kwa hiyo, nikaona ni vema niandike dhidi ya vitabu hivi ili kuzima moto wa ghadhabu za Waislamu na kupunguza chuki ya jamii nzima na kuzima hasira ya watu  wanaoweza kuhamaki na kuleta fujo ambazo hutishia usalama wa Taifa. Ni wazi kuwa mimi niliandika tu dhidi ya vitabu hivi vya kashfa kwani niliona kuwa kuwandika ndio ilikuwa njiya pekee ya kuzima mwale wa hasira miongoni mwa Mashabiki wa Uislamu” (pp. 308-309). Kisha anaendeleya kusema; “Niliyoyaandika dhidi ya Wamishenari yalitokana na utashi wa kuwadhibiti Waislamu kwa hikima na kuwafurahisha na kuzima hisiya zao mbaya za uwasi. Natamka mimi ni Muislamu mwaminifu mno na msaidizi mno kwa serikali ya Muingereza. Kuna sababu tatu zilizonifikisha mimi katika utii huu wa kiwango cha juu kabisa kwa Muingereza; kwanza ni ushawishi wa baba yangu, pili neema kubwa za serikali hii, wahai wa Allah” (pp. 309-310)

-Akaandika hivyo hivyo katika nyongeza ya kitabu chake Shahadatu’l Qur’an  iliyobeba kichwa, ombi linalostahili upendeleo wa serikali, “Dini yangu ninayoitangaza tena na tena ni kwamba Uislamu unagawanyika katika sehemu mbili. Ya kwanza ni kumtii Allah, ya pili ni kuitii serikali ambayo inalinda usalama wa Taifa, inatupa hifadhi, na kutukinga na madhalimu. Serikali hii ambayo sote tunapaswa kuitii ni serikali ya Muingereza.”

Piya katika juzuu ya VII ya Conveying The Message, tunakuta waraka kwa Bwana mkubwa Mtawala wa wilaya ambapo alimuhakikishia Mtawala utii wa familiya yake kwa serikali ya Waingereza. Aliripoti baruwa ambazo Mirza Ghulam Murat Khan alikuwa amezipokeya kutoka kwa Mtawala wa Lahore na mshauri wa masuwala ya fedha wa Punjab pamoja na watawala wengine wa kiingereza ambao walishuhudiya utumishi wake mkubwa ambao unaashiriya ukweli wake, uaminifu wake, utii wake, na mapenzi yake kwa Waingereza, na ikawaorodhesha wanafamiliya muhimu wa familiya yake waliotumikiya Waingereza. Kisha akasema “Kazi muhimu ambayo kwayo mimi nilijitoleya na bado najitoleya kuifanya ni kuzigeuza nyoyo za Waislamu kutoka katika Uislamu kuelekeya katika ukweli, upendo, utii na fadhila za dhati kwa serikali ya Waingereza, na kuondokana na dhana mbovu kama vile vita vitakatifu na imani nyingine za kipumbavu ambazo zinaharibu mahusiano mema na Waingereza. (pp10 

-Sikushugulika tu na kuzijaza nyoyo za Waislamu wa India utii wa dhati kwa Waingereza bali piya nilandika vitabu vingi kwa Kiarabu, kipersia na Kiudu ambamo niliwafafanuliya wananchi wa nchi za Kiislamu jinsi sisi tanavyopitisha masiku ya uhai wetu kwa usalama, furaha, fanaka na uhuru chini ya hifadhi ya Serikali ya   Waingereza (pp. 10). Kisha akatowa orodha ndefu ya vitabu vyake vinavyothibitisha mapenzi yake ya dhati na utii wake mkubwa kwa Waingereza.

-Kisha akaandika “Serikali ithibitishe kama yale maelfu ya Waislamu wanaoniita mimi kafiri, wanaonilaani mimi na wafuwasi wangu, na wanatudhuru eti kwa sababu mimi niliandika maelfu ya matamko ambayo yalijaa shukurani zangu kwa serikali, zilizototelewa nami kwa  busara yangu, moyo wangu na kwa imani yangu yote na kuzichapisha katika nchi zote za Kiarabu. Je mambo haya hayako dhahiri? Mimi nasema kuwa dhehebu langu lina utii wa kiwango cha juu kabisa kwa serikali ya Waingereza na kwamba ni dhehebu la kiislamu lenye ukweli, uwanifu na utii mkubwa kabisa kwa sababu linatangaza uatayarifu wake wa kujitolea kila kitu kwa ajili ya Waingereza. Kanuni za Waingereza hazituweki sisi hatarini kwa namna yoyote ile. Kisha akaandika “Mimi nina hakika kuwa muda wa kuwa wafuwasi wangu wanaongezeka, basi wale wenye itakadi ya vita vitakatifu dhidi ya Utawala wa wavamizi wanapunguwa. Kuniamini mimi ni kukataa kuwepo kwa vita vitakatifu.” (pp.17)

Bila kujali kama lugha hiyo na maneno hayo yanaswihi kutamkwa na Mtume, sisi tunataka kuvuta hisiya za msomaji azingatie ukweli kuwa haya ndiyo malengo ya mwasisi wa dini hii na haya ndiyo malengo ambayo kwayo alijituma, aliteteya Uislamu na kusambaza mafundisho yake.

Je hii ndiyo kazi yenyewe ya kuutumikiya ‘Uislamu’ inayojuzu kupewa shukurani na heshima pamoja na kuwa tumeona uchochezi na malengo yake? Na kama bado tu ni vigumu kwa baadhi ya watu kuuona ukweli wa kazi hii ya kuutumikiya Uislamu, tunawaomba watafakari haya tunayoyanukuu kutoka katika maneno ya Makadiani wenyewe.

-         “Sisi  tulikipata kitabu cha Muhandisi wa Kiitaliano ambaye alishika nafasi muhimu nchini Afghanistan. Kitabu hicho kwanza kilichapishwa kibahati tu na ndipo hapo sisi tulipopata nakala yake. Katika kitabu hiki mwandishi anasema kuwa Sahib Zadeh Abdullatif ambaye ni Kadiani, aliuwawa nchini Afghanistan kwa sababu alikuwa akiwashawishi watu waachane na vita ‘vitakatifu’. Serikali ikacheleya  wito huu usije kufifiliza hamasa ya kupiganiya uhuru katika nyoyo za Waafghani na hivyo kuwafanya wawe watumwa wa Waingereza. Tunahitimisha kutokana na ukweli huu kuwa utawala wa Afghanistan haukumuuwa Kadiani huyo ila kwa sababu aliwataka watu kuachana na ‘vita vitakatifu’ ( Mirza Bashir’s speech on a Friday Al-Fadl 6 Aug 1935).

-Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan alitowa tangazo lifuwatalo. “Baada ya Mulla Abdulhalim Jihar Asiyanis na Mulla Nur Ali Hanuti kuwa makadiani, wakaanza kufundisha itakadi zao za uzushi kwa jina la ijitihadi.... Baada ya muda fulani wakakamatwa kwa kosa jingine na kushitakiwa. Baruwa kutoka kwa watu fulani wa nje zilikamatwa ambazo zilithibitisha ukaragosi na njama zao dhidi ya maslahi ya Afghanistan. Baruwa hizo zinafichuwa wazi wazi kabisa jinsi watu hao walivyokuwa wamepiga hatuwa kubwa ya kujiuza kwa maadui wa Afghanistan” (Al-Fadl, 3 Mar 1925).

-         “Ingawaje nilikwenda Russia kuwalingania watu waingie katika Ukadiani,mara zote nilifanya hivyo na kuitumikia serikali ya Uingereza kwa wakati mmoja kwa sababu maslahi yetu na maslahi ya serikali ya Waingereza yanawiyana kabisa” (Mohammad Amin, a Qadiani preacher in his essay published in Al-Fadl 28 Sep 1922).

-          Dunia inatudhania sisi ni vibaraka wa Qadiani. Pale Waziri wa Ujerumani aliposhiriki katika ufunguzi wa Kituo cha Ahmadia nchini Ujerumani, serikali yake ikamlaumu  na kumuuliza ‘Kwa nini umeshiriki katika hafla inayowahusu watu ambao ni vibaraka wa Waingereza?’  ( A speech by Qadiani’s Caliph Nov 1934)

-         “ Twatumai kuwa, kwa kupanuka kwa utawala wa Waingereza,  nafasi za kupata wafuwasi  wapya wengi kutoka kwa Waislamu na wasioWaislamu nazo zitaongezeka” (Opinions concerning Lord Harding’s tour in Iraq published in Al-fadl, 11 Feb 1910

-         “ Serikali ya Waingereza ni kama pepo kwetu. Ahmadia wanapeta chini ya hifadhi ya pepo hii. Mkiiacha nyinyi wenyewe mtaona mvuwa ya kutisha ya mishale ya sumu itakayowashukieni juu ya vichwa vyenu. Sasa kwa nini basi hamshukuru neema za serikali hii ilihali nyote mwajuwa namna maslahi yake yanavyofungamana na yetu na namna mafanikio yake yanavyogusa maslahi yetu. Popote serikali hii inapotwaa nchi mpya na kuiweka katika himaya yake, na sisi tunapata uwanja mpya kwa ajili ya itikadi zetu” (Al-Fadl 19 oct 1915).

-         “Mahusiyano baina Kadiani na serikali ya Muingereza ni tofauti na wengine wotewale; hiyo ni kwa sababu maslahi yetu yanahitaji jambo hili. Ni faida zilioje  ambazo serikali ya Mwingereza inatuongezea, na kadri utawala wa Muingereza unavyotuongezeya nafasi ndivyo ustawi unavyozidi kuongozeka. Endapo itahujumiwa-Mungu aepushie mbali- sisi hatutaweza kuishi salama. (Qadianis caliph’s declaration Al-Fadl 27 Jul 1918)

Hivyo basi, tumefafanuwa ukweli halisi juu ya Ukadiani, kuziweka wazi itikadi, nyendo na matendo. Na sasa tutafafanuwa namna lilivyoibuka dhehebu hili

1.      Nusu karne ilipita ambapo Waislamu bado walikuwa na maisha mabaya chini ya utawala wa Waingereza. Kisha ghafla mtu mmoja akadai kuwa yeye ni Mtume. Akadai kuwa ilikuwa haitoshi kwa Waislamu kumuwamini Muhammad (s.a.w) bali kama walitaka kuwa na imani ya kweli na Uislamu sahihi,basi wamuamini yeye piya. Wale wasiomuamini yeye wametoka nje ya wigo wa Uislamu Hivyo mzushi akazuka miongoni mwa jamii iliyoungana kudai eti yeye ni mtume.

2.      Kwa mujibu wa uzushi wake, Mtu huyu alianzisha Jumuiya yake mpya na jamii huru iliyopingana na Waislamu kama walivyokuwa Wahindu na Wakristo. Na wakatofautiana na imani, tabia, matarajio na mateso ya Waislamu.

3.      Mwasisi wa Jumuiya hii mpya, tangiya mwanzo kabisa wa uzushi wake, aliona kuwa Jamii ya Waislamu isingeweza kustahamili kuhujumiwa, hivyo yeye na genge lake wakaamuwa kuwa watumishi watiifu, wakweli na wenye upendo kwa utawala wa Waingereza. Hii haikuwa sera ya maisha tu, bali piya walitambuwa ukweli  kuwa maslahi yake yalikwenda sambamba na ushindi wa Waingereza siyo tu nchini India bali piya katika nchi nyingine za Waislamu ili kueneza sumu na uzushi wake.

4.      Dhehebu hili kwa hila yake na Waingereza lilivuruga jitihada zote za Waislamu katika kipindi cha miyaka hamsini iliyopita ili kujitenga na jamii ya Waislamu. Serikali ikaendelea kung’ang’aniya kuwa dhehebu hili lichukuliwe kama sehemu ya Waislamu licha ya tofauti zake. Waislamu waliathirika mno na hatuwa hizi huku Makadiani wakipata manufaa makubwa.

 Licha ya jitihada zote za Wanazuoni, bado serikali ikaendeleya kuwatiya imani Waislamu kuwa Makadiani ni moja ya makundi ya Waislamu ili kuwaachiya Makadiani waeneze mafundisho yao miongoni mwa Waislamu.

Muislamu hataepuka kufuwata ukadiani iwapo kundi hilo linahesabiwa kisheriya kuwa ni dhehebu la kiislamu. Jambo hili linawanufaisha, kwa kiasi kikubwa, Makadiani kwani wanaongeza idadi na nguvu yao. Waislamu wanaathirika kwani jamii  hii mpya inayopingana nao ilikuwa inachipuka kama kansa mwilini mwao.

Tatizo la ukadiani likajitokeza mjini Punjab; likaisibu na kuiharibu hivyo lilikuwa ni jambo la kimaumbile kuwa Waislamu waliokuwa na ghadhabu zaidi dhidi ya Makadiani ni wale wa Punjab.

Dhehebu hili likapata bahashishi zote za serikali ya Waingereza ambapo lilipata nyadhifa nyingi jeshini, Polisi, katika vyombo vya sheriya na Utawala katika nchi.

Ni ajabu kuwa dhehebu hili lilipata nyadhifa zote hizi zilizotengwa kwa waislamu kwa sababu serikali ililihesabu kuwa ni moja ya madhehebu ya Kiislamu na inaendelea kuwatiya imani waislamu kuwa nyadhifa hizi zinatolewa kwao tu. Waislamu wanatendewa hivyo hivyo katika uchumi, biashara, viwanda na kilimo 

Maududi piya ameandika kitabu; Finality of Prophethood (Mwisho wa Utume)