Bismillah Al-Rehman Al-Raheem
AlFatwa International 28 (Swahili)
Mwisho
wa utume
Uongo mwingine wa Qadiani wafichuka!
Na Dr. Sayyid
Rashid Ali
Utangulizi
Ndugu wasomaji
Assalam alaykum
Waislamu, tangu
wakati wa Mtume Muhammad(s.a.w) hadi hii
leo wanaamini pasi na tone la shaka kuwa hitimisho la utume ni Muhammad(s.a.w),
na kuwa Qur'an ndio mwisho wa ujumbe wa
Allah ulioletwa kuwaongoza Wanaadamu mpaka siku ya Kiyama.
Dhana ya mwisho wa ujumbe
na utume ni tofali muhimu sana katika jengo zima la Uislamu, inayobeba nafasi
muhimu sana katika maisha binafsi ya Muislamu na yale ya jamii kwa ujumla,
inayojenga mahusiano ya kidugu yanayovuka mipaka ya kijiografia, rangi na mila.
Udugu huu wa kiulimwengu unaojengwa na Uislamu
unaufanya umma wote kuwa mmoja
Hiki ndicho kikwazo na
pigo kubwa kwa maadui wa Uislamu ambao wamekuwa wakijaribu kila wawezavyo
kuharibu jengo hilo la umoja na udugu
tangu wakati wa Mtume(s.a.w) hadi hivi leo. Maadui wa Uislamu katika
zama hizi, wamekuwa wakijaribu kuwagawa Waislamu kwa kutumia mbinu kuu ya
kupotosha mafundisho ya Qur'an na kuchapisha maandiko yanayochafua
shakhsia ya Mtume(s.a.w).
Akizungumzia
"Popote maadui wa Uislamu
walipopanga kushambulia mizizi ya Uislamu, walijaribu kuhoji uthabiti wa Qur'an
na kuchafua shakhsia ya Mtume (s.a.w). Tunapigwa vita hivyo
kutoka nje. Tatizo hasa linalojitokeza hata hivyo ni
pale miongoni mwetu wanapoasi
Imani ya Waislamu
Imani ya
Waislamu juu ya Mwisho utume imewekwa wazi katika Qur'an. Hapa tunanukuu aya moja inayobainisha
Hakuwa Muhammad baba wa yeyote kati ya wanaume wenu. Lakini yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume. Na mwenyezi
Mungu ni mjuzi wa kila kitu(33:40).
Kanuni ya msingi katika
kutafsiri aya za Qur'an ni kutafsiri kwa kutumia aya kwa aya au kutafsiri kwa
kutumia mafundisho ya Mtume(s.a.w) na mwisho kutumia
kauli za masahaba wake.
Katika aya tuliyoinukuu
hapo juu neno Khatam limefasiriwa
Khutba ya Mwisho
Katika Khutba ya Miwisho
aliyoitoa kwenye uwanja wa Arafa wakati wa Hija yake ya mwisho, Mtume(s.a.w) alisema.
"Enyi
watu! Hapana Mtume atakayeinuliwa
baada yangu na hapatakuwa na umma mpya baada ya huu wenu(Taz.
Seerat Ibn Hisham, khutba ya mwisho).
Katika vitabu vya
Hadithi
Vitabu mbali mbali
vimenukuu Hadithi za Mtume(s.a.w) zinazosisitiza kuwa
yeye ndiye Mwisho wa Utume. Hapa tungependa kunukuu Hadithi Sahihi iliyotumia
neno Khatam:
"Kutatokea
wadanganyifu thalathini katika uma wangu, kila mmoja miongoni mwao atadai kuwa
yeye ni Mtume, lakini jueni kuwa MIMI ndiye Khatama Nabiyyiin,
hapatakuwa na Mtume baada yangu.(Sunan Abu
Daud, Kitab al Fitan).
Mtume(s.a.w) katika Hadithi hii ametumia neno Khatam un
Nabiyyin kwa kujinasibu nalo yeye Mwenyewe na akatilia mkazo kwa kuongeza
kuwa "Hapana Mtume baada yangu". Ni wazi Mtume alijua kuwa
kutatokea wenye akili twevu katika watu wa umma wake
watakaojaribu kutafsiri vibaya neno
Udanganyifu Nambari 1 wa Kadian- Madai ya Utume
Baada ya kueleza imani ya
Waislamu juu Mwisho wa Utume, sasa hebu tuone imani ya
makadiani juu ya Khataman un Nabiyyin, mwisho wa Utume?
Unapozungumza na Kadiani yeyote yule atadai kuwa yeye naye anaamini kuwa
Mtume Muhammad ndiye mwisho wa Mitume. Hata hivyo unafiki wake hufichuka pale
tu utakapomuuliza anamaanisha nini anapotamka neno Khaataman Nabiyyin. Baada ya
hapo udanganyifu wake hudhihirika kwa sababu ana ueleo
wake binafsi wa neno hili
. Ni Muhuri wa Manabii lakini si Muhuri umaanishao
mwisho wa Utume(
. Mmbora wa Mitume.
Katika kuthibitisha dai lao hutoa maelezo marefu kushikilia msimamo wa kijinga
usio na mantiki. Suala hili linatukumbusha jinsi kazi ya Mirza ilivyo na undumakuwili; sehemu ikidai kuunga mkono mafundisho ya
jumla ya Uislamu ikionesha pia maana ya Khatam kuwa ni mwisho na sehemu
nyengine ikikana na kubadilisha maana ya Muhuri wa Mitume kuwa ni idhinisho la
utume. Mirza kwa dhahiri yake ametumbukiza dhana za
kishetani katika mfundisho yake aliyodai kuwa ni Uislamu. Katika sehemu kadhaa
za mafundisho yake amedai kuwa hapana Mtume baada ya Muhammad, alifanya hivyo
Mirza ametumia janja hii ili kwa sura ya nje ionekane kuwa Ahmadiya wanaamini sawa na
Waislamu wengine lakini kwa ndani apotoshe mafundisho haya kwa kutumbukiza
dhana zake za kishetani. Makadian wanadai kuwa Mirza hakutaja kuwa yeye ni Mtume, wanatoa nukuu za maandiko kuthibitisha
Nukuu zinazoonesha
kukana kwa Mirza kuwa yeye si Mtume
"Je anaweza akawepo
mzushi atakayedai kuwa yeye ni Mtume na mjumbe wa Mwenyezi Mungu akiiamini
Qur'an, na mtu huyo akadai kuamini Qur'an na
aya isemayo "Walakin Rasuulallah Wakhaataman Nabiyyin" kuwa ni
neno la Mwenyezi Mungu, bado akaamini vile vile kuwa mimi nami ni Mtume na
mjumbe wa Allah baada ya Mtume mtukufu(s.a.w)?(Anjam Atham, Roohani Khazain
Juzuu 11 uk. 27)
"Nafahamu kwamba
chochote kinachopingana na Qur'an ni cha uongo, rida(kuritadi) na kisicho na
ithibati, hivyo ni kwa vipi mimi nidai utume hali ya kuwa ni Muislamu?"(Hamamatul Bushra, Roohan Khazain juzuu ya 7 uk. 297).
"Enyi watu msiwe maadui wa Qur'an na baada ya Khaataman Nabiyyin msianzishe mfumo
mpya wa ufunuo wa kitume. Mumuonee haya Allah kwa yeyote yule
atakayekutokezeeni".(Asmani Faisla, Roohan
Khazain juzuu ya 4 uk. 335).
Licha ya maelezo hayo,
Mirza kwa upande mwingine alifuma mantiki ya
upotoshaji kuhalalisha madai yake ya Utume.
"Mwenyezi Mungu
alihisi kwamba katika zama hizi kutafika wakati atakaohitajika Mujadid mkubwa
kwa hiyo muhuri(idhinisho) la Mungu litafanya kazi ya
kuwaidhinisha wafuasi wa Mtume wafikie daraja itakayowafanya wakati fulani
waonekane ni umati wake na wakati mwingine waonekane ni Mitume, kwa sababu
Mwenyezi Mungu amemfanya Mtume(s.a.w) kuwa shahidi wa Muhuri ya kwamba amempiga
chapa ya Muhuri ili kumfanya awe mkamilifu zaidi..."(Haqiqatul Wahi,
Roohan Khazain juzuu ya 22 uk. 99-100).
"Maana ya Khataman
Nabiyyin ni hii kwamba bila muhuri wake hapana utume
wa yeyote unaoweza kuthibitishwa. Ni kwa kugongwa Muhuri tu
ndipo usahihi na uthabiti wa karatasi unapoonekana."(Malfoozat e-
Ahmadiyya juzuu ya 5 uk. 290).
Kimahubiri, kwa maneno
mengine Khaataman Nabiyyin kwa Mtume(s.a.w) inaashiria daraja kubwa na ni kwa
maana hii yeye amekuwa Muhuri wa Mitume, ikiwa na maana kwamba baada yake
watazaliwa mitume ambao sharti lao ni kumfuata yeye."(Barua
ya Mian Mahamood, Khalifa wa Qadian, AlFazl Qadian ya tarehe 29 Aprili 1927).
Kwa hakika mpinzani wetu Moulvi
Sahebaan amefanya makosa makubwa katika kuelewa maana ya Khatamn Nabiyyin, Yeye(Muhammad (s.a.w) ni Khataman Nabiyyin kwa maana kwamba
amefanywa kuwa Muhuri wa idhinisho kwa Mitume."(ALFazl
Qadian tarehe 8 Desemba 1915).
"Hatupingi kwamba Mtume(s.a.w) ni Khaataman Nabiyyin lakini maana ya Khatam si
ile wanayoilewa Waislmu wengi ambayo inapinga utukufu wa Mtume Muhammad(s.a.w)
kwamba ameunyima fursa umma wake ya
utukufu wa Utume.(AlFazl Qadian tarehe 22 August 1939).
"Hapana yeyote katika
Ulimwengu anayeweza ukweli halisi wa Khaataman Nubuwway wa Muhammad ila yule
ambaye ni Khatam ul Awliya kama Hazrat Khataman Anbiyya, kwa sababu kuelewa
ukweli halisi wa kitu kunategemea kustahiki kwa mtu katika kitu hicho na ni
ukweli uliothibitika ni kwamba mtu anayestahiki Khatimiya ni ama Mtume(s.a.w)
au Hazrat Masihi Mowood(Mirza Saheb."( Taz.Jarida
la Qadian Tasheed ul Azhan, Na. 8, juzuu ya 12, uk.201 chini ya mada iliyopewa
kichwa "Ukweli halisi wa Khatmi Nubuwat wa Muhammad, la mwezi Agosti
1917).
Udanganyifu nambari 2 wa Kadian- Maana ya Khatam:
Makadiani wamekuwa wakitoa
vijisababu vingi kuhalalisha maana
1. Khaatama ush-Shu'Araa(Muhuri wa Washairi) ambayo imetumika kwa mshairi
Abu Tammam. (Taz. Wafiyatul A'yan, juzuu. 1,
2. Khataman ush Shuaraa
vile vile limetumika kwa Abul Tayyeb. (Muqaddama Deewanul Mutanabbi Misri uk. 4).
3. Khataman ush Shuaraa
vile vile limetumika kwa Abul A'la Alme'ry(tazama
rejea hiyo hiyo, uk.4 katika footnote(tanbihi)
4. Khataman ush Shuaraa
limetumika kwa Sheikh Ali Huzain wa
5. Khataman ush Shuaraa
limetumika kwa Habeeb Shiraza wa
6. Khatam ul Auliya-(Muhuri
wa watakatifu) limetumika kwa Hazrat Ali(r.a). (Taz. Tafsir Safi, sura ya AlAhzab) je yupo hivi leo yeyote yule anayeweza kufikia Wilaayat iwapo maana ya
Khatam ni mwisho?
7. Khatama Al Auliyaa- limetumika kwa Imamu
Shafii. (Taz.
8. Khataman Auliyaa-
limetumika kwa Sheikh Ibnul 'Aarbee.(Fotohat Makiyya).
9. Khatam Al Karaam
10. Khataman Al Ilmu Al
Aimmah(Muhuri
wa viongozi wa dini) limetumika kwa Imam Muhammad Abdah wa Misri.(Tafseer
Alfatehah, uk.148) je leo hatuna viongozi?
11. Khatam Atul Mujahediin(Muhuri
wa Mujahidiin) limetumika kwa AlSayyad Ahmad Sanosi. Akhbar AlJamiatul
Islamiyya, Palestina, 27 Muharram, 1352)
12. Khatama Al Muhaqqiqiin(Muhuri
wa wasomi watafiti) limetumika kwa Ahmad Bin Idrees. (Al'Aqadum Nafees)
13. Khatam tul Ulamaa
Al Muhaqqdiqiin(Muhuri
wa Watafiti0 limetumika kwa Abul Fazl Aloosi.
14. Khatama Al
Muhaqqiqiin limetumika kwa Shaikh Al Azhar Saleem
Al Bashree. (Al Haraab, uk. 372)
15. Khaatam tul
Muhaqqiqiin limetumika kwa Sheikh Imam Suyuut.
16. Khaataman al Muhaddithiin(muhuri
wa wapokezi) limetumika Shah Waliyyullah wa
17. Khamatamal Huffaz (muhuri
wa Mahaafidh). Limetumika kwa
Sheikh Shamsuddin
18. Khataman Al Aulia(muhuri wa
Watakatifu) limetumika kwa Mtakatifu wa juu. (Tazkiratul Auliyaa, p Ghaib422.
19. Khatama Al Aulia
limetumika kwa Watakatifu waliopiga hatua za
mafanikio. (Fatoohul Ghaib, p43)
20. Khatama Atul Fuqaaha(Muhuri
wa Majaji) limetumika kwa Al Sheikh Najeet.(Akbaar Siraat al Mustaqeem Yaafaa,
27 Rajab, 1354 A.H).
21. Khatama al
Mufassireen (Muhuri wa wa Wafasiri) limetumika kwa
Shaikh Rasheed Raza. (Al Jaameemiatul Islamia, 9 Jamadiy Thaan, 1354 A.H)
22. Khatama atul Fuqaha
limetumika kwa Shaikh Abdul Haque.(Tafsirul Akleel)
23. Khatama Al. Muhaqqeen(Muhuri
wa Watafiti limetumika kwa Ashaikh Muhammad Najeet, (Al Islam Asr Shi'baan 1354
A.H).
24. Khataman Al Wilaaya(Muhuri
wa utakatifu) kwa mbora wa Watukufu).(Muqaddima ibni Khuldoon, p 271).
25. Khatama Al
Muhaddithiin wal Mufassiriin(Muhuri
wa wapokezi na Wafasiri) limetumika kwa Shah 'Abbdul' Azeez.(Hadiyyatul Shi'ah)
26. Khatamn Al
Makhlooqaat Al- Jismaaniyyah(Muhuri
wa maumbile) limetumika kwa Wanaadamu. (Tafsiir Kabeer, juzuu 2, p.22,
imechapishwa Misri)
27. Khatam-Atul-Huffaz limetumika
Shaikh Muhammad Abdullah.(AlRisaail Naadirah, uk.30)
28. Khatam Atul
Muhaqqiqiin limetumika kwa Allama Sa'adudiin
Taftazaan. (Shra Hadiithul Arbaiin, uk1)
29. Thatama Atul Hufaaz
limetumika kwa Ibn Hajrul Asqalaan.(Tabqatul
Madlaseen).
30. Khatam Al Mufassiriin(Muhuri
wa Wafasiri) limetumika kwa Maulana Muhammad Qaassim.(Israare Quraan).
31. Khataman Al Muhaddithiin(Muhuri
wa Wapokezi)limetumika kwa Imamu Suyuut. (Hadiyatul She'eah, uk. 210)
32. Khatama Al Hukkaam(Muhuri
wa Watawala) limetmika kwa Wafalme).(Hujjatul Islam, uk.35)
33. Khataman Al Kaamiliin(Muhuri
wa wakamilifu) limetumika kwa Mtume(Hujjatul Islam, uk. 35).
34. Khataman Al Miraatab(Muhuri
wa vinyago) kwa vinyango vyene taswira ya watu).
35. Khatam Al Kamaala(Muhuri
wa miujiza) limetumika kwa Mtume(s.a.w)(ibid 140)
36.Khatam
al Asfiyaat al Immah(Muhuri wa maruhani wa Taifa) limetumika kwa Issa
(A.S). (Baqiyyatul Mutaqaddimiin),
37. Khatama Al Ausiyaa(Muhuri
wa watoa Nasaha, Washauri) limetumika Sahaba Ali)(Minar Hudaa)
38. Khatam Al Mua'llimiin(Muhuri
wa Waalimu/ Wasomi) limetumika kwa Mtume(s.a.w). (Alsiraatul Sawee na Allama
Muhammad Sabtain,sasa, mimi ni mwalimu, na mnajua
kwamba nitabaki kuwa hivyo, baada ya Mtume(s.a.w) lakini wakati wote ninakaribi
kuwa mwalimu kwa ukamilifu zaidi
39. Khaatamn Al Muhaddithiin(Muhuri wa Wapokezi) limetumika kwa Al Shaikhul
Sadooq.(Kitaab Man Laa yahdarahul Faqiih).
40. Khatam Al
Muhaddithiin, limetumika kwa Maulana Anwar Sjha wa kashmir.(Kitab
Raeesul Ahrar)
Katika mifano yote hiyo
iliyotolewa na Mirza hakuna hata rejea moja ya Hadithi za Mtume(s.a.w)
iliyotumika kuthibitisha madai hayo. Kwa nini?
Kwa
nini Makadiani wameziondoa Hadithi hizi?
Ingawa kila Kadiani
akiwemo Mirza mwenyewe, wanadai kwamba wanaamini Qur'an na Hadithi na
wanampenda Mtume(s.a.w), bado wamezipuuza hadithi
hizo, ambazo zinzkanusha kwa uwazi kabisa madai ya Mirza Ghulam Ahmad, Qadiani.
Uthibitisho uko katika nukuu ifuatayo inayotokana na
kitabu cha Mirza:
"Msingi wa madai yetu sio Hadithi za Mtume wala Qur'an bali ni Wahyi
ulionijia. ndiyo, katika kuunga mkono vile vile
tunawasilisha Hadithi hizo ambazo ni kwa mujibu wa Qur'an na hazigongani na
Wahyi wangu, hadithi zilizobaki nazitupilia mbali mitihili ya karatasi
chafu"(Roohan Khazain Vol. 19 uk. 140).
Nukuu hiyo inaonesha sura
halisi ya Mirza Qadian na harakati zake za Ahmadiyya.
Hadithi yoyote inayopingana na madai ya Mirza
hutupiliwa mbali mithili ya takataka. Mtu mwenye dharau
Kitu kingine!, rejea moja, ambayo ingepasa kuwa muhimu kwa kila Kadiani
ambayo vile vile ni mashuhuri katika zilizokosekana katika orodha hiyo, ni ipi
hiyo? Ni ile inayotokana na vitabu vyake mwenyewe
Mirza Ghulam Ahmad. Orodha hiyo hapo juu mara kwa mara hunukuliwa katika
maandiko Ahmadiyya kuhalalisha tafsiri
Udanganyifu wa 3 wa Kadiani-
Tafsiri pekee inayo ya Khatam inayopatikana katika Kamusi la Mirza
Neno Khatam, limetolewa
mifano zaidi ya 40 na Makadina lakini hakuna hata
mfano mmoja unaotolewa kutoka katika vitabu vya Mirza Qadian. Haishangazi kama utakavyoona kurasa za mbele. Waulizwe Makadiani Mirza
alikuwa na maana gani kwa neno Khatam? Hii ni muhimu
Tunapoviangalia vitabu vya
Mirza Qadian, tunakutana na nukuu ambazo zinaweka wazi
jinsi Mirza alivyoilewa maana ya Neno Khatam:
Khatam ul Walad Anbiya- mtoto wa kiume wa mwisho
“Mimi nilikuwa Khatam ul Walad(muhuri wa watoto) kwa baba yangu, hapana mtoto
mwengine aliyezaliwa baada yangu”(Braheem Ahmadiyya sehemu ya tano, Roohan
Khazain, juzuu ya 212 uk. 113).
2. Khatam ul Anbiya- Mtume wa mwisho
“Baadhi ya bishara katika
vitabu vya awali vya Mwenyezi Mungu kuhusiana na Nabii Issa zinafanana na na bishara (ya kuja
Mirza) ambayo Mayahudi hawataikubali.
3. Khatam ul Khulafa-
mwisho wa Mkhalifa.
“Kiroho mimi ni Khatam ul
Khulafa katika Uilsmu,
“Nukuu
kutoka vitabu vya Mirza Ghulam Ahmad, zinathibitisha kwamba neno Khatam Mirza
Ghulam lina maana mwisho au mwisho au chochote ambacho kilichopigwa muhuri. Je hii ndio sababu ya wao kupuuzia na ndio kuoziondoa
kimya kimya kunakolenga kuwazuga watu au kutoyafahamu maandiko ya Mirza? Unaachiwa wewe msomaji uamue.
Udanganyifu wa 4-Mirza adai kuwa yeye ndiye mwisho wa Mitume.
Suala ni
kwamba kwa nini maana ya neno moja imekuwa ikibadilika inakuja kuelezea Khatam
un Nabiyyin? Na kwa hakika iwapo maana ya neno Khatam
un Nabiyyin ni kwamba Mitume zaidi watakuja kwa idhinisho na muhuri wa Mitume,
kwa hiyo neno Nabiyyin kwa mujibu sarufi ya kirabu maana yake lazime kuwepo
walau mitume watatu zaidi. Lakini maandiko ya Mirza Ghulam yanatupa taarifa
nyingine:
Abarikiwe yule
anayenitambua mimi. Katika njia zote za Mwenyezi Mungu
mimi ndiye njia ya mwisho, katika mianga yake yote,
mimi ndiye mwanga wa mwisho. Bahati mbaya yule anayenitelekeza, kwa sababu bila
ya mimi kote ni
Jarida rasmi la makadiani
liliandika:
“Nukuu hizi zinathibitisha
kwamba kwa ajili ya Masihi aliyeahidiwa hapana mwingine anayeweza kuwa Mtume
baada ya Mtume(s.a.w) ila ni mtume mmoja tu aliye wa
lazima na kuja kwa mitume wengi kutatia dosari busara ya mpango wa Mwenyezi
Mungu.”(Tasheed ul Azhan, Qadian, Na. 8, juzuu ya 12, uk.11
tarehe Agosti 1917).
Ni wazi kwamba maelezo
haya potofu juu ya neno Khatam, hayana maana ya mwisho bali
muhuri, yalikuwa yamefungua mlango wa utume, na kwa kupitia upenyo huu Mirza
yeye huyo kwa mara nyngine akaufunga. Kwa maneno mengine, Mirza ameona haya
alijaribu kuiba taji la Khatama un Nabiyyin kutoka kwa Mtume(s.a.w),
yaweza kuwa kejeli mbaya kwa Mtume(s.a.w).
Kwa kweli jambo
Udanganyifu Na. 5-Nani
Mirza Qadian
Kila Qadian atasema
kwamba, anaamini Khatam Nabiyyin, kwamba anamtambua Muhammad(s.a.w)
kuwa ni Miwsho wa Mitume, lakini bado atamtambua Mirza
Hebu ifahamike kwamba
mfuasi muaminifu wa Mirza Ahmad Kadian lazima akitii
kile kilichosemwa na kuandikwa na MIrza, imani yake inapaswa kuwa imani ya
inayoelezwa na maadniko ya Mirza, bila ya kujali kuwa yeye kasoma vitabu hivyo
au la. Kadian hawezi kuwa na imani inayojikanganya na
maandiko ya Mirza. Iwapo hakubaliani na mafundisho
yake ajikute kuwa si mkweli katika imani hiyo ya ‘Uislamu’ hivyo ni bora
awakane Mirza na Jamaat yake. Hawezi kupanda majahazi mawili
tofauti. Akisema hivi basi ni vyema ionekane
sasa Mirza ana maana gani katika hiyo Khataman Nabiyyin.
Mirza amedai kuwa yeye
ndiye Muhammad
Wahyi wa
Mirza unatufahamisha ifuatavyo:
“Muhammad Rasuulullah wa
Laziina ma’ahoo ashiddahuu alal Kuffari Ruhamahuu baina hum’ katika ufunuo huu
Mwenyezi Mungu ameniita mimi Muhammad na vile vile mjumbe(Roohan
Khazain juzuu 18
Yeyote anayenitofautisha
mimi na Mustafa(s.a.w), hakuniona mimi na
hanitambui”(Roohani Khazain juzuu 16uk.171).
Mirza adai kuwa yeye ni Khatam ul Anbiyya.
Nimekuwa nikisema kuwa kwa
mujibu wa aya “Waakhariina minhum lamma yalhaquu behim na wengineo miongoni
mwao ambao hawajaungana nanyi(Qur’an 62:3) katika aina ya Borooz(
iliyotafsiriwa na Makadiani kuwa ni taswira, nakala halisi) mimi ni yule yule
Mtume, Khataman ul Anbiya(mwisho wa Mitume). Na miaka ishirini iliyopita
Mwenyezi Mungu ameniita mimi Muhammad na Ahmad katika
Braheen Ahmadiyya, na kutangaza kwamba mimi ni Mtume mtukufu. Kwa hivyo utume
hakuna namna yoyote unagongana na hadhi ya Mtume mtukufu(s.a.w)
Utume ulifikia mwisho kwa
Mtume wetu(s.a.w). Kwa hiyo baada yake hakuna Mtume
isipokuwa yule ambaye ameng’arishwa na mwanga wake na
yule ambaye amefanywa mrithi na Mwenyezi Mungu. Jueni kuwa umwisho alipewa Muhammad(s.a.w) tangu
mwanzo na kisha baadaye akapewa(Mirza)
ambaye alifundishwa na roho na kufanywa kivuli chake. Kwa hivyo amebarikiwa
yule ambaye amefundisha na amebarikiwa yule ambaye amejifunza(Mirza).
Kwa hivyo Mwisho wa Utume ulikadiriwa kuwa Milenia sita ambayo ni siku ya sita
katika masiku ya Mwenyezi Mungu....Kwa hivyo Masihi aliyeahidiwa alizaliwa
katika Milenia ya sita”.(Zamima Khutba Ilhamiah,
Roohani Khazain juzuu ya 16uk 310).
Mirza adai yeye ni
nakala halisi ya Muhammad(s.w)
Walakin Rasuulallah wa
Khaataman Nabiyyin, katika aya hii kuna utabiri uliojicha hapa ambao ni kwamba
kuna muhuri unaohusiana utume mpaka siku ya hukumu, na isipokuwa kwa nakala
halisi amaye ni yeye, hapana yeyote mwenye uwezo wa kufungua lango la eleimu
iliyojificha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ka walivyokuwa Mitume; na kwa vile huyo
nakala halisi wa Muhammad amabye ni yule Masihi aliyeahidiwa tangu zama za
awali, ni mimi kwa hiyo utume ni nakala aniliyopewa. Sasa ulimwengu mzima
hautasiaidia mbele ya utume huu kwa sababu kuna muhuri
wa Manabii. Mtu anayefanana na Muhammad kwa sifa zote
ameshatokea. sasa mbali ya dirisha
Mirza adai yeye ni Muhammad aliyekuja kwa umbile lingine
"Nilipokuwa ni yule
Mutme aliyekuja kwa umbile lingine na nilipokamilisha yale yote ya Muhammad
ikiwa ni pamoja na Utume unaojiakisi kwa kioo cha kivuli changu, hivyo ni nani
huyo anayeweza kudai utume akiwa mtu mwingine"(Ek Ghait Ka Izala, uk.8
Roohan Khazain, vol 18,uk. 212).
"Mwenyezi Mungu
amenipa mimi neema ya aliyompa Mtume Mtukufu na
akanifanya mimi mkamilifu na amenifanya kuwa mwenye huru na mpole
Mirza amedai kuwa yeye
ni mbora kuliko Mtume(s.a.w).
"Ukweli ni kwamba
kiini cha kuja katika umbile jingine la Mtume mtukufu mwisho wa milenia ya
sita(zama hizi katika sura ya Mirza), kina nguvu zaidi, kikamilifu zaidi na
chenye msukumo zaidi kuliko zile zama za awali, ni sawa na usiku wa mbalamwezi
ya mwezi 14 mng'aro(Khutba i Ilhamiyah, Roohan Khazain, juzuu 16 uk 271-272).
Utukufu wa Mtume wetu(s.a.w) ulionekana miaka elfu 5 ukiwa sawa na sifa zake
na kipindi hicho hakikuwa kilele cha mandeleo ya kiroho. Kilikuwa hatua ya
mwanzo kuukwea mnara mrefu wa ukamilifu wake. Baada ya
hapo kumea huko kiroho kwenyewe kulifikia haiba yake kamili mnamo miaka
alipozaliwa Qadian wakati huu"(Mirza in Khutba i Ilhamiyya, Roohan
Khazain, vol 16,
Mirza ameingizwa katika
Kalima ya Shahada
Pamoja na kuja Masihi
aliyeahidiwa imetokea tofauti moja(katika maana ya Kalima) imetokea na hiyo
ilikuwa kabla ya kuja Masihi, katika maana ya Muhammad Rasuulullah nyakati hizo
ilikuwa wakitajumuishwa na mitume, lakini alipokuja Masihi aliyeahidiwa, Mtume
mmoja zaidi ameongezwa katika maana Muhammad Rasuulullah...kwsa hiyo katika
kuingia Uislamu bado ni Kalima hiyo,
tofauti moja tu ni kwamba kuja kwa Msihi aliyeahidiwa kumemuongeza Mtume mmoja
katika maana yake...zaidi, hata kama tutakubali kwa kujaalia kutokuwezekana
kwamba jina takatifu la Mtume(s.a.w) kwamba limejumuishwa katika kalima tukufu
kwasababu yeye ni mwisho wa Mitume hata hivyo hapana haja na hatuhitaji kalima
mpya kwa sababu Masihi aliyeahidiwa si mtu anayeweza kutenganishwa na Mtume
mtukufu, kama yeye(Mirza) mwenyewe alivyosema: "Umbile langu ni lile hasa
umbile la Muhammad Rasuulullah".
Vile vile, "yule anayenitenganisha mimi na
Mustafa hatakuwa ameniona mimi wala hanitambui. Na hoja yake hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu ameahidi kwamba atamleta katika
umbo lingine "Khataman Nabiyyin" katika ulimwengu huu kwa mara
nyingine zaidi
Shairi lifuatalo lilisomwa
mbele ya Mirza ambaye alilipenda na aliripotiwa kusema
Jazakallah shairi
"Muhammad ametumwa
tena miongoni mwetu na atakayekuwa mkubwa zaidi kuliko
kabla ya hapo. Aanayetaka kumuona Muhammad katika ukamilifu anapaswa
kumuangalia Ghulam Ahmad wa Qadian"
(Shairi hilo lilitungwa na
Qazi Zahoor Ahmad Akmal Qadian ambalo lilisomwa mbele ya Mirza Qadian,
lilichapishwa katika Gazeti la Paigham us Sulh la tarehe 14 Machi, 1916)
Kwa mwanga wa maandiko hayo hapo juu, Machapicho rasmi ya Makadiani
yalieneza imani imani hii:
"Hivyo yupo yeyote
mwenye shaka kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma Muhammad(s.a.w)
tena katika nchi ya Kadiani kukamilisha ahadi yake?(Kalimat al Fasl na Mirza
Basheer Ahmad mtoto wa Mirza Ghulam A. Qadian, Review of Religions
Taji la Masihi aliyeahidiwa , mbele ya Mwenyezi Mungu ndilo Taji la
Mtume(s.a.w). Kwa maneno mengine, katika kumbukumbu za Mwenyezi Mungu hapana
uwili au tofauti kati ya Masihi aliyeahidiwa na Mtume(s.a.w).
Wote hao wawili wana hadhi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Kwa nafasi, hadhi na jina
Masihi Mowood si kitu
kingine kinachotofautiana na Mtume(s.a.w), lakini ni
yeye ambaye amekuja tena katika ulimwengu akiwa katika sura halisi...Kwa hiyo
kuna shaka yoyote kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma tena katika Qadian?"(Kalimat Alfas uk.104-105, Review of Religion Qadian March 1915.
Hitimisho
Ni wazi kutokana na kile kilichosemwa hapo juu kwamba ndio dini ya Ukadiani
kuwa imani zifuatazo:
. Mirza ni
Mtume na mjumbe wa Mwenyezi Mungu
. Mirza ni
Muhammd aliyekuja kwa umbo lingine
. Mirza hatenganishwi na Mtume(s.a.w)
. Mirza ana hadfhi sawa na
Mtume(s.a.w)
. MIrza ni mbora kuliko Mtume(s.a.w)
. Mirza ni
mtume wa mwisho
. Kwa hiyo Mirza ndiye
Khatam un Nabiyin
Tahadhari:
Pale Qadian anapodai kuwa
anamini Mtume(s.a.w)
Kwa mujibu wa Fatwa yake,
iliyotajwa huko nyuma Mirza ni mdanganyifu, mzushi,,
si muumini wa Qur'an, anaipinga Qur'an, muongo, Murtad, sio Muislamu, adui wa
Qur an ana hana haya mbele ya Mwenyezi Mungu.
Yaa Allah waepusha
waislamu na imani ya Ukadiani iliyojighushia jina la
Uislamu. Ya Allah warejeshe kwenye njia sahihi wale waliopotea kwa bahati mbaya kutokana na udanganyifu wa Ahmadiyya?
Wassalaam alaykum alaa mani tTaba'al hudaa
Amani iwe juu ya wale
wanaofuata uongofu.
Dr Syed Rashid Ali
Dibba Fujairah