Bismillahir rahamanir rahiim
SWAHILI
Sema ukweli umedhihiri, uongo umejitenga
Mirza Ahmad Qadiani, ndiye Mahdi au Masihi aliyeahidiwa?
Na.
Dk. Rashid
Assalaam
Alaykum
Uislamu dini ni teule ya Allah; Qur'an ni ujumbe wa mwisho wa Muumba kwa
Wanaadamu ulioletwa kupitia Mitume wake na Mtume wa mwisho katika mlolongo wa
mitume hao ni Muhammad(SAW).
Katika
hadithi kadhaa, Mtume ameripotiwa kusema kwamba yeye ni Mtume wa mwisho wa
Allah(SW). Mtume Muhammad
alibashiri juu ya kuja kwa Mahdi(a.s) na kuja tena kwa Nabii Issa kabla ya
kiyama.
Hata hivyo, katika kipindi cha miaka 1400 iliyopita wamejitokeza
wadanganyifu wengi ambao wamekuwa wakitoa madai ya uongo kuhusiana na nyadhifa
hizi tatu; Mtume, Masiha na Mahdi. Katika wadanganyifu hao Mirza alidai kuwa
yeye ni Mtume, yeye ni Masih na yeye ni Mujadid(Muhuishaji wa Uislamu).
Makala hii fupi itachunguza
madai yote haya matatu kwa kutumia Qur'an na Hadithi za Mtume kwa ajili ya
manufaa ya Waislamu wote hasa wale wasio na mwanga mzuri wa mafundisho ya
Uislamu ambao pamoja na kutomuona wala kumsikia Mirza lakini wametumbukia
kiupofu kufuata itikadi yake kutokana na harakati za kundi la Ahmadiyya.
Uislamu - Dini teule ya Allah
Mwenyezi
anatufahamisha katika Qur'an:
"Leo
hii nimekamilisha ujumbe wangu kwenu na nimekuchagulieni Uislamu kuwa dini
yenu(njia yenu ya maisha)(5:3)
Kuhusiana na Mtume Muhammad(s.a.w)
Allah
anatufahamisha kuwa Muhammad(s.w) ndiye Mtume wa mwisho na hakuna Mtume
mwingine baada yake:
"Muhammad si
baba wa yetote miongoni mwa wanaume wenu bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na
Muhuri(mwisho) wa Mitume na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu(33:40).
Mtume
Muhammad katika hadithi kadhaa ameweka wazi zaidi kwamba yeye ndiye Mjumbe na
Mtume wa mwisho wa Allah(s.w), na hakuna mtume wmingine baada yake. Baadhi ya Hadithi hizo ni:
Mtume
amesema: "Wana wa Israil waliongozwa
na Mitume. Kila Mtume alipotawafu, aliinuliwa Mtume mwingine kushika nafasi
hiyo. Lakini baada yangu hakuna Mtume mwingine; watakaofuata baada yangu ni
Makhalifa.(Bukhari, Kitab al Manaqib).
Katika
Hadithi nyingine Mtume ameripotiwa kusema: Nafasi yangu katika mlolongo wa
mitume walionitangulia inaweza kufafanuliwa na mfano ufuatao:
"Mtu amejenga nyumba na kuinakshi vizuri lakini ikawa kwenye kona moja
likakosekana tofali moja.. Watu wakaajabia uzuri wa nyumba hiyo lakini wakashangazwa na kukosekana
tofali katika kona hiyo. Mimi ninafanana na tofali hilo na mimi ni wa mwisho
katika mlolongo wa Mitume". (Bukhari, Kitab Manaqib)( Kwa maneno mengine
kuinuliwa kwa Mtume Muhammad(s.a.w) kunakamilisha haja ya utume, ameziba mwanya
unaoweza kuhitajia kuja kuzibwa na mtume mwingine).
Kadhalika
Mtume(s.a.w) amesema: Mwenyezi Mungu amenifadhilisha mimi katika mambo sita
ambayo mitume wengine hawakufadhilishwa mambo hayo ni:
1.
Nimetunukiwa urahimu na ufasaha wa kusema
2.
Nimebarikiwa uwezo wa kuwashinda maadui
3.
Nimehalalishiwa kupigana vita
4.
Ardhi yote imefanywa mahali pa kufanyia ibada kwangu na imefanya kuwa ya kujitaharishia.
Kwa maneno mengine katika dini yangu
swala haukufungiwa iwe inafanyika amahali maalum pa ibada. Swala
ya kuswaliwa mahali popote twahara katika
Ardhi hii. na
yanapokosekana
maji inajuzu kuchukua udhu kwa kutumia udongo(kutayamamu)
na kujisafisha miili kwa kutmia udongo inapotokea
uhaba wa maji.
5.
Nimetumwa na Allah kupeleka ujumbe kwa ulimwengu mzima. Na
6.
Mlolongo wa Mitume wa Allah kwa Wanaadamu umekomea kwangu
Mtume(s.a.w)
amesema: Mkufu wa wajumbe na Manabii
umekamilika baada ya kuja kwangu. Hakutakuwa na Mtume atakayekuja baada
yangu"(Tirimidh, Kitab-ur Rouya
babu Zahab-un - Nubuwwa, Musnad Ahmad, Marwiyat- Anas bin Malik)
Mtume(s.a.w) amesema: ”Mimi ni
Muhammad, Mimi ni Ahmad, mimi ni mfutaji, ukafiri utafutwa kupitia mafundisho
yangu; mimi ni mkutanishaji. Watu watakutanishwa siku ya mwisho baada yangu(Kwa
maneno mengine kitakachokuja baada yangu ni simu ya hesabu). Mimi ni mwisho kwa maana kwamba hapana mtume
atakayekuja baada yangu"(Bukhari na Muslim, Kitab al Fadhaail, Bab:
Asmaun Nabi; Tirmidh, Kitab ul Adab, Bab: Asma un Nabi; Muatta, Kitab u Asmain
nabi, Al Mustdrak Hakim, Kitabul Fitan, Bab: Dajjal).
Abdur
Rahman Bin Jubair ameripoti: Nilimsikia Abdullah Bin Amr ibn Al As akihadithi
kwamba siku moja Mtume alitoka nje ya nyumba yake na kujumuika nasi. Kwa jinsi
alivyoonekana ilikuwa kama anatuaga.
Akasema:
"Mimi
ni Muhammad, sijui kusoma wala kuandika ni Mtume wa Mwenyezi Mungu' akarudia
mara tatu kusema hivyo. Kisha akatamka: hapatakuwa na Mtume mwingine baada
yangu"(
Musnad Ahmad, Marwiyat Abdullah bin Amr ibn-As).
Mtume(s.a.w)
alimwambia Ali kwamba, Wewe unahusiana na
mimi kama vile ilivyokuwa kwa Harun na Musa(a.s). Lakini hapatakuwa na Mtume
baada yangu". (Bukhari na
Muslim, Kitab Fadhail as Sahaba).
Thauban
ameripoti kwamba: Mtume(s.a.w) amesema: Kutaibuka wadanganyifu thalathini
katika umma wangu na kila mmoja kati yao atautangazia ulimwengu kuwa yeye ni
Mtume, lakini jueni kwamba mimi ndiye wa mwisho katika mlolongo wa Mitume wa
Allah na hakuna Nabii atakayekuja baada yangu".(Abu Dawud, Kitab ul Fitan).
Mtume(s.a.w)
amesema: Hakuna Mtume atakayeinuliwa baada yangu na kwa hiyo hapatakuwa na
wafuasi wa Mtume mpya baada yangu"(Baihaq,
Kitab ul Rouya; Tabaran).
Mtume(s.a.w)
amesema: Mimi ni wa mwisho katika mlolongo wa Mitume wa Allah na Msikiti
wangu(akiashiria msikiti wa Madina) ndio wa mwisho".(Muslim, Kitab ul Hajj; Bab: Fadl us Salat bi Masjid Makka wala
Madina).
Kutokana
na Hadithi hizi sahihi, itakuwa wazi kwa msomaji kwamba
hakuna Mtume baada ya Muhammad. Hata hivyo akionesha kupuuza kabisa maelezo
hayo ya Mtume, Mirza Ghulam Qadiani ni miongoni wa waliodai kuwa ni Mitume wa
Allah. Mirza ametamka wazi wazi kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu matamshi
ambayo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Qur'an na Hadithi za Mtume(s.a.w).
Ni nani atakayekuwa Imam Mahdi kama ilivyobashiriwa
katika Ahadithi za Mtume Muhammad(s.a.w).
Dai
jingine la Mirza Mwasisi wa Kundi la Ahmadiyya ni kwamba yeye ndiye Imam Mahdi.
Waislamu wengi wameonekana kutekwa na dai hili. Hebu tutazame Mtume(s.a.w) nini
amesema kuhusiana na kuja kwa Imam Mahdi.
.
Neno halitafutika mpaka mtu miongoni mwa
familia yangu, ambaye jina lake litakuwa
jina langu, atakayewaongoza Waarab wote(Tirmidh
Sahihi, juzuu ya 9, uk. 74; Abu
Dawud, Sahihi, juzuu5, uk.207; vile vile imeripotiwa na Ali bin Abi Talib, Abu Sai'd
, Um Salma, Abu Huraiyra).
. Kabla ya siku ya Hukumu, Allah atamleta
kutoka mafichoni Mahdi anayetokana na Familia yangu. hata kama
itakuwa imebaki siku moja ya maisha haya ya ulimwengu atapigania Haki na usawa
katika ardhi hii na ataondoa ufisadi na ukandamizaji. (Musnad Ahmad Ibn Hanbal,
juzuu ya 1, uk. 99).
Walau
itabaki siku moja kabla ya kiama, bado Allah atampeleka mtu kutoka katika
familia yangu atakayepigania kusimamisha haki na usawa, hata kama ukandamizaji
huo utakuwa umeenea kiasi gani katika ardhi.(Abu Dawood).
.
Masih aliyeahidiwa atatoka katika ukoo wangu katika nasaba ya Fatima(Binti wa
Mtume). (Sunan Ibn Majah, juzuu 2., hadithi na. 4086.
.
Mahdi ni mmoja kati yetu, ni miongoni mwa Ahlul Bayti. (Sunnan Ibn Majah, juzuu
2, hadithi na. 4085.
Kwa
mujibu wa hadithi nyingi sahihi na zinazokubalika za Mtume(s.a.w) Imam Mahdi
ameelezwa:
1. Atatokana na ukoo wa Mtume(s.a.w) na kizazi cha Fatima
2. Atakuwa na uso wa bapa na pua ya kuchongoka
3. Atatokea usiku mmoja
4. Atakuja muda mfupi kabla ya kiama
5. Atafanana jina na Mtume(s.a.w)
6. Atakimbia kutoka Madina kwenda Makka ambako watu watampokea na kula kiapo
mbele yake
7. Atapokea kiapo na kuwasaidia watu wa Iraq
8. Atapigana vita.
9. Ataongoza sehemu kubwa ya Waarabu kwa mujibu wa sunna kwa muda wa miaka
saba
10. Ataeneza haki na usawa katika ardhi
11. Ataondoa ufisadi na ukandamizaji
12. Hatakuwa yule masihi aliyeahidiwa
Je Mirza Ghulam Qadian alifikia
vigezo na kukamilisha majukumu haya?
Hadithi
zinazoelezea juu ya ujaji wa Issa bin Maryam
Mirza
amedai kwamba yeye ndiye Masihi aliyeahidiwa yaani Issa bin Maryam aliyebashiriwa
na Mtume(s.a.w) atakayekuja kabla ya siku ya kiama. Alikuwa
sahihi kwa madai yake haya? Hebu tutazame Mtume(s.a.w) amesemaji kuhusiana na
hili:
"Naapa
kwa yule mikono yake inamiliki uhai wangu, Mwana wa Maryam(Issa) atatoa
Talbiya(Labbaika Allahumma Labbaika) kwa ajili ya Hajj, au Umra au yote kwa
wakati mmoja katika mlima wa Rawha."(Sahih Muslim, kitabu cha 7, Na.
2877).
Mwenyezi
Mungu atamtuma Masih Ibn Maryam. Atashukia jirani na mnara mweupe wa mji wa
Damascus, akiwa amevaa shuka mbili
za njano, akiwa juu ya mabega ya malaika wawili.(Sahih Muslim, juzuu ya 8. uk. 192-193.
Masih atakufa baada ya kukamilisha muda aliokadiriwa
kuishi hapa duniani na Waislamu watamswalia na kumzika jirani na kaburi la
Mtume, Abubakar na Omar."(Mishkat, uk.480).
Mujammi Ibn Jariya al-Ansar ameeleza kwamba alimsikia
mtume(s.a.w) akisema: Mwana wa Maryam atamuua mpinga Kristo(Dajjal) katika
lango la Ludda.(Tirmidh na Ahmad).
Kwa
mujibu wa hadithi hizi sahihi yafuatayo yanafahamika:
1.
Masihi aliyeahidiwa si
mwingine ila ni Issa bin Maryam
2.
Atakuja kuwa miongoni mwa
Waislamu, atashukia jirani na mnara mweupe ulioko Damascuss, Syria, akiwa
amejigubika shuka mbili za njano akiwa katika mabega ya malaika wawili.
3. Ataswali nyuma ya Imam Mahdi
4.
Atapambana na kumuua Dajjal
katika lango la Ludd;
5.
Masiha atatawala na kuongoza
dola ya kiislamu kwa mujibu wa sharia ya Qur'an
6.
Watu wa kitabu watakiri kuwa
Issa ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na watasilimu(4:159), watavunja misalaba na
jizya kwao itaondolewa.
7.
Atapambana na Yaajuj na Maajuj
na atashinda vita hivyo
8.
Uislamu na Haki vitatawala,
ukandamizaji utaondoshwa na vita sehemu mbali mbali vitamalizwa.
9.
Kila mtu atapata kipato
kinachomtosha na chuki, wivu na tamaa vitafutika
10. Masih atahiji au atafanya Umra
11. Atakufa baada ya kuishi duniani kwa muda wa miaka 40
na atazikwa jirani na kaburi
la Mtume. Kuja kwake kutakuwa alama mojawapo ya kiama.(43:61).
Je Mirza ametimiza masharti haya ambayo Mtume ameapa kuwa yatatokea.
Je, Mirza Ghulam Ahmad alikuwa;
Mtume au Masih aliyetabiriwa au Imam Mahd?
Mirza
hakuwa Mtume au Mahdi wala Masih aliyetabiriwa bali alikuwa:
.
Mtoto wa Chirag Bibi, na si mtoto wa mwana wa Maryam
.
Hatokani na ukoo wa Mtume(s.a.w)
.
Hakupata nafasi ya kutawala nchi na kusimamisha haki.
Mirza
Qadiani anakiri mwenyewe:
."Sijadai kwamba mimi ni Mahdi
atakayekuja ambaye atatokana na ukoo
Fatima"(Braheen-e-Ahmadiyya V. Roohani Khaazin
juzuu ya 21 uk. 356).
."Tunakiri hivi kwa sababu huenda
wakaja Mahdi wengi siku za usoni na huenda mmoja wao akawa na jina la Imam Muhammad."(Roohani
Khazain
juzuu ya 3 uk. 197).
."Inawezekana
na kwa hakika muda fulani huko mbeleni atakuja mtu Takayeitwa Masih
ambaye
ni yule aliyebashiriwa na Mtume, kwa sababu mimi siku mtawala na
sikuwa na amri
katika ulimwengu huu bali nilikuwa fukara na mnyonge.
."Huenda wakaja Masih zaidi ya 10,000
na wa kweli akawa yule atakayeshukia Damascuss.(Izala -e-Auham), Roohani Khazain juzuu ya 3
uk. 251).
Kwa hiyo Mirza alijijua kwamba yeye si Imam Mahdi wala mcha Mungu yeyote
aliyebashiriwa na Mtume, licha ya hivyo wafuasi wake wameendelea kusisitiza
kwamba alikuwa Imam Mahdi. Na kama kweli alikuwa Imam Mahdi basi alishindwa
kutimiza majukumu aliyotakiwa kuyafanya kwa mujibu wa hadithi. Licha ya kujua
kwamba madai yake yanapingana
kabisa na mafunzo ya Mtume Muhammad, tamaa ya ya kishetani ilimsukuma Mirza
afumbie macho dhambi kubwa aliyokuwa akiitenda. Alihalalisha madai yake kwa
kusema:
"Msingi wa madai yetu sio Hadithi, ni Qur'an na
Wahyi niliokuwa nikiupokea. Ndio, na katika kuthibitisha hili ningeonesha
Hadithi ambazo kwa mujibu wa Qur'an hazipingani na Wahyi wangu. Hadithi
nyingine nazitupilia mbali kama karatasi isiyohitajika."(Roohani Khazain juzuu ya 19. uk. 140).
Ni wazi kabisa mwasisi wa kundi la Ahmadiya ametoa madai yanayopingana
kabisa na Quran. Maulamaa wa Makka, Madina, Cairo na Ulimwengi mzima wa
kiislamu wametangaza ya kuwa hawa ni Murtad na kwa hivyo ni Makafiri si
miongoni mwa makundi ya kiislamu. Mirza na wafuasi wake ni waasi wanaotakiwa
kupigwa vita na Waislamu wote duniani. Mirza alikufa miaka 100 na kidogo
iliyopita lakini wafuasi wake wangalipo wanaendelea kudanganya watu kwa jina la
Uislamu.
Ujinga unaotokana na kukosa mafunzo sahihi ya Uislamu na mafunzo potofu
ya Mirza Ghulam Ahmad ni matunda
ya harakati za wamishenari. Ni jukumu la kila Muislamu kuulinda Uislamu dhidi
ya udanganyifu wa Murtadi hawa. Muislamu asikubali kutumbukia kwenye uongo wa
Ahmadiyya kwa sababu ya ujinga.
Mafunzo ya Uislamu yako bayana, afanye hima kuyajua. Ifahamike kwamba mtu
anapoamua kujiunga na Murtadi hawa ajue amekufuru. Ukweli uko bayana na uongo
uko bayana. Hakuna kulazimishwa mtu katika mas'ala ya dini.
Mwenyezi
Mungu awalinde Waislamu kutokana na ukafiri unaoenezwa na harakati za Ahmadiyya
kwa kuyapotosha mafunzo ya Uislamu.
Ewe Mwenyezi Mungu warejeshe kwenye Uislamu Waislamu
waliozugwa na Uhamadiyya. Wawezeshe kulijua lipi la kweli na lipi la uongo na
wape hidaya ya kufuata njia iliyo sahihi. Amiin.
Wamaa alaina illal balaagh
Hatukuwa sisi ila wafikishaji
Wassalaam alaykum
Kundi la Harakati za kupinga Uhamadiya
P.o.Box 11560
Dibba, AlFujaira
Muungano wa Falme za Kiarabu