BISMILLAH RAHMANIIR RAHIIM
25th Sept 2003
Ni nani alikuwa Mungu wa mirza wa qadiyyan?
[NA DK Sayid Rashid Ally]
watukufu waislamu
Asalam Aleykum
Kwa mujibu wa imani ya kiislamu MwenyeziMungu ndiye muumba wa ulimwengu na kila kitu kilichopo ndani yake ndiye muweza wa yote mfalme na muhimiliwa kila kilichopo ulimwenguni na nje ya ulimwengu.
Yeye ni mmoja na mpweke hana mshirika yeye ni mwingi wa rehema .mjuzi wa yote wa milele na milele na mola wa walimwengu wote,Mfalme wa siku ya malipo.
Hakika yake ameepukana na aina zote za mapungufu,dosari na kasoro.hashikwi na usingizi na wala alali hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna aliyefanana naye.
MwenyeziMungu ameleta mitume na manabii(amani na rehema ziwe juu yao)amewashushia wahyi ili wawaongoze wanadamu katika njia sahihi nako ni kumpwekesha mwenyezimungu.na katika hao mitume na manabii wa mwisho wao katika ule mlolomgo mrefu wa manabii si mwingine ila ni Mustafa Muhammad[s.a.w]ndiye aliyeleta ujumbe wa mwisho kabisa katika kitabu cha QURAN ili kiwaongoze wanadamu katika maisha ya o ya kila siku mpaka siku ya mwisho. Lakini Mirza Ghulam Ahmad mzaliwa wa qadiyyan ambaye ndiye muanzilishi wa dini ya ahmadiyya[qadiyyan]yeye alikuwa na dhana ya ajabu sana juu ya Mungu.japo kuwa alidai kuwa yeye ni muislamu mtazamo wake juu ya Mungu sio ule unaobainishwa na uislamu.hivyo mtu unastaajabu kwani Mirza Ghulam alidai yeye anapata ufunuo toka kwa mungu hizo funuo anazodai kushushiwa na huyo Mungu wake ni za ajabu na zenye fedheha kubwa ndani yake kiasi kwamba moja kwa moja mtu unaamini kabisa bila kipingamizi kuwa hizo funuo zake si za kutoka kwa mungu bali funuo hizo zaMirza alikuwa anafunuliwa na shetani na kwa hiyo Mirza hakuwa muislamu bali ni kafiri wa wazi wazi InshaAllah katika makala hii tutaonesha funuo hizo anazodai kufunuliwa Mirza toka katika vitabu vyake mwenyewe Mirza tutataja kitabu ,kurasa na jalada ambamo zimo funuo hizo mtajionea kweli funuo hizi ni kutoka kwa mungu au shetani?
Mirza anasema
‘qayuum-ul-alamiin’ni moja
ya majina au sifa za mwenyemungu ni mwenye
mikono na miguu mingi
isiyoweza kuhesabika na kila mguu ni mrefu kiasi
ambacho hauwezi kuhesabika
na mungu ana upana usio na mwisho na
urefu usio na ukomo na yuko
kama chui na pia ana nyaya zilizosambaa
sehemu zote za dunia’ Taz.Roohan khazain juzuu ya 3uk.90
Mirza anadai kapata ufunuo kwa kiarabu mungu anamwambia
‘Nahmaduka[nakutukuza wewe]’Tazama Haqiiqatul-wahyi,Roohan khazain juz.22 uk 97
MIRZA ADAI MUNGU KASHUKA
CHINI KWA AJILI YAKE
Katika ufunuo huu Mirza anadai mungu kamwambia hivi
‘nimeshuka chini kwa ajili yako’Taz.HaqiqatulRoohan Khazain juz.22uk.97
Mirza
anasema kuwa kapata ufunuo mungu anamwambia kuwa atashuka kijijini alikozaliwa
Mirza yaani kijiji cha qadiyyani Mirza anasema:-
‘punde nimepata wahyi kuwa
mungu atashuka kule qadiyyan kulingana na
ahadi yake’Taz.tadhkirah collection of inspiration uk 452 toleo la 2 akiendelea zaidi na madai yake upotovu Mirza hapa anadai mungu atashuka kama mtoto Mirza anasema kapata ufunuo unamwambia “Tunakupa habari njema za mtoto ambaye kwaye haki itadhihirika kama vile mungu ameshuka chini”Haqiiqatull wahyi,Roohan khazainJuz.2 uk 99
Mirza anasema:-
“Mungu wa kweli ni yule
aliyemtuma mtume wake kule Qadiyyan’
Taz. Dafa Alba Roohan khazain juz.18 uk.231
Hii maana yake ni kuwa Mirza anajithibitisha kuwa yeye ni nabii wa kweli na mungu aliyemtuma yeye ndiye Mungu wa kweli lakini kwa vile Mirza ni mzushi mkubwa kabisa na ni wakala wa shetani na huyo anayeitwa mungu wake anayemshushia wahyi si chochote bali ni sheitwani!!! Tutaona zaidi uko mbeleni katika sehemu inayofuata itadhihirishia zaidi kuwa huyu anayemtuma Mirza ni sheitwani aliyemlaghai Mirza na kufanikiwa kuingia naye motoni.
Wapendwa katika imani Quran tukufu na hadith sahihi za Mtume zinatuthibishia kuwa baada ya kuja nabii mtukufu Muhammad [s.a.w]unabii umekoma na wahyi pia umekoma hata hivyo Mirza yeye bado anafanya ugagalizi na kudai kuwa yeye ni nabii wa mungu na mpokezi wa wahyi kutoka kwa mungu miongoni mwa madai chungu mzima aliyoyatoa kuhalalishia upotovu wake ili kuhalisha madai yake ya unabii hapa mirza anadai ikuwa ulimi wa Mungu una ugonjwa fulani Mirza anasema
‘Je mtu mwenye akili timamu
anaweza kukubali kuwa eti katika zama
hizi mungu anasikiliza
lakini hazungumzi kitu sasa basi swali linakuja
kwa nini hazungumzi je amepata ugonjwa kwenye ulimi wake?”
Taz.Zamima braheen ahmadiyya sehemu ya 5,Roohan khazain juz 21uk321
Mirza anaendelea kusema hapa sasa anasema yeye kaambiwa na mungu kuwa ametoka katika katika kiti chake cha ufalme mirza anasema kaambiwa na Mungu wake[sheitwani] hivi
“wewe kwangu unatoka katika
kiti changu cha ufalme”
Taz.Haqiiqatu-l-wahyi,Roohan
khazain juz.22uk89
Mirza hapa sasa anazidi kututhibitisha wahyi wake ni washetani sasa hapa anadai kuwa ni mungu mirza anasema
“Nimeona katika ndoto yangu
kuwa mimi ni mungu na nikaamini
kuwa ni kweli” Taz.kitabul-bariyah,Roohan khazain juz.3uk.103
Mirza anasema
“Mungu aliingia mwilini
mwangu….na katika hali hiyo nikawa nasema tunataka
Pepo mpya na ardhi mpya na
mbingu mpya kwa hiyo nikaanza kuumba mbingu
Na ardhi katika umbile dogo
ndani kukiwa hamna utaratibu wa vitu tofauti
Kisha kwa matakwa ya mungu
nikaumba mfumo wa vitu mbalimbali ni
Mimi nikawa ninajiona kumbe
nina uwezo wa kuumba hivyo nikaumba
Mbingu na dunia nikasema
tumeipamba mbingu na dunia kwa mataa
Kisha nikasema kuwa sasa tutaumba mtu kutokana na udongo wa ardhi” Taz. Kitabul bariyyah,Roohan khazain juz.3uk.104-105
Mirza anaendelea kudaiyeye na mungu kitu kimoja anasema kaambiwa hivi na mungu wake
“Wewe kwangu ni kama kitu kimoja na dhati moja”Taz.haqiiqatul wahyi,Roohan khazain juz.22 uk 89
MIRZA ADAI KAGEUZWA NI MKE
WA MUNGU
Mirza anasema
“kama vile maryamu roho ya
Issa ilipulizwa mwilini mwake na mimi
pia nikawa mja mzito na baada
ya miezi mingi kutokana na ufunuo
uliomo katika barahheen
Ahmadiyya sura ya 4uk 556 nikageuzwa kutoka
maryam na kuwa Issa bin Maryam’Taz,kishtee-e-nooh,Roohan khazainjuz.19uk50
kwa
hiyo wapenzi wasomaji mnajionea vituko hivyo vya Mirza yaani anabadilika kutoka
katika mirza bin chiragh bibi na kuwa Maryam alafu anakuwa mja mzito wa miezi
kumi na baadaye anajizaa mwenyewe na
kuwa Issa na kisha anadai kuwa yeye ndiye Issa bin maryam masih aliyeahidiwa
Wasomaji nadhani mtaona tunatumia maneno makali lakini ndio hivyo maana mirza mwenyewe ndio katamka hivyo nasi anatufanya tufikie hapo kwani nia yetu ni kumdhihirisha waziwazi watu wote waone upotovu wake na yote hayo tunayanukuu kutoka katika vitabu vyake kama yalivyo ninyi wenyewe mtapima na kumuona alivyokuwa punguani sasa hapa anadai kapata hedhi Mirza anasema kuwa mungu wake kamwambia hivi
“Babuillah bukhsh anataka kuona damu yako ya mwezi au japo
apate taarifa juu
yako lakini mungu atakuonesha fadhila zake ambazo zitadumu daima na mwilini mwako kuna hedhi bali mtoto ndiye anaendelea kukuwa mtoto huyo ni kama mwana wa mungu”Taz.tatumma haqiqatul wahyi, Roohan khazain juz.22 uk 581
tukiendelea zaidi na uchambuzi wetu hapa sasa Mirza anadai mungu kawa kama mwanaume na yeye ni kama mwanamke
“wakati Fulani Hazrat Masih muwuud alieleza hali hii kuwa wahyi kuwa ulimshukia katika hali ambapo mungu alikuwa kama mwanamme na yeye kama mwanamke na mungu akaonesha ulijali wake kwake”[kwa wanaoelewa dokezo hili linatosha]Taz.islam qurbqn track no 34by Qazi yar mohammed qadiyyan ASTAGHFIRULLAH wasomaji tokea kuja kwa wanadamu hakuna hata mmoja ambaye amethubutu kutoa madai kama hayo hata wale manabii wa urongo je tujiulize ni mungu gani huyo anayeweza kumgeuza nabii wake kuwa mkewe bila shaka huyo anayemzungumza Mirza si mungu bali ni shetwani na nabii wake ndioMirza
MIRZA ADAI TENA SASA YEYE
NI MWANA WA MUNGU
Mirza anasema kaambiwa hivi katika ufunuo na huyo mungu wake [sheitwani]
“Wewe [Mirza]kwangu mimi ni kama mwanangu kuanzia zama hizi,wakristo wapumbavu waliokuwa wamemfanya yesu ni mungu kwa hiyo busara ya mungu ikataka maneno mengine zaidi yatumike kwa mtu mnyenyekevu ili macho ya wakristo yafumbuke na wayaelewe hayo maneno ambayo kwayo wamemfanya Yesu ni mungu na katika umma huu ni mtu mmoja tu ambaye kwa maneno hayo yametunika”Taz.Haqiqatull wahyi, Roohan khazain Juz.22 uk.89
MIRZA ADAI MUNGU ATAKUJA
KAMA MWIZI